Kukumbuka ndoto

Kukumbuka ndoto

Zeus1

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
7,301
Reaction score
9,487
Hivi,kuna njia yoyote unaweza fanya ili uweze kukumbuka ndoto uliyoota??

Au technologically kuweza kuirecord??
I think kuna kitu kikubwa sana kwenye ndoto.
 
Wakati mwingine nilikua na swali Kama Hilo maana nilikua naota ila ikifika mchana natamani nimsimulie mtu ndoto yangu ila nikawa nashindwa

Nikaanza utaratibu huu chumbani kwangu Kuna pen na daftari ikitokea nimeota ndoto nikistuka tu kutoka kwenye ndoto huwa naandika vyote Ninavyoweka kukumbuka kutoka katika ndoto hata Kama ni kidogo Sana (mradi tu nimekumbuka ) kutoka kwenye ndoto naandika kesho yake naisoma Tena

Hii inasadia Sana kukumbuka na vitu vingine

Mfano Nina ndoto niliota wakati flani niliota Kuna paka mwenye rangi nyeupe na nyeusi ananikoromea Kama akitaka kuning'ata nikapigana nae harafu nikampiga hapo Hapo nikastuka

Hii ndoto niliindaka kwenye simu (though hapa nimeacha vitu vingine Sana kwenye hiyo ndoto)

Asante Mungu niliweza kijua tafasiri yake
 
Ndoto zangu zinafanana mara nyingi. Na huwa nakumbuka kila nikiota.

1. Huwa naota napaa. Yaani nakuwa na uwezo kuruka juu hivi,najiongeza juu kwa juu. Nakuwa kama nashuka chini najiongeza juu na juu mpaka kufikia usawa wa mita 200 mpaka 300 kwenda juu. Nafurahi sana nikiruka hivyo. Watu wanakusanyika wananishangaa huo uwezo. Nakuwa naruka sehemu moja,siendi mbali. Huwa nafurahia sana nikiwa ktk hiyo hali. Na hii naiota mara nyingi sana.

2. Naota naimba hivi. Kila nikiimba huo wimbo unakuwa na merod nzuri sana. Kila nikiimba ndotoni wimbo unakuwa mzuri sana. Mara moja moja nikishtuka nafanikiwa kujirecod kwenye simu vile nilivyokuwa naimba ndotoni.
 
Ni kazi unless ukiwa mazingira ya mchana ukutane na kitu kilichokuwa kwenye ndoto inaweza kukusaidia kukumbuka.
Kama ni muamini Mwombe Mungu akukumbushe maana Yeye husema na watu wake kwa kupitia ndoto.
 
Cjui kuendesha vyombo vya moto ila kwenye ndoto naviburuza kichizi ani
Poa bora yako

Mi pia naviendeshaga sema shida kwangu mda mwingine nikiendeshaga gari au pikipiki, ajabu natumiaga pedo za baskeli. Ujinga ujinga tu eti nakanyaga pikipiki au nasimamia gari 😂🤦‍♂️🤦‍♂️
 
Mimi nikiota

Sometimes nipo kwenye ndoto najua kabisa ninaota

Kama ni ya kutisha nafosi nishtuke usingizini japo inakuwa ngumu kama mwili vile umekakamaa

Ikiwa ni nzuri nafosi muendelezo sometimes nashindwa ku control narration
Nashtuka usingizini kesho naifosi hio ndoto naiota tena naendelea muendelezo
 
Poa bora yako

Mi pia naviendeshaga sema shida kwangu mda mwingine nikiendeshaga gari au pikipiki, ajabu natumiaga pedo za baskeli. Ujinga ujinga tu eti nakanyaga pikipiki au nasimamia gari 😂🤦‍♂️🤦‍♂️
hahah hamna rangi utaacha ona
 
Siri ni kwamba unapokuwa umelala ubongo unakuwa katika sleep mode.Yaani unafanya kazi ila unakuwa umepumzika hivyo hushindwa kufanya kazi ya kurecord/ kutunza kumbukumbu ya kile kilichokuwamo kwa wakati huo.
 
Mimi huwa nikiota ndoto nikishtuka usiku baada ya ndoto kuisha huwa naitafsiri kujua inamaanisha nini basi hua nachukua ile tafsiri na kuiacha ndoto na hii nikuona ugumu wa kuitunza ndoto
 
Ukiwa mtu wa kiroho na imani, yani kuwa karibu na Mungu, utakuwa unaota ndoto...

Pia utakuwa unazikumbuka...

Ndoto ni njia ya Mungu kutoa taarifa ya maisha ya mwanadamu...

Ni hatari kutoota ndoto...maana utakuwa unapoteza taarifa kutoka kwa Mungu...

Maisha tunayoishi huanzia rohoni yani ndotoni...

Ukisoma Biblia utaona Yusufu aliota ndoto kuwa angetawala ndugu zake...
Mwanzo 37:50...
 
Wale mnaoota mnapaa na kuendesha vitu ndotoni, inabidi mjitahidi kuongeza nguvu za kiroho!! Maana hapa ni wachawi wanawatumia la madereva na mnaruka nao!! Mbaya zaidi ni kwamba Kuna watu wanawaona ka wachawi kwa kuwa mnashiriki kuwanga
 
nishaota ndoto najenga nyumba yangu, maranyingine naota nafanya finishing kwenye nyumba ambayo ni yangu,
hii ndoto inamaana gani mwenye kujua? Mshana Jr Rakims
 
Hivi,kuna njia yoyote unaweza fanya ili uweze kukumbuka ndoto uliyoota??

Au technologically kuweza kuirecord??
I think kuna kitu kikubwa sana kwenye ndoto.
Kunywa maji kidogo kabla ya kulala,Itasaidia kukumbuka ndoto uliyo ota usiku wakati umeamka.
 
Dah! Ndoto hizi! Ila ndoto unayobaki na ushahidi asubuhi ni ile ya kumtafuna mwanamke tuu. Hizi nyingine ni usanii mtupu, ubongo unatuchezea tu.
 
Ndoto ni nyingi mojawapo ni hii

Tarehe 28.8.2021 wakati korona imepamba moto niliota nachanjwa chanjo ya korona usingizini, nilipoamka nilikuta matobo mawili mkono wa kushoto, niliyapiga picha na makovu yapo mpaka leo.

Wakati mwingi naota naimba yaani naimba nyimbo za Mungu, its wonderful.

Hata wazazi wangu walipokaribia kufariki niliota, though walifariki miaka tofauti.

Majuzi hapo rafiki yangu aliyefariki kwa korona ambaye aliniaga na siku ya tatu akafariki niliota ananiambia waambie wajengee kaburi, nilipofuatilia kweli lilikuwa halijajengewa japo alifariki one year ago nimewapa habari (was my friend in Jesus Christ )
 
Back
Top Bottom