Kulikoni Kimara Suka na bomoa bomoa?

Kulikoni Kimara Suka na bomoa bomoa?

Kwanza TV

Member
Joined
May 2, 2017
Posts
33
Reaction score
69
Ilikuwa ni simanzi na vilio kwa wakazi wa Kimara Suka wiki iliyopita baada ya baadhi ya nyumba kubomolewa na watu wanaodaiwa kutoka TANROADS.
Wakazi tuliowahoji walionyesha kusononeka na pia kukata tamaa huku wengi wakikiri hawana pa kwenda na wamelazimika kulala nje na familia zao. Kwa mujibu wa wakazi hawa, wao walienda mahakamani na kesi bado iko mahakamani hivyo kitendo cha kuwabomolea kimewakuta hawajajiandaa kwani wanasubiri hukumu.



Kwanza TV imewasiliana na TANROADS ili kupata majibu kwa upande wa serikali kuhusu ubomoaji uliofanyika na tutaendelea kuwapa taarifa zaidi
 
Kama kweli tunahitaji kuibadilisha Dar na kuwa mji wa kisasa nilazima tukubari hili kufanyika.
Hakuna namna mji huu umejengwa hovyo hovyo
Anaye pinga hatumii Akili anaangalia Leo siyo Kesho
 
Kama kweli tunahitaji kuibadilisha Dar na kuwa mji wa kisasa nilazima tukubari hili kufanyika.
Hakuna namna mji huu umejengwa hovyo hovyo
Anaye pinga hatumii Akili anaangalia Leo siyo Kesho


Hakuna mtu anayepinga maendeleo, tatizo ni serikali inapochukua ardhi za wananchi na kuharibu mali zao kwa nguvu bila fidia. Kumbuka halali ya serikali ni mita 61 tu na hizo ililipa fidia, mita zingine 61 bado hawajalipa fidia ya ardhi na majengo. Sasa hivi munashangilia serikali ikidhulumu wananchi hawa lakini kumbuka kuwa HAKI ya mtu inacheleweshwa na kamwe haipotei.
 
Wabomolewe tu haiwezekani jiji kubwa kama dar lina kabarabara kembamba namna hiyo kutoka mikoani, leo watu wanalalamika lakini baada ya miaka 10 ndio wataona matunda ya ubomoaji huu. Nawakumbusha pia wakazi wa kuanzia ubungo maji hadi kimara mwisho, mita hizo 121.5 zinawahusu tafteni mapema kwa kuhamia msije mkaanza kulia na nyie
 
Kama kweli tunahitaji kuibadilisha Dar na kuwa mji wa kisasa nilazima tukubari hili kufanyika.
Hakuna namna mji huu umejengwa hovyo hovyo
Anaye pinga hatumii Akili anaangalia Leo siyo Kesho

Aliyekwambia kuondoa hovyo hovyo ni kutanua barabara tu ni nani?? Kwani hakuna alternative zingine za kufanyika juu ya upanuzi wa hizo barabara??

Mji ulipangwa vibaya, tunakubaliana, lakini ni nini hatma ya hizo familia ambazo miaka nenda rudi walikuwepo hapo wao na wajukuu zao?? Je ni kuwabomolea na kuwaacha wanalala nje na wajukuu zao?? Umewapa maeneo mengine wamekataa kwenda??

Yote haya ni hiki chama na uzembe wetu wa watanzania kila mmoja kwa nafasi yake. Kuna mkenya alipata niambia, TZ hata na ng`ombe tunaweza ongozwa. We dont ask. Hivi sawa, vile sawa.

Halafu we uliyebahatika kuiona kesho utuambie kama umeona kuna changes zozote au ndiyo tunaendelea kupigwa tu.

Kila mmoja apambane na hali yake. Poleni wakazi wa morogoro Rd.
 
UPDATE:
Tulitaka kujua kutoka Waziri wa Ardhi William Lukuvi kama wananchi wanabomolewa wana hati miliki halali inayotambuliwa na Wizara yake, basi inakuwa vipi leo wanabomolewa bila fidia na kuitwa wavamizi?
Lakini Waziri alikataa kuongelea hili suala la Bomoabomoa bila kusikiliza swali

 
Back
Top Bottom