Mkuu kosa ni kosa tu^^
Tuwasaidie kama tuna nafasi maana katika hao pia tumo na sisi tunazo namba ambazo ni kweli tunazitumia pale tu inapohitajika
^^
Mkuu kosa ni kosa tu
Halibadiliki kuwa sio kosa kwakuwa na sisi tunalifanya
Kama ni kupewa makavu live tupewe tu!
^^
Kweli lakini pia kwa baadhi ya watu ukweli kwao si rafiki, na kwa wengine ukweli ni kichocheo cha kusonga mbele.
Ukiniambia ukweli mimi ntakuona wa maana na si mnafiki.
Katika misaada Tunasema kuwa usiwape samaki wafundishe kuvua.
^^
ni kweli kuna namba hata tumeshasahau kama tunazo lakini ni vizuri kweli kutumia siku una shida tu?. yaani hujawasiliana na mtu kama miezi sita na siku unayopigia au kumtext unalia shida hapo hapo, ukishasaidiwa unapotea, siku unayoibuka unalia tena shida. kweli kipindi chote hicho unashindwa hata kutoa salamu mpaka shida nyingine ikukute!!^^
Tuwasaidie kama tuna nafasi maana katika hao pia tumo na sisi tunazo namba ambazo ni kweli tunazitumia pale tu inapohitajika
^^
we unajiskiaje mtu anakutafuta wakati wa shida tu?mtu akiwa kazongwa na shida sometimes anakosa kujiamini
so akiwa anakuja tu kukusalmia,anaogopa kuonekana 'kaleta shida ingine'
so bora huyo ambae akikutafuta basi ana shida ya kweli.....
Nafikiri inapotokea hali kama hiyo unaweza kumfikiria huyo mwenzio na hali yake je ni kweli yuko bize kiasi hicho?au ye kutwa kushinda kwenye bao na bado hataki walau mawasiliano ya angalau mara moja kukujulia hali mpaka pale shida inapomkumba?,maanake kwa kweli kuna wenzetu wengine hata watoto zao wanawasahau sura maanake kuondoka bado hata jogoo hajawika na kurudi watoto washalala siku nyingi,na mwigine ye kazi yake kushinda kwenye vijiwe kunywa kahawa na kupiga soga na wenzie vijiweni kucheza bao asuuhi mapaka jioni 24/7,ukishajua hali halisi ya huyo mtu uamuzi unabakia wa kwako sasa eiza umsaidie au la.
we unajiskiaje mtu anakutafuta wakati wa shida tu?