Kula matunda tu usiku ni formular ambayo haiko applicable kwa hapa kwetu Afrika

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
6,528
12,622
Nilihudhuria darasa flani la mambo ya afya coz niliona mwili wangu umekua mkubwa mno so nilitaka darasa la namna ya kupunguza, moja ya masomo ilikuwa ni kula matunda tu usiku.

Nimejaribu jana ila leo nimeshindwa, nimekula matunda saa 1 na nusu nikapanda bed kulala ila sasa hivi saa 3 naskia nenge ya ajabu, imebidi niingie jikoni kurusha nguna tu.

Nadhani hii formula ya matunda tu usiku kwa sisi waafrika haiko applicable kabisa, tuwaachie wazungu tu.

3e0af27d706c0eaa.jpg
 
Nilihudhuria darasa flani la mambo ya afya coz niliona mwili wangu umekua mkubwa mno so nilitaka darasa la namna ya kupunguza, moja ya masomo ilikua ni kula matunda tu usiku...
Usiwasemee Waafrika wote. Sisi wengine tumeweza kula matunda tu usiku.

Hata mimi mwanzoni nilikuwa napata shida, lakini baada ya siku chache nikazoea. Nina zaidi ya miaka saba sasa tangu nianze huu utaratibu wa kula matunda usiku na nimeshazoea kabisa na mwili wangu naumudu sana.

Ukiweka nia kila jambo linawezekana. Ni suala la kuwa na nidhamu tu.

Jitahidi. Hatimaye utaweza tu. Usikate tamaa.

Kila laheri.
 
Usiwasemee Waafrika wote. Sisi wengine tumeweza kula matunda tu usiku.
Hata mimi mwanzoni nilikuwa napata shida, lakini baada ya siku chache nikazoea. Nina zaidi ya miaka saba sasa tangu nianze huu utaratibu wa kula matunda usiku na nimeshazoea kabisa na mwili wangu naumudu sana...
Sawa mkuu
 
inategemea,kwa mfano leo nimepiga biriani moja matata sana mpaka sahivi sina mpango tena wa kula.ukila vizuri mchana unaweza kulalia matunda.
Sawa kabisa. Tunashauriwa kula kifungua kinywa cha kushiba na chakula cha mchana cha kutosha. Jioni unamalizia na matunda na bites kama karanga unashushia na kahawa, chai au sharubati (juice) siku inakuwa imepita hiyo!
 

Dah mkuu umenichekesha, na mm niliwahi kupitia formula hiyo nikashindwa mana ubao unakupiga Ile mbaya hulali aiseee, nilichofanya nilinunua jezi na Mpira nikawa nakwenda mazoezi hasa weekend, mwili haukupungua ila nili gain strong muscles na wepesi na msosi nikaendelea kugonga kama Kawa na mwili haukuongezeka Tena nikawa kama na maintain.
 

Dah mkuu umenichekesha, na mm niliwahi kupitia formula hiyo nikashindwa mana ubao unakupiga Ile mbaya hulali aiseee, nilichofanya nilinunua jezi na Mpira nikawa nakwenda mazoezi hasa weekend, mwili haukupungua ila nili gain strong muscles na wepesi na msosi nikaendelea kugonga kama Kawa na mwili haukuongezeka Tena nikawa kama na maintain.
Ha ha ha..hili suala ni gumu sana mkuu.
 
Pole sana ndugu. Nna tatizo kama lako, uzito wangu ulishafika 100+ kgs.

Nina week sasa nakula mlo mmoja tu kwa siku, yaani nimedhamiria kufanya hivi for the next 10 weeks. Target ni kupungua kilo 5 katika kipindi hiki.

Inahitaji determination ya hali ya juu, mimi ni mtu wa kula kula kila dakika, yaani ikipita miwa nimo, wakipitisha azam ukwaju nipo, wakipitisha fenesi nipo, etc

Ila sasa qm fighting uraibu wa kula, am determined kula mlo mmoja tu from now on wards hadi nitapofikisha kilo 72 nazotakiwa kuwa nazo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom