Kidamva
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,578
- 1,984
Salamu wana JF
Naleta mada hii ya uzoefu wangu katika kufuga kuku wa nyama (broilers).
Nimekuwa mfugaji kwa miezi sita sasa. Awali nilipewa matumaini sana kuwa wana biashara nzuri kama ambavyo wengi wanavyoaminishwa humu. Lakini ufugaji huu una changamoto nyingi kiasi ambacho faida yake hutaiona.
Tatizo kubwa ni gharama ya Chakula. Ni kweli hawa kuku wanachukua hadi week 5 hadi uwauze, lakini chakula chake ni bei ghali, inabidi ujipanhe sana maana kukibwenyewe wakisha fikisha week ya tatu wanakula kama wamechanganyikiwa.
Kuna brand nyingi za vyakula na bei inatofautiana na ubora. Inaanzia kati ya Sh52,000 hadi Sh71,000 kwa kilo 50.
Inategemea unafuga kuku wangapi ndio ujue watatumia kiasi gani.
Hao kuku wanakula usiku na mchana, hawana mapumziko, sasa ole wako uwafanyie ubahili. Utashangaa zimefika week 5 hawauziki. Hasara. Au wakati mwingine ukiwabadilishia chakula walichozoea wanadumaa.
Inabidi uwe na mtaji wa kutosha kuwalisha kikamilifu kwa mwezi mzima. Kama una hela ya mawazo usifanye hii biashara.
Ahsanteni