Kuku mnywa mayai

Kuku mnywa mayai

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,632
Reaction score
8,452
Kuna kuku ambao wao wakitaga mayai, huyatoboa na kuyafyonza wenyewe. Kuku hao, huatamia majivu au majani na kutotoa hewa.
Kuku hawa, huwafanya wafugaji kuwa makini sana pale wanapoona kuku hawa wanaingia bandani kwenda kutaga. Lengo la kuwa makini ni kwenda kuokota mayai pindi tu kuku wamalizapo kutaga. Maana ukichelewa kidogo tu, unakuta ameshalipasua tayari kwaajiri ya kufyonza.

Je, tuendelee kuwa makini kusubiri kuku watage ili tuokote mayai tuyaweke sehemu salama yawe mengi na kuku wakianza kuatamia tuyarudishe wayaatimie ili huko mbele tukapate vifaranga wengi?
Au tuwaache kuku watage na wafyonze mayai waliyoyataga ili baadae waje kuatamania majivu?
 
Kuku achinjwe na mayai tuyakaange.
Maana hata siku akibahatisha akatotoa, atatotoa mfanano wake
 
Kuku anayekula mayai anachinwa mdomo aache hiyo tabia.
 
Nakumbuka enzi zile mama alikuwa ana chukua mkaa ana Choma mdomo
 
Nakumbuka enzi zile mama alikuwa ana chukua mkaa ana Choma mdomo

Halafu akishachomwa mdomo anachukiza.Anakuwa kama wadada wale wa kusiriba milipustiki kwenye milipsi mikubwaa.
 
Wakate mdomo wa juu. Ila nahisi kuna kitu ulikua unamaanisha kwa kutumia mfano wa kuku.
 
Back
Top Bottom