Kulikoni ITV kutotangaza habari za Simba SC? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni ITV kutotangaza habari za Simba SC?

Discussion in 'Sports' started by MzeePunch, Mar 15, 2010.

 1. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimeshangazwa na kitendo cha ITV kutotangaza michezo ya Simba SC hata kwa tukio kubwa kama la kutwaa ubingwa wa Vodacom Premier League. Nimeambiwa eti wamewanunia viongozi wa Simba kwa sababu waliwakatalia kurusha 'live' moja ya mechi zao. Kwa maoni yangu huo sio uamuzi sahihi. Ni 'very unprofessional', inabidi ITV wajirudi kabla ya kupoteza umaarufu. Watambue kwamba Simba ni klabu kubwa na ina wapenzi wengi ndani na nje ya nchi. Great Thinkers wengine mnalionaje hili?
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ITV ni chombo chenye kuendelezaa chuki pia katika jamiii?? Siamini ITV yaweza kuwa na ugomvi na SSC labda kuna watu ndani ya ITV na SSC wenye chuki zao binafsi na kuziingiza katikaa taasisi zao.

  Kama ni kweli basi kosa kubwa kwa chombo cha kuheshimika kama ITV.
   
 3. m

  mob JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  kipekee jana sikubahatika kuangalia taarifa ya habari ila leo nimeturn niaangalia magazeti ikawa ivo ivo hawatangazi hata kwenye siku za nyuma ilikuwa ivo ivo.huu unaweza kuwa ni chuki binafsi na pia inaweza ikaleta shida siku za mbeleni.
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mmmmh labda kulikuwa na habari zingine muhimu zaidi kiasi kwamba muda haukutosha kuingiza habari ya SSC.....au hata pengine waandishi wao wote wa michezo walikuwa kwenye bonanza la wiki ya NSSF ambapo team ya IPP (The Dream Team) ilikuwa ikipepetana na timu ya Wizara ya habari na hivyo kutotuma ripota wao katika mchezo wa SSC na Azamu FC (wana ramba ramba).

  Wana Simba mmekereka?...kama vipi lipieni kipindi maalumu ITV ili wawarushe kwa saa nzima.

  Otherwise sioni kama kuna chuki binafsi.......mbona hata ushindi wa Man U wa jana ITV hawakutangaza? Au pia wana ugomvi na viongozi wa Man U???
   
 5. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mhh kazi ipo.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  midomo hiyo:D:D:D
   
 7. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Mimi binafsi huwa siangalii michezo ITV kwa sababu huwa ni wachovu sana kwenye eneo hilo. Lakini jana nikiwa bar wakati taarifa ya habari ya saa 2 ikiwa hewani ilipofika wakati wa michezo hawakutangaza chochote kuhusu Simba. Nikaambiwa hao (ITV) wana bifu na Simba hivyo huwa hawatangazi habari zao. Wao habari kubwa ya michezo ilikuwa timu yao ya IPP kuifunga timu nyingine kwenye michuano ya Kombe la NSSF. Ilibidi jamaa wahamie Star TV ambako walitangaza habari za Simba. Sidhani kama ni vema kuendekeza chuki na kisasi kwenye vyombo vya habari kama TV.
   
 8. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli hata mimi nilishangaa jana hawakutangaza kabisa habari hizo. Nikabaki kuchungulia TBC1 kwa sababu walisema kwenye muhtasari. Kitenge naona kazeeka vibaya. Labda wakuwa wao wamekataza.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Diagnosis = Myopia!! just seek for therapeutic intervention!!!
   
 10. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mwanzoni walikuwa wanatangaza kwa kuwa walikuwa wanapata maslahi yao kama vile kupitia matangazo ya mechi. Sasa hivi hawatangazi kwa kuwa hawapati maslahi makubwa. Ujumbe huo huo wanaupeleka kwa waandishi wao individually, kwamba kama kuna mshiko (bahasha) leteni habari kituoni itangazwe vizuri. Kama hakuna mshiko (bahasha) msiilete habari kituoni (hata kama ni nzuri). Similarly, this applies kwa habari isiyo nzuri/iliyo mbaya. Kama kuna mshiko basi utolewe ili habari mbaya isitangazwe, kama hakuna mshiko basi habari mbaya itatangazwa. So, generally wanatupa picha kwamba maslahi binafsi kwanza, halafu baadaye maslahi ya taifa (kama wakipenda). HII NI RUSHWA kwa kuwa mwandishi/kituo cha matangazo hakiwajibiki equally eti kwa kuwa kilinyimwa fursa ya pesa!
   
 11. K

  Kinnega Member

  #11
  Mar 15, 2010
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio swala la "Wana Simba mmekereka," ni swala zaidi la kiufundi/kikazi kuhusu uandishi habari nchini:
  Jana habari muhimu kuliko zote nchini kimichezo ilikuwa ni kuna timu imeshinda ubingwa, haijalishi ni ipi, kuna mechi iliyoamua klabu bingwa itakayoiwakilisha Tanzania kimataifa. Utaachaje kuiripoti?

  Badala yake wanaonyesha mmiliki wa stesheni akitembelea timu yake ya IPP kwenye kombe la mbuzi la NSSF. Ndio "habari muhimu zaidi" unayoisema hiyo? Wiki chache zilizopita wakatumia masaa kutwa wanatuonyesha pati ya kufunga mwaka ya IPP na wanavyocheza mziki na kula na kunywa, nani anataka kuona pati yao?

  Ni maadili ya kiuandishi, kwamba unaandika wanachojali watazamaji, sio mmiliki na pati zake.
  Ushawahi kumuona R. Murdoch kwenye TV? Ushawahi kuona pati ya wafanyakazi wa CNN kwenye TV ? Kamwe!

  Bora TBC walitupa mpango mzima mpaka jinsi polisi walivyomnusuru Sheikh Yahaya kutoka kwa wananchi wenye hasira waliozingira nyumba yake kwa kubashiri uongo kuwa Simba ingefungwa na Azam. Japo kwa Waziri Mkuchika nako "the revolution will not be televised."
   
 12. Arsenal

  Arsenal Senior Member

  #12
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ITV wanashindwa kuelewa kitu kimoja simba kama simba hawapati hasara yoyote kwa kutotangazwa na ITV ila nimeona watu wengi sana cku izi wanatune star tv kwa ajili iyo so ITV bila ya wao kujua wanazipa promo their own competitors!! mi binafsi sikuwa naangalia Star Tv but baada ya kutaka kujua jana simba ilikuaje uwanja wa taifa nikatune Star Tv na nimeipenda they have good coverage not only in sport ata other news so watu kama mimi nadhani tutakuwa wengi and thats the reason ITV are promoting their own competition!!haimake sense Nipashe waandike news za Simba but ITV wasi broadcast to me its childish thinking......sio kama tunaangalia ITV anyways!!!
   
 13. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
   
 14. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
   
 15. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwani CNN ndo benchmark ya perfection ama professionalism? Mambo mangapi ambayo hasiyo na interest na matakwa ya wamarekani tunayaona hayatangazwi na CNN?

  ITV sio chombo cha kwanza kususia kutoa habari za taasisi ama mtu fulani......je umesahau mwaka juzi jinsi ambavyo jukwaa la wahariri lilivyoshawishi vyombo vya habari hapa nchini kususia kutangaza habari za Waziri wa Habari na Utamaduni Mh. Mkuchika?

  Haya mambo yanatokea dunia nzima....fuatilia yanayoendelea Indonesia sasa hivi utabaini ninachokizungumza.
   
 16. N

  Nanu JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ilianza wakati viongozi wa Simba walipotaka kuyavunja vifaa vya kurushia matangazo vya ITV uwanja wa uhuru. Simba waliwazuia waandishi kutangaza habari ya simba siku ile na kuanzia hapo ITV hawakujishughulisha tena na Simba. Wamesusa!!!!! Nadhani uongozi wa TFF inabidi kufanyia kazi hili ili timu zetu zipate kuonekana zikicheza na umma uhabarishwe vizuri.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ukisikia kufulia ndio huko jamani
   
 18. I

  Irizar JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo Tanzania yetu ya leo. Kila kitu pesa, hapendwi mtu bana hapa.
   
 19. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Sasa kama viongozi wenyewe wa SSC walikataa mambo yao yasitangazwe na vyombo vya IPP, kwa nini ITV ing'ana'ganie kutangaza?Viongozi wanakuwa mbogo hata kutaka kuvunja Camera za ITV pale uwanja wa Uhuru, kisa, mchezo ukioneshwa live mapato yatapungua kwa watu kutokwenda Uwanjani! Je, wale wa mikoani wasioweza kwenda mpirani! Mbona wamecover vizuri tu kwenye magazeti yao ya leo. Kama unahitaji habari za timu fulani, yafaa ugaramie pia(nunua gazeti) au tune station nyingine.
   
 20. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Na kwakuongezea pia, waandishi walimsusia Omari Mapuri hadi wenye nchi wakaamua kumpa ubalozi nje!
   
Loading...