Kukutwa unaongea peke yako

Kukutwa unaongea peke yako

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,139
Reaction score
12,882
🥺

Ukimkuta mtu anaongea peke yake mheshimu

Watoto ni kawaida, unakuta kitoto kimeshika vikopo kinaongea na kujijibu peke yake

Watu wanao ongea peke yao na kujijibu wamefanya mambo makubwa duniani

Waandishi wa Novel.

Tamthilia kama vile prison break, money heist ulishawahi kujiuliza huwa wanaandikaje script?

Huwa wanaongea na kujijibu wenyewe

Kama unachangamoto sometimes sio lazima uulize watu wengine kaa chini jiuliZe kisha jijibu mwenyewe ikibidi andika maswali na majibu yako kwenye karatasi

Wengine huongea peke yao kimya kimya

Je, ulishawahi kuongea peke yako kimya kimya au kwa sauti?
 
Nakazia.

Mtu ambaye anaongea peke yake muheshimu.

Achana na kuongea kutokana na
Depression, stress na kadhalika.

Kuna mtu hana Tatizo lolote lakini anasemezana,anaweza piga stori na kikundi cha watu cha kufikirika na akawini.

Hata wanamuziki kuna muda wanajikuta wanafanya bonge la show,na nyomi la watu ni kubwa Kwa kuimagine tu.

Mimi mwenyewe naongea Sana peke yangu,zipo faida.

1.kujisahihisha
2.Kusikiliza zaidi kuliko kuongea
3.Kufikiri kabla ya kutenda.
4.kutokuwa mropokaji.
5.kuwa na Busara
 
Nikifikwa na magumu ya kuniumiza machungu ambayo siwezi kumsimulia mtu huwa naliaaaa au naongea mwenyew inanipunguzia kiasi fulani..au ndio tatizo ya afya ya akili inaanza
 
Back
Top Bottom