Vigogo wanunua ghorofa bil 2.7 badala ya bil 1.2
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA), kwa baraka za Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo, imenunua jengo la ghorofa moja kwa shilingi bilioni 2.7 badala ya Sh. bilioni 1.19, kama ilivyoshauriwa na Mthamini Mkuu wa Serikali, uchunguzi wa muda mrefu wa Raia Mwema umebaini.
Kwa mujibu huo, unaothibitishwa na nyaraka mbalimbali, Agosti 29, 2011, Menejimenti ya BRELA ililipa Sh. bilioni 2.7, kupitia hundi namba 000340, kwa ajili ya kununua jengo hilo katika kiwanja namba 24 kilichoko Ada Estate, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam ambacho kilikuwa kikimilikiwa na Balozi (mstaafu) Raphael Haji Lukindo ambaye kwa sasa ni marehemu.
Malipo hayo yalifanywa na Menejimenti ya BRELA kwa baraka za Bodi, bila kujali ripoti ya tathmini ya thamani ya mali hiyo kwa kuzingatia bei ya soko kwa wakati huo, tathmini ambayo ilifanywa na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali (CV), baada ya menejimenti ya BRELA kuiomba ofisi hiyo kufanya tathmini.
Katika tathmini yake, Ofisi ya Mthamini Mkuu ilieleza kuwa thamani halisi ya jengo na kiwanja hicho, kwa bei ya soko ni Sh. bilioni 1.19.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Julai 2011, tathmini ya bei ya jengo, kwa bei ya soko, ilikuwa Sh. 132,077,200, wakati thamani ya kazi za eneo husika (site works) ni Sh. 13,207,720 na thamani ya ardhi ilikuwa Sh. 1,044,927,500, na hivyo kufanya jumla ya bei halisi ya soko kwa eneo lote hilo kuwa Sh. 1,190,212,420.
Hata hivyo, Mthamini huyo alipendekeza kiasi hicho chote cha bei halisi ya soko kitamkwe Sh. 1,190,000,000 wakati wa majadiliano ya bei kati ya mnunuzi na muuzaji.
Uchunguzi kutoka vyanzo mbalimbali vya Wakala, unaoungwa mkono na baadhi ya nyaraka, umebainisha kwamba biashara hiyo ya Menejimenti ya BRELA na Balozi Lukindo ilifanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya BRELA kama mnunuzi na Kampuni ya Uwakili ya Godson Nyange iliyomwakilisha muuzaji, Balozi Lukindo.
Aidha, katika uchunguzi huo, Raia Mwema limebaini kuwa fedha hizo Sh. bilioni 2.7 zililipwa kupitia akaunti namba 001001037609260001 iliyoko Benki ya Azania, tawi la Mazido, Dar es Salaam, akaunti inayomilikiwa na Godson Hudson Nyange (Wakili) kwa maelekezo ya maandishi ya mwenye mali, Balozi Lukindo.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa BRELA wakati wa mchakato huo wa kununua nyumba na kiwanja hicho, Esteriano Mahingila, ambaye kwa sasa amestaafu kwa mujibu wa sheria, amekiri BRELA kununua jengo na kiwanja hicho kwa Sh. bilioni 2.7.
Alipoulizwa na Raia Mwema ni kwa vipi kiasi kilicholipwa ni kikubwa karibu mara mbili ya thamani halisi iliyopendekezwa na Mthamini Mkuu wa Serikali, licha ya uamuzi wake (Mahingila) kuiomba ofisi hiyo imfanyie tathimini kabla ya kufikia makubaliano kati ya mnunuzi na muuzaji, alisema "hakukuwa na ulazima wa kufuata ushauri wa Mthamini Mkuu wa Serikali".
"Ni kweli ripoti ya Mthamini Mkuu wa Serikali ilipofanya tathmini, katika maoni yake, ilisema thamani hiyo uliyoitaja (Sh bilioni 1.19), lakini sisi (BRELA) baada ya kufanya utafiti wa majengo mbalimbali tuliyotaka kununua, tulibaini bei ya soko kwa wakati ule, kwa eneo kama lile, ilikuwa hiyo tuliyolipa (Sh bilioni 2.7)... lakini pia ifahamike ripoti ya Valuer ni opinion (maoni) tu, si approval (idhinisho), na kwa hiyo si lazima sana maoni yao yafuatwe."
Namna BRELA ilivyoomba ushauri
Julai 25, 2011, Ofisi ya BRELA, kupitia barua yenye Kumb. Na MIT/RC/OS 168/81, ilimwandikia Mthamini Mkuu wa Serikali ikimuomba kutathmini jengo na kiwanja hicho, chenye hati namba 186038/119, mali ya Balozi Lukindo, kama sheria ya ununuzi wa mali za umma zisizohamishika inavyotaka, kabla ya pande mbili hizo kufikia muafaka wa makubaliano ya mauziano.
Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali baada ya kupokea maombi hayo, ilifanya kazi yake hiyo na kuikamilisha ndani ya muda mfupi wa chini ya mwezi mmoja na kukabidhi ripoti BRELA kama walivyoagizwa, lakini ikipendekeza thamani halisi ya mali hiyo, kwa bei ya soko kwa wakati huo, kuwa ni Sh. bilioni 1.19.
Pamoja na kuwepo ushauri huo wa Mthamini Mkuu wa Serikali, Agosti 29, 2011, ikiwa ni wiki chache tu baada ya kupokea maoni na ushauri wa ofisi ya watalaamu wa tathmini, BRELA, katika barua yake yenye Kumb. Na. MIT/BRELA/BK/104/256, ilimwandikia Meneja wa National Microfinance Bank (NMB), tawi la Kariakoo, Dar es Salaam, kulipa Sh. 2,700,000,000 kwa Godson Hudson Nyange (Wakili na pia Mteja) kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja namba 24 kilichopo Eda Estate, Kinondoni.
"Tafadhali fedha hizo zitoke kwenye akaunti ya matumizi ya BRELA, namba 2041000044 na uzihamishie kwenye akaunti namba 001001037609260001, Azania Bank Ltd, tawi la Mazido, kama nakala ya mauziano iliyosainiwa Agosti 24 iliyoambatanishwa pamoja na barua hii inavyoeleza," inasema barua hiyo ya maelekezo kwa meneja huyo wa tawi la NMB Kariakoo, iliyosainiwa na E.E.Mahingila na T.P. Kadish, Meneja Biashara wa BRELA.
Hundi ya fedha hizo, yenye namba 000340 ilikuwa imeandikwa siku hiyo hiyo ya Jumatatu ya Agosti 29, 2011, na kuwasilishwa benki kwa ajili hiyo, na kwa mujibu wa kumbukumbu za kibenki ndani ya tawi hilo, inaonyesha kuwa fedha hizo zilihamishwa rasmi kwenda kwa mteja huyo siku iliyofuata, Agosti 30, 2011.
Hata hivyo, kumbukumbu zilizopo ndani ya ofisi za Wakala kuhusiana na ununuzi wa jengo na kiwanja hicho zinathibitisha pasipo shaka kwamba, hatua ya BRELA kuomba kufanyiwa tathmini ya mali hizo, ililenga kutimiza matakwa ya kisheria tu kwa sababu makubaliano kati ya muuzaji na mnunuzi yalikuwa yamekwishafikiwa, ikiwa ni pamoja na kuomba na kupata idhini kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo.
Kwa mfano, barua ya Mapunjo inayojibu dokezo la Mahingila la jana yake lililoomba idhini ya Katibu Mkuu huyo kununua kiwanja hicho namba 24, eneo la Eda Estate, kwa kiasi hicho cha fedha Sh. bilioni 2.7 iliandikwa Julai 22, 2011, kwa maana ya siku tatu kabla ya BRELA kumwandikia Mthamini Mkuu wa Serikali ili amfanyie tathmini eneo hilo, barua iliyoandikwa Julai 25.
Inaelezwa na vyanzo vyetu vya habari hizi kwamba kuandikwa kwa barua hiyo kwenda kwa Mtathimini Mkuu wa Serikali kulitokana na msisitizo wa Mapunjo juu ya uzingatiaji wa sheria za nchi katika mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo ambaye, hata hivyo, alishindwa kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa wakati wote na si kuandika tu barua.
Katika barua yake hiyo, Katibu Mkuu huyo, pamoja na mambo mengine aliandika: "Tafadhali rejea dokezo lako la tarehe 21 Julai kuhusu kichwa cha habari hapo juu (ununuzi wa eneo la kujenga ofisi ya BRELA)…ninakubaliana na kuanzishwa na kuendelezwa kwa mchakato wa kiwanja hicho. Aidha, nasisitiza kuwa katika ununuzi huo, taratibu zote za ununuzi zizingatiwe kwa mujibu wa sheria za nchi."
Bodi yafumba macho
Lakini pia hata katika kikao cha Bodi ya Ushauri wa Wizara (MAB), kilichokaa Agosti 18,2011, ambacho ndicho kiliridhia ununuzi huo na kwa bei hiyo ya Sh bilioni 2.7, maelezo ya menejimenti ya BRELA hayakugusia kabisa ushauri wala maoni ya Mthamini Mkuu wa Serikali juu ya thamani halisi ya mali hiyo, ili pengine kikao hicho nacho kiwe na taarifa juu ya tathimini hiyo.
Wakati Mahingila akisema tathmini ya thamani ya mali inayokusudiwa kununuliwa na Serikali au taasisi yoyote ya umma inayofanywa na Mthamini Mkuu wa Serikali ni maoni tu na si lazima yafuatwe, Kaimu Mthamini Mkuu wa Serikali katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Joseph Kleruu, amesema kisheria, Serikali au idara ya Serikali inapoomba kufanyiwa tathimini ya mali inayokusudiwa kununuliwa kwa kutumia fedha za umma, hairuhusiwi kwenda zaidi au mbali ya thamani ya bei halisi iliyopendekezwa na Ofisi yake.
Kwa mujibu wa Kleruu, bei ya thamani iliyotathiminiwa inatakiwa iwe bei dira na kikomo katika majadiliano kati ya mnunuzi na muuzaji, vinginevyo anasema kama mali hiyo ni lazima inunuliwe au kama kuna mazingira yanayolazimisha ununuzi huo ufanyike kwa bei ya juu zaidi ya iliyopendekezwa na Mthamini Mkuu wa Serikali, pengine kutokana na uzuri na umuhimu wa eneo, taasisi iliyoomba kufanyiwa tathimini, inapaswa kurudi tena Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali kuomba ushauri, hatua ambayo BRELA hawakuifanya.
Kwa maelezo hayo ya Kleruu, bei dira na kikomo katika majadiliano ya BRELA na mwenye mali, Balozi Lukindo, kupitia Wakili Nyange na kampuni ya udalali, Ben Consult Ltd-Real Estate Agent, kisheria ilipaswa kuwa Sh. 1,190,000,000.
Kitendo cha BRELA kununua kiwanja hicho kwa Sh 2, 700,000,000 kunaongeza gharama au hasara ya Sh. 1,510,000,000 kutoka tathmini hiyo ya wataalamu wa Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali.
Aidha, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya tathmini ya Julai 2011, kiwanja hicho kina ukubwa wa mita za mraba 4,179.71; huku jengo pekee likiwa limechukua mita za mraba 383.46. Ni kiwanja chenye hatimiliki ya miaka 99 kikiwa kilimilikishwa na Serikali kwa aliyekuwa mmiliki wake wa mwisho, Balozi Lukindo, Oktoba Mosi, 1968 kwa hati (title) namba 186038/119.
"Ni maoni yetu kwamba kwa bei ya soko la wazi (open market value) kwa mali iliyoko kiwanja namba 24, Ada Estate, jijini Dar es Salaam, kwa kuhamisha haki ya umiliki, inafikia thamani ya Shilingi za Kitanzania bilioni moja na milioni mia moja tisini (1,190,000,000) tu," inahitimisha ripoti hiyo ya tathmini ya thamani iliyofanywa na Mthamini Mkuu wa Serikali baada ya kuagizwa na BRELA kufanya kazi hiyo kabla ya manunuzi. Ripoti ilisainiwa na Seleman J. Kassase, Ofisa Tathmini Daraja la Pili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mapunjo, alipotafutwa kuzungumzia suala hili, alisema mtu sahihi wa kulizungumzia ni Mwenyekiti wa Bodi ya BRELA, Profesa Lucian Msambichaka, kwa maelezo kwamba taasisi zote zilizoko chini ya wizara nchini zinasimamiwa na bodi.
Hata alipokumbushwa kwamba ipo barua aliyowaandikia BRELA kubariki ununuzi huo, lakini akiagiza kufuatwa kwa taratibu na sheria za ununuzi, alikiri kufanya hivyo, lakini akasema nafasi ya Katibu Mkuu wa Wizara katika mchakato kama huo, ni sawa na mtu anayebariki mimba ya mtoto, kwani kabla ya mimba kupatikana kuna mchakato unakuwa umefanyika huko nyuma kati ya mama na baba, na kwa hiyo ndiyo amesisitiza atafutwe Mwenyekiti wa Bodi ya BRELA.
Alipotafutwa Profesa Msambichaka, alikiri kufahamu ununuzi wa kiwanja hicho namba 24, Ada Estate kwa kiasi hicho cha fedha, lakini akasema pamoja na ukweli kwamba yeye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya BRELA, lakini katika sakata hili hana lolote la kusema.
"Sasa hapo unanitaka mimi niseme nini? Mimi si Mwenyekiti Mtendaji wa BRELA na wala si Msemaji Mkuu wa BRELA. Kazi yangu ni kuongoza vikao tu. Ninachoweza kusema tu ni kwamba ninafahamu kama BRELA imenunua kiwanja hicho unachokisema na kwa kiasi hicho cha pesa, lakini ukiniuliza kama taratibu za kisheria zilizingatiwa au la, hiyo siwezi kusema," alisema Profesa Msambichaka.
Lakini katika mazungumzo yake na gazeti hili, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda alishangaa: "Umesema tathmini ya thamani ya kiwanja na jengo lililomo iliyofanywa na Mthamini Mkuu wa Serikali ilisema thamani ni Sh. bilioni 1.190, lakini BRELA wamenunua kwa Sh. bilioni 2.7…hiyo sasa ni kazi mpya umenipa, nipe siku mbili tatu hivi ili nami nilifanyie kazi, kisha nitarudi kwako," alisema Dk Kigoda.
Juhudi za kumpata Godson Hudson Nyange wa Kampuni ya Uwakili ya Godson Nyange, iliyomwakilisha muuzaji, Balozi Lukindo, huku akaunti ya kampuni hiyo, iliyoko Benki ya Azania, tawi la Mazido, ikitumika kuwekea fedha hizo kutoka BRELA kwenda kwa muuzaji, hazikuweza kufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni.
Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa kampuni hiyo ambaye jina na sahihi yake vinajitokeza katika baadhi ya nyaraka za mauziano hayo, ukiwemo waraka wa hati ya mashahidi, Juvenalis Ngowi, amekiri kampuni yao hiyo kusimamia mauzo hayo, lakini alisema yeye alihusika kwenye upande wa ushahidi na uthibitisho wa mikataba tu.
"Mimi nilishuhudia mikataba, sikusimamia mauzo, ni vitu viwili tofauti (kusimamia na kushuhudia). Nili-attest documents (shuhudia, thibitisha nyaraka)."
Source: Raia mwema