Kulichotokea hadi nikawa Mwalimu

Kulichotokea hadi nikawa Mwalimu

NUKTA

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Posts
454
Reaction score
413
Ndoto yangu kubwa ilikuwa kusoma sheria na kuwa wakili, niliyamudu vyema masomo ya sanaa hasa Kingereza na Geography na History ila naandika hapa nikiwa mwalimu wa somo la kemia na biologia tena tegemezi hapa mjini

Nilianza kuisaliti ndoto yangu ndani ya chumba cha mtihani mwaka 2008, pale ambapo somo la HISTORIA liliponipa kisogo, nilitoka ndani ya chumba cha mtihani nikiwa siamini kama walau ntapata daraja B. Nashukuru nilikua nikisoma masomo ya sayansi pia sio kwa kujiegesha ila kwa kubobea haswaa wengi darasani waliniita mteule

Hivyo nikahamishia juhudi zote huko hasa nikifungua macho na masikio kuhusu mtihani wa vitendo (practicals)

Nilibadili mtizamo na kujaza masomo ya sayansi nikianza na PCB halafu nikajaza pia HGL kama chaguo la pili ili ikitokea bahati ndoto yangu iendelee kuishi. Nashukuru Mungu nilifaulu vizuri nikipata daraja la kwanza alama 15. Nikachaguliwa shule ya secondary Shinyanga mchepuo wa PCB.

Nasema wazi sikufurahiii hata kidogo ila hali ilikua tofauti kwa jamii iliyonizunguka kila MTU alinisifia hii ikanibadili fikra na mtazamo nikatamani kuwa DAKTARI.,,

Nilipoanza masomo nilizidi kukosa raha na kukata tamaa napenda kuongea hasa kuweka mjadala na ubishi wa hoja wenye mifano kuntu kwa mdomo au maandishi. Hili nikalikosa kwenye FIZIKIA KEMIA NA BIOLOGIA, kote nakutana na vitu vya ajabu ajabu natakiwa kukalili duh NILIKONDA .. ila nikajikaza kiume,,Biological science,,, ilinitesa

Huku Mechanics na organic chemistry ikanimalizaaaa......changanya na uongozi wa taaluma nilikua nao nikaonaa wazii naambulia patupu na WATU watanishangaa...................

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli ume became [emoji2][emoji2][emoji2] siku nyingine uwe unaandika heading kwa kiswahili


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kweli ume became [emoji2][emoji2][emoji2] siku nyingine uwe unaandika heading kwa kiswahili


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwa maandishi yake hapo hajakosea "how I became a teacher" au angesema "how I ended up to be a teacher" ulitaka aseme "how I become"?????? Totally wrong...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hv kwa nini watu wakifeli ndio waende kusomea ualimu? asilimia kubwa ya walimu, polisi na wajeshi walifeli sekondari ndo wakajiunga na fani
 
Malizia basi...

Ila kwa kifupi ni wewe mwenyewe ulijiweka ukumbane na uliyopitia. Pole.. natumaini sasa na mbeleni baada ya kuandika haya utapambana kuondoa udhaifu wako kwenye mengi uliyonayo kwa mema na amani maishani mwako.
 
hv kwa nini watu wakifeli ndio waende kusomea ualimu? asilimia kubwa ya walimu, polisi na wajeshi walifeli sekondari ndo wakajiunga na fani
sio..kweli..Nina marafiki zangu nilisoma nao advance,walipata division one tena za point kali kunizidi Mimi,but walichagua kusoma ualimu pasipokushurutishwa na mtu.kila mtu anasoma anachokipenda..afu pia hakuna kitu kizuri katika maisha kama kufanya kazi unayoipenda kutoka moyon.
Nina dada angu ni ofisa wa ngazi za juu tu ndani ya jeshi la polisi, alikua mmoja wa best students katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2000,alipiga law udsm,lakini akachagua kuwa polisi mwenyewe na anaipenda kazi yake sana.
 
Ndoto yangu kubwa ilikuwa kusoma sheria na kuwa wakili, niliyamudu vyema masomo ya sanaa hasa Kingereza na Geography na History ila naandika hapa nikiwa mwalimu wa somo la kemia na biologia tena tegemezi hapa mjini

Nilianza kuisaliti ndoto yangu ndani ya chumba cha mtihani mwaka 2008, pale ambapo somo la HISTORIA liliponipa kisogo, nilitoka ndani ya chumba cha mtihani nikiwa siamini kama walau ntapata daraja B. Nashukuru nilikua nikisoma masomo ya sayansi pia sio kwa kujiegesha ila kwa kubobea haswaa wengi darasani waliniita mteule

Hivyo nikahamishia juhudi zote huko hasa nikifungua macho na masikio kuhusu mtihani wa vitendo (practicals)

Nilibadili mtizamo na kujaza masomo ya sayansi nikianza na PCB halafu nikajaza pia HGL kama chaguo la pili ili ikitokea bahati ndoto yangu iendelee kuishi. Nashukuru Mungu nilifaulu vizuri nikipata daraja la kwanza alama 15. Nikachaguliwa shule ya secondary Shinyanga mchepuo wa PCB.

Nasema wazi sikufurahiii hata kidogo ila hali ilikua tofauti kwa jamii iliyonizunguka kila MTU alinisifia hii ikanibadili fikra na mtazamo nikatamani kuwa DAKTARI.,,

Nilipoanza masomo nilizidi kukosa raha na kukata tamaa napenda kuongea hasa kuweka mjadala na ubishi wa hoja wenye mifano kuntu kwa mdomo au maandishi. Hili nikalikosa kwenye FIZIKIA KEMIA NA BIOLOGIA, kote nakutana na vitu vya ajabu ajabu natakiwa kukalili duh NILIKONDA .. ila nikajikaza kiume,,Biological science,,, ilinitesa

Huku Mechanics na organic chemistry ikanimalizaaaa......changanya na uongozi wa taaluma nilikua nao nikaonaa wazii naambulia patupu na WATU watanishangaa...................

INAENDELEAA.....
Nilipoingia katika mtihani wa Physics paper 1, mambo yalikua tofauti,,, nilipagawa nikaona kama maisha yangu yanasimama hakuna nulichogusa kikasogea,,,, nilikata tamaa.. ... Kwa tabu nilimudu kupata daraja la tatu alama 15. Huku nikipata S ya Fizikia ,D ya kemia na E ya biologia.. Sitaki kumlaumu MTU au mazingira ila nafsi yangu mwenyewe ,,,
Mzee nyumbani alinipa.moyo akanambia sio mbaya naweza kupata nafasi ya kusoma ualimu ,,sikuwahi kuwaza hilii. Niliomba nafas ya chuo kupitia TCU second round mwaka 2011,, nikapangiwa chuo cha MWENGE kipo moshi,, kusoma shaahada ya ualimu wa Kemia na biologia,.. Nilifika chuoni nikaanza masomo.bila kupata mkopo Kwa takriban miez miwili.. Mzee akakubali kunisomesha miaka miatatu ,,,,nikawaza na kuwazua kwa gharama ile ninhemudu kusoma CLINICAL MEDICINE Kw a level ya diploma,,nikaomba chuo kimya kimya nikapata chuo kimoja mbeya kinaitwa St Aggrey.. Nikaenda fasta nikalipa ada nusu nikaanza kupiga kitabu roho kidogo ikaridhikaa,,kitabu nikakimudu vizurii,,,
Majanga ni pale mzee alipobaini kuwa nasoma chuo tofaut na course tofautii akaamua kunisusa ,,,akanambia nikitaka yeye alipe ada basi nikasome ualimu... Sikumuelewa ,,,nikaacha chuo
Nikapanda basi. Hadi Morogoro ,,,nikapikelewa na Mjomba angu mpamabanji nikatuliza kichwa hapo nasubiri Mzee abadili maamuzi.. ,,ilikua ni April 2012.. ..Nikaona kukaa bure sio mpango nikajisogeza KIHONDA SECONDARY,,nikaomba kujitoleaa,,,,,Walinipokea kwa mikono miwili nikapewa kufundisha CHEMISTRY,,, kidato cha tatu,, Vijana walinipokea vizurii nikawapanga kusoma jioni wakaitikia kwa pamoja bila ubishi nakumbuka niliwatoza kama 3000/= masomo ya jioni na nikawapata kama 80. ,hiii ilinipa hamasaa nikapita mitaa ya CCM kuna sehemu wanaiita Manzese maarufu sana kwa tuition,,, nikapata kibanda cha kujishikiza hapo..nakumbukaa Nilimfundisha mama mmoja maada 2 za kemia ,,Extraction of metal na Organic chemistry,, kwa madai yake akasema amenielewaa sanaa she paid 100K (laki moja) . ingawa Mimi nili hitaji 50k... Hakuishia hapo baada ya wiki mbili nilitwa Educate secondary wakaomba nifundishe chemistry kwa ki salary kama cha 250K per month It was a suprise kwa kweli ,,nilikubali Mara moja ,,,,baadae yule mama alinipigia simu na kunieleza alichofanya hadi nikaitwa pale.... Nilifanya kazi kama mtumwa kwa nguvu zote,, pia nilijifunza kuandaa kemikali mbalimbali kutoka kwa madam mmoja (SHEMUHINA) alikua akifundisha Educare na Kihonda ........... ... Nilipiga kazi hapo.hadi October 2012.......


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza mtu aliyefeli ni aliyepata daraja gani sekondari?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kufeli ni kule kupata daraja ambalo halitaweza kukufanya utimize ndoto yako, kwa mfano Kaka yangu mkubwa alikua na ndoto kubwa ya kuwa daktari lakini target yake ikiwa Chuo cha Muhimbili tu, akaishia kupata 3:13 ya PCB akakata tamaa ingawa alishauriwa aende kusoma udaktari KCMC au Bugando ila akagoma akaishia kusoma Uchumi Kilimo pale SUA...Kuna mwingine target yake ilikua ni ualimu tu na form four akapata division 4 yenye D kadhaa kumuwezesha kusoma ualimu basi hatuwezi sema amefeli
So kufeli ni kushindwa kuperform vilivyo kufikia ndoto ulizokua nazo awali kabla matokeo hayajabadili malengo yako kufit matokeo hayo currently

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio..kweli..Nina marafiki zangu nilisoma nao advance,walipata division one tena za point kali kunizidi Mimi,but walichagua kusoma ualimu pasipokushurutishwa na mtu.kila mtu anasoma anachokipenda..afu pia hakuna kitu kizuri katika maisha kama kufanya kazi unayoipenda kutoka moyon.
Nina dada angu ni ofisa wa ngazi za juu tu ndani ya jeshi la polisi, alikua mmoja wa best students katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2000,alipiga law udsm,lakini akachagua kuwa polisi mwenyewe na anaipenda kazi yake sana.
ndio maana nimesema asilimia kubwa, sasa iko hv watu walikua wanakimbilia ualimu sababu ya uhakika wa ajira, kipindi cha nyuma ilikua mwalimu ukitoka chuo ajira nje nje, huo ndio ukweli ndugu yangu tena nikiwa chuo cha ualimu butimba mtu alikuja kuripoti ana division 1 ya saba watu wote tulimshangaa kumbe kilikua cheti feki na sasa kashatumbuliwa
huo ndio ukweli umwela na uticha asilimia kubwa walifeli au umasikini unawasumbua ili wawe na uhakika wa ajira
 
Back
Top Bottom