Kama Hii Ndio Situation ya Bomoa Bomoa ya Ubungo na Kimara Bila Fidia, Then Faraja Pekee ni Kuwa, Watafidiwa Tuu!.


Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,216
Likes
30,059
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,216 30,059 280
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kuwafariji, watu wote waliokumbwa na bomoa bomoa popote pale bila fidia, japo hiyo bomoa bomoa katika baadhi ya maeneo, imefanyika kwa dhulma kubwa, ikiwemo kupuuzwa kwa zuio la mahakama, then waathirika na wahanga wa bomoa bomoa hii, wasiwe na wasiwasi, kwa sababu mwisho wa siku, wote watafidiwa, ila fidia hiyo sio lazima ifidiwe sasa italipwa tuu hata mbele ya safari.

Kwa vile sisi binadamu wote tunaoishi humu duniani, tunasemekana, tuko safarini tuu, mambo yote tunayokutana nayo ni mapito tuu ya dunia hii, na yote huishia mwisho wa safari yetu katika makao yetu ya milele.

Baada ya kusikia hadi jengo la Tanesco litabomolewa bila fidia, na ile miundombinu ya DRT pele Ungo iliyogharimu mabilioni ya shilingi kwa fedha za mkopo, nayo pia itabomolewa ma kujengwa upya, then nimepitia historia ya hii bomoa bomoa,

TUKIREKEA KWENYE MAMBO YA SHERIA
Bomoa bomoa holela aliyotangaza Waziri wa Miundo Mbinu Mhe John Magufuli kati ya Ubungo hadi Kiruvia haijawahi kuwa na uhalali wowote wa kisheria tokea mwaka 2001 alipoagiza mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara kupandwa kinyemela Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi. Hii ni kutokana na na wananchi hao hadi leo hii ikiwa ni miaka 9 hawajapatiwa fursa ya kusikilizwa kuwa waliipataje ardhi ambayo yeye anadai ni hifadhi ya barabara baada ya wao kuishi hapo kwa zaidi ya miaka 30.
Wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi Mhe John Magufuli alidai kwa mbwebwe ya hali ya juu kuwa nimeagiza kupandwa kwa alama hizo kwa mujibu wa ibara ya 4 ya Kanuni za Sheia ya barabara Tangazo la Serikali namba 161 Tar 05/05 1967 inayotaja upana wa hifadhi ya barabara kati ya Ubungo hadi Kibaha ni Futi 300 hadi 400. Maskini kumbe Ibara hiyo iliposhateza uhai baada Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha kwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 ambayo iliwekwa sahihi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 15 Mei 1999 ili kuanza kutumika kama sheria.
Vifungu 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 vinatamka kuwa:-

Historia inaonyesha kuwa ujenzi wa barabara iliyokusudiwa na sheria ya barabara ya 1967 anavyotumia Mhe John Magufuli ulikamilika mwanzoni mwa miaka 70, katika kipindi hicho Serikali ya awamu ya kwanza ilitekeleza sera ya operesheni vijiji nchi nzima. Katika eneo kati ya Ubungo na Kibaha vilianzishwa vijiji vya ujamaa vilivyoitwa Kimara, Mbezi, Kwembe, Kibamba na Kiruvia. Wakati wa ugawaji wa ardhi kwa wanavijiji mamlaka iliyohusika kugawa ardhi kwa mujibu wa sheria yaani halmashauri za vijiji hazikuwa na utambuzi wa ibara hiyo na kwa kuwa kazi ya eneo la ziada lilotengwa kati ya Ubungo hadi Kiruvia ilikamilka baada ya ujenzi wa barabara ugawaji wa ardhi ulizingatia hifadhi ya Futi 150 tu. Zoezi la ugawaji wa ardhi ndani ya vijiji vilivyoanzishwa lilikuwa chini ya usimamizi wa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Wilaya n.k.
Kwa zaidi ya miaka 30 kutokea kuanzishwa kwa vijiji vya Kimara, Mbezi, Kwembe,Kibamba na Kiruvia hakuna mamlaka yoyote au kiongozi aliyepinga uwepo wa wananchi katika eneo hilo hadi 2001 Mhe John Magufuli alipoagiza mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara kuwekwa kinyemela Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi kati ya Ubungo hadi Kiruvia. Hata Master Plan ya Jiji la Dar es Salaam iliyotayarshwa miaka ya 1970 inatambua kuwa upana wa hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Kibaha ni Futi 150 tu na ndio ilitumika kuwawezesha mamia ya wanavijiji na wananchi waliokuwa wakimiliki ardhi katika vijiji hivi kumilikishwa ardhi yao kwa kupatiwa hati miliki.
Kwa msingi huo ni upotoshaji wa haia ya juu kwa kiongozi mwandamizi kama Mhe John Magufuli kudai kuwa wananchi waliohamishiwa katika vijiji vya ujamaa ni wavamizi wa hifadhi za barabara.
Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheia ya barabara-Tangazo la Serikali namba 161 la Tar 05/05 1967 inatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara zote kuu hapa nchini (Trunk Roads) utakuwa ni Futi 75 kila upande. Ibara ya 29 (1a, b) ya Kanuni za Sheria ya Barabara namba 13 ya 2007-Tangazo la Serikali Na 21 la Tar 23 Januari 2009, inatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa barabara zote kuu (trunk roads) ziwe za njia moja (single carriageway), mau njia mbili (dual carriage ways) utakuwa ni Mita 60 tu, yaani Mita 30 kila upande wa barabara.
Kwa mujibu wa sheria ya barabara ya 1967 eneo linalotosha na kuhusika kwa upanuzi wa barabara katika barabara zote kuu (Trunk Roads) lilikuwa ni Futi 150 kwa sheria mpya ya mwaka 2007 ni Mita 60 yaani Mita 30 kila upande. Ibara ya 27 Kanuni ya mpya inatamka kuwa upana wa chini kabisa wa njia moja ya barabara katika barabara kuu (Trunk Roads) utakuwa si chini ya Mita 3.25.
Hivyo upana wa hifadhi ya barabara wa Futi 150 wa 1967 unao uwezo wa kuzalisha njia za barabara 14 kwa maana ya njia 7 za kuelekea Kibaha na 7 za kuja Dar. Aidha upana wa hifadhi ya barabara uliowekwa na sheria mpya ya barabara ya 2007 wa Mita 60 unao uwezo wa kuzalisha njia za barabara 18 yaani 9 za kuelekea Kibaha na njia 9 za barabara za kuja Dar. Hivyo Mhe John Magufuli hana sababu zozote za msingi za kulazimisha nyumba zilizoko nje ya Mita 30 kila upande wa barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia kubomolewa kwa kuwa hazina uhusiano wowote na msongamano wa magari na hazizuii kwa namna yoyote ile upanuzi wa barabara hiyo.
Kinyume na madai ya Magufuli, tovuti ya TANROAD inaonyesha kuwa licha ya tatizo la msongamano wa magari hakuna mpango wowote wa kupanua barabara kati ya Kimara hadi Mlandizi kwa sasa. Hivyo hakuna sababau zozote za msingi kuhalalisha ubomoaji wa nyumba zilizoko nje ya eneo halali hifadhi ya barabara la Mita 30 kila upande bila ya wananchi kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria.
Hivyo madai ya upotoshaji wa umma ya Waziri wa Wizara ya Miundo Mbinu Mhe John Magufuli kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro unasababishwa na wananchi waliojenga nyumba nje ya eneo halali la hifadhi ya barabara la Futi 150 au Mita 45 hayana msingi wowote, Nia yake ni kutumia tatizo hilo na ujenzi wa barabara za mradi wa mabasi yaendayo kasi kuwawekea alama za X wananchi wenye nyumba nje ya eneo halali la hifadhi ya barabara la Futi 150 au Mita 45 kati ya Ubungo hadi Kimara.
Kutokana na njama za aina hii za kuwakoseha wananchi haki zao kwa makusudi alizoanzisha Mhe John Magufuli mwaka 2001, eneo kati ya Ubungo hadi Kibaha lilidumazwa kiuchumi baada ya wamiliki wa ardhi iliyoko kati ya Mita 45 hadi 120 kushindwa kulitumia kiuchumi. Hali hiyo imesababiisha wananchi kupoteza nafasi za ajira, kujiajiri na kujikimu kimaisha na hivyo umasikini kuongezeka kwa kasi sana. Kukosekana kwa huduma kama vile za kibenki, maduka makubwa, ATM n.k tofauti na maeneo mengine yaliyopitiwa na barabara kuu kama vile barabara ya Bagamoyo, Kilwa n.k ni mifano halisi ya umaskini ulioletwa na matumizi mabaya ya madaraka ya Mhe John Magufuli.
Kati ya 2001 hadi 2010 Mhe Charles Keenja alipokuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo alishindwa kutilia maanani malalamiko haya ya idadi kubwa ya wananchi wanaoishi ndani ya eneo la ukubwa wa Mita 100 kila upande wa barabara kutokea Ubungo hadi Kiruvia. Ongezeko kubwa la wakazi na mahitaji ya huduma mbali mbali vikapeleeka kuongezeka kwa hasira za wananchi dhidi ya CCM. Itakumbukwa kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Jimbo la Ubungo walijitokeza kujiandikisha, kupiga kura, kuwa mawakala na hatimaye kulinda kura za mbunge katika kituo cha kujumlisha matokeo.
Ni imani yangu kuwa baada ya Waziri Mkuu kuchkua hatua za kufaa baada ya kupokea malalamiko wapiga kura wa Jimbo la Ubungo watakuwa wamefarijika na kutambua kuwa sio viongozi wote wa CCM wana tabia kama za mbunge wao wa zamani za kutelekeza wananchi au zinzopfanana na huyu mbomoaji holela wa nyumba zao.
Ni imani yangu kuwa bado nafasi ipo ya kutumia busara na hekima kama ile iliyotumika mwaka 2001 wakati wa upanuzi wa barabara ya Dar-Mlandizi ambapo nyumba zilizoguswa ni zile tu zilizoko katika eneo linalohitajika kwa upanuzi kwa wakati husika tu. Ndio maana hata leo zipo nyumba zilizobomolewa nusu, robo, uzio tu n.k Busara hii itawezesha barabara ya Morogoro iweze kupanuliwa bila kusababisha wakimbizi wa ndani (internally displaced persons) kwa kuwa makosa yalikwishafanyika huko nyuma hususana kwa uande wa serikali yenyewe katika operesheni vijiji.
Ushauri kwa Mhe Mizengo Pinda ni kuwa tabia ya ung'ang'anizi usiokuwa na msingi wa Mhe John Magufuli imesababisha yakafanyika makosa wakati wa utungwaji wa Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 ambapo Kanuni ibara ya 29 (2) imeshindwa kuzingatia mahitaji ya vifungu vya 15 na 16 vya sheria ya Ardhi ya Vijiji kwa kunukuu ibara ya 4 ya Kanuni za mwak 1967 huku ikupunguza kidogo eneo la hifadhi ya barabara kutoka Mita 120 hadi 60 tu kila upande. Ilikuondoa kabisa mgogoro ibara 29 (2) iondolee kabisa na kubaki Ibara 29 (1) ambayo inataja hifadhi ya barabara ya nchi nzima kuwa ni MIta 60, yaani Mita 30 kila upande.
Kunukuliwa upya kwa ibara ya 4 ya Kanuni ya 1967 katika Knuni mpya tafsiri yake ni kuwa sasa (2009) Serikali inataka kuitwaa upya ardhi iliyopo kati ya Mita 30 hadi 120 kutoka katika ya barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia hivyo inawajibika kuwalipa fidia wananchi waliopo ili waondoke na kuacha hifadhi ya barabara yenyae upana wa Mita 120 kutoka katika ya barabara ili kumridhisha mtu mmoja mbaye ni Mhe John Magufuli.
Nimejiridhisha ni kweli kabisa hii bomoa bomoa, haitendi haki katika baadhi ya maeneo, hivyo faraja pekee kwa waliobomolewa Ubungo na Kimara na kwinginepo bila fidia, ni kuwa, hatimaye wote watafidiwa tuu, hata kama fidia hiyo sio sasa, then watafidiwa mbele ya safari, na wakati huo huo, hao waliowatenda nao pia watalipwa haki yao stahiki zao kwa mujibu wa matendo yao, malipo ni hapa hapa duniani au mbele ya safari.

Fidia hiyo itapatikana kupitia hukumu pekee ya haki hapa duniani inayoitwa hukumu ya karma.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili ...
Poleni sana!.
Paskali
 
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
21,598
Likes
63,402
Points
280
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
21,598 63,402 280
Aiseeee umefikia hapo!!!
Itabidi nikae vizuri nikusome uliyoandika nimechungulia tu sentensi mbili tatu..
 
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Messages
5,175
Likes
5,597
Points
280
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2010
5,175 5,597 280
Mkuu kuna mambo yanafanya watu weusi tuonekane wahovyo hovyo sana..

Jengo hili linauhusiano wa moja kwa moja na serikali lakini limejengwa kwenye hifadhi ya barabara, upande mwingine kuna wizara ya serikali nayo iko ndani ya road reserve, upande mwingine ni hiyo miundombinu ya DRT nayo ni ya kubomolewa..Pembeni ya makao makuu ya Tanesco nako kuna 100MW power plant nayo sijui tunaifanyaje..

Hivi wakati vyoote hivi vinajengwa serikali ilikuwa haina plan ya miundombinu ya nchi na upcoming projects kwenye maeneo haya, hivi tunawezaje kuchezea hela za kodi za wananchi kiasi hiki??
Katika hali hii kweli kuna mtu atakuwa tayari kuja kuwekeza mamilioni ya hela maana hatuaminiki na kesho yetu hatuijui kama taifa...
 
BAFA

BAFA

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2011
Messages
2,699
Likes
4,028
Points
280
BAFA

BAFA

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2011
2,699 4,028 280
Kitu kimoja kwa mh raisi magufuli nia yake njema(kama anavotaka tuamini hvo) isije ikajaleta athari na hasara kwa taifa baadae na naamini yeye atakuwa liable kwa hili. Hebu kuwa msikivu na mwenye huruma juu ya hili la bomoabomoa
 
tweenty4seven

tweenty4seven

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2013
Messages
8,204
Likes
6,171
Points
280
tweenty4seven

tweenty4seven

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2013
8,204 6,171 280
Inauma sana, kukiuka maksudi sheria na zuio la mahakama, natamani hapa kwetu pia tungempata Gen. Constantino Chiwenga mwingine. Hii ingesaidia kuwashikisha adabu wanaosigina katiba na sheria za nchi.
Ukweli mchungu huo
 
Copenhagen DN

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Messages
6,071
Likes
8,343
Points
280
Age
29
Copenhagen DN

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2014
6,071 8,343 280
Pasco huyu jamaa kweli jamani Hana PTSD? There is something wrong with this dude, he has a serious mental shakeup am sure about. Tufukunyue his past there is something. Dr Kitila Mkumbo saidia mtu wako bana ishu za maji siyo zako
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,491
Likes
117,407
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,491 117,407 280
Any person with a mental case is not fit to lead any country in this World.

Pasco huyu jamaa kweli jamani Hana PTSD? There is something wrong with this dude, he has a serious mental shakeup am sure about. Tufukunyue his past there is something. Dr Kitila Mkumbo saidia mtu wako bana ishu za maji siyo zako
 
Horseshoe Arch

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Messages
11,662
Likes
5,559
Points
280
Horseshoe Arch

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2009
11,662 5,559 280
Any person with a mental case is not fit to lead any country in this World.
Bush Jr, Trump wote wana bipolar disorder na bado wamekuwa watawala wa dunia...YES ukitawala marekani umetawala dunia...namwonea tu huruma babu yangu wa 'Shimbabwe'
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,491
Likes
117,407
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,491 117,407 280
What is going on in America is a very good example that there are some people in this World who are unfit to lead anything let alone to lead the country.

Bush Jr, Trump wote wana bipolar disorder na bado wamekuwa watawala wa dunia...YES ukitawala marekani umetawala dunia...namwonea tu huruma babu yangu wa 'Shimbabwe'
 

Forum statistics

Threads 1,237,184
Members 475,465
Posts 29,280,589