Kuku wangu wanataga na hakuna jogoo. Je, kuna uwezekano wa mayai kuanguliwa?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,825
Habari zenu,

Nina kuku wa kienyeji hapa kwangu ambao nimewazuia wasizagae mtaani, sasa wiki hii kuku wote wakubwa wameanza kutaga na hapa sina jogoo hata mmoja.

Je, niendelee kula haya mayai au niwaachie kuna uwezekano wa kuja kuanguliwa?
 
Kuku wanataga mayai hakuna hata jogoo inakuwaje, sio bure kuna likuku huwa tena nahisi mida ya usiku usiku😂
 
Kuku wanataga mayai hakuna hata jogoo inakuwaje, sio bure kuna likuku huwa tena nahisi mida ya usiku usiku😂

Yai linaweza kutagwa bila jogoo...jogoo kitu pekee anafanya ni kuhamisha chromosomes kwenda kwenye yai teke lililo mwilini mwa kuku jike ili kuunda kiumbe kitachokua ndani ya yai pindi litapotagwa...

Hata wanawake huwa wanadondosha yai/mayai kila mwezi na hutolewa na damu ya hedhi kama hayajarutubishwa na mbegu za kiume...

Yai ni seli inayojitegemea...
 
bila jogoo hawawezi kutotoa we kula tu mayai au wapeleke kwa jirani kama kuna jogoo awapande
 
IMG_0789.jpg

Njoo kwangu uchukue jogoo mambo yawe vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom