Kuku wa kuchoma au wakuokwa

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,296
7,670
Jinsi ya kumatayarisha kuku
  • Mgawe kuku kwenye kifua,Mgeuze ili mgongo uwe juu na mchanechane kwenye mapaja na kifua,dhumuni la kufanya hivo ni ili viungo vikolee vizuri.
20140614_141123.jpg
  • Kama unavyoona pembeni kuna vitunguu swaumu,vitwange na umpake mkuku,fanya kama unamfanyia masaji,weka viungo kwenye sehemu zote ulizomkata mkata hakikisha vinainga ndani,kisha muweke All around spices,na mchanganyiko wa viungo vya kuku vyenye uzile,giligilani,pilipilimanga,Kari,pilipili ya unga red paprika,endelea kumfanyia masaji tumia vidole.Malizia na juisi ya limau.Ukiwa unamuweka viungo muweke pande zote.Baada ya hapo kuku atakuwa na muonekano huu
20140614_141944.jpg
  • Muache kuku akolee viungo masaa kadhaa.
  • Washa oven na uweke moto 200-225 degrees
  • Mchome kuku na katikati uwe unachukua ile sausi inayotoka kwa kuku na kumnyinyizia kwa juu.Akiiva juu mgeuze na upande wa pili ili apate rangi na upande huo.Mwishoni ukitaka crispy skinn weka grill juu kwa dakika tano.
20140417_202333.jpg
  • Kuku tayari kwa kuliwa,unaweza kumla na msosi wowote,wali,chipsi ugali n.k
All around spices
20140614_142157.jpg
Cc Revocatus Kashaga
 
Mami, sema tu adress nikutumie maana nimechepuka kidogo kutoka Sikonge maana Smile kanizingua nimeamua na mimi kutafuta Pipa nibebe kidogo Box na mwezi wa 12 narudi tena Sikonge :)

Goli za jana umeziona lakini? Cameroon walitia huruma.
Mi napenda sana tandoori chicken. Ngoja ni-place order yangu kabisa ili zije on time tayari kwa kuangalia kombe la dunia.
 
Last edited by a moderator:
Dah!!! pembeni una mchicha wako wa nazi, pili pili mbuzi na ugali wa kufa mtu na gudulia la maji baridi, ukitoka hapo mpaka jasho inatoka kwa utamu wa msosi.
 
Dah!!! pembeni una mchicha wako wa nazi, pili pili mbuzi na ugali wa kufa mtu na gudulia la maji baridi, ukitoka hapo mpaka jasho inatoka kwa utamu wa msosi.
nishakuweke pilipili hapo BAK,au ukibadilishia na ile pilipili ya maembe ya farkhina naona utamaliza kuku mzima peke yako....
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Dah!!! pembeni una mchicha wako wa nazi, pili pili mbuzi na ugali wa kufa mtu na gudulia la maji baridi, ukitoka hapo mpaka jasho inatoka kwa utamu wa msosi.

Maji kwenye gudulia nimecheka mpaka nataka kupaliwa.....mie mroho huyo nala na salad tu lol
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom