Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,639
- 29,512
Wadau za wikiend?
Nina shida naomba msaada wenu please,
Hivi karibuni nimeamua nami kufuga kuku hapa nyumbani kwangu kwa ajili ya kujiongezea kipato pia hata kula nyumbani. Kwa kua ndio mara yangu ya kwanza kujihusisha na ufugaji wa Kuku basi niliamua kuulizia kwanza wataalam mbalimbali juu ya hii kitu na walinishauri nianze na Jogoo mmoja na Mitetea kama wanne au watano hivi. Mwanzo sikuwaelewa maana sikudhani kama Jogoo mmoja anaweza akawatimizia haja zao wale mitetea wote wanne lakini kwa vile wengi walishauri hivi basi nami nikanunua hao kuku kwa hiyo ratio ya 1:5.
Sasa shida imekuja kua toka nimewanunua hawa kuku ni kama miezi mitatu sasa na hakuna hata yai moja. Kuchunguza vizuri kumbe ni Jogoo ndio shida. Yaani huyu Jogoo hajisikii kabisa kufanya naniliu na hao mitetea. Yaani hao mitetea wanaweza wakajipitisha mbele yake na yeye akawaangalia tu. Ninmejaribu kutumia siku mbili hizi za wikiend hii kumchunguza huyu Jogoo toka asubuhi hadi jioni sijaelewa kabisa nyendo zake.
Nimewaza mengi sana juu ya huyu Jogoo, Mwanzo nilidhani labda ni mzee lakini sio Mzee ki hivyo, na wala sio mdogo pia, ni umri wa makamo tu ambao majogoo wengine wa rika lake nawaona wanapiga kazi kisawasawa. Nimefikiri pengine kama kuna binadamu ambao sio rijali au sio ridhiki basi pengine hata huyu Jogoo anaweza kua wa dizaini hiyo pia. Au pia inaweza kua ameumbwa na aibu sana au ni domo zege labda. Au anaweza akawa anatokea jamii ya kuku ambao hawapendi sana mambo ya kupandana pandana. Angekua binadamu ningesema ameokoka (mlokole) lakini kwa kuku sidhani.
Wale wazoefu msaada wenu unahitajika please, maana miezi zaidi ya mitatu sijapata hata yai la kuonja na ninawahudumia gharama kubwa tu za bure.
Ahsanteni