Kuku wa nyama wanafaida kama ukifuga wengi. Mimi ninafuga hawa kuku. Nilianza na kuku 200 kwa mara ya kwanza. Ninawalisha chakula toka kampuni ya Hill. Hawa jamaa chakula chao ni pellets , wana starter,growers na finisher nilitumia mifuko nane. Walipofika wiki ya nne niliuza kuku 100 kwa being ya sh. 5000 na walipofika wiki ya tank niliuza kuku 100 Kwa bei ya sh 5,500 .Nilipata jumla ya sh 1,050,000. Faida ilipatikana kiasi ila kuna mambo kadhaa nilijifunza kama vile kuhakikisha kuku unaowaingiza sokoni wamefikia uzito unaoridhisha, kupunguza ghàrama za uendeshaji kadiri inacyowezekana, kufuga kuanzia kuku 300 nakuendelea, uwe na chakula cha kutosha, at least uwe na batch mbili na kuendelea kwa mwezi mmoja au hizo wiki tano. Mimi huwa nauza kwa hao jamaa wa hapo Mbagala rangi tatu sokoni. Nilicho experience solo ni kubwa has a kuku wakiwa na uzito unaoridhisha.