CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,950
- 9,509
- Thread starter
-
- #21
nimekupata Mkubwa kweli hii ni mbegu ya maana, vp hiyo company unayosema inaagiza kutoka INDIA hawaagizi hawa kuku wa malawi, au hawa kuku wa malawi (weus) ma wale wekundu wanawaita (kuchi) wapi wanataga vzuri na hawasumbui kwa magonjwa! au ni kuku aina gani wanaotaga vizur na wanapatikana hapa Bongo?
Nakushukuru sn Mkubwa kwa taarifa mna mawazo ya mzingi sn, sasa naomba unisaidie kuulisa hizo kuulizie fertilized eggs za kuku wa Austrolop, upatikanaji wake, wanauza kwa idadi gani (mfano tray kuanzia ngap) na bei kwa kila tray!Mkuu Kuku wa Malawi ni huku Bongo, Ila kama nilivyo sema hawa ni Austrolopu ila wali crosiwa na kuku wa Kienyeji kupata hao wa Malawi, Jamaa hawaagizi Kuku wakubwa, wanaagiza vifaranga au Fertilized eggs, hivyo labda ni kuulizie fertilized eggs ya hawa kuku wa Austrolop kama una mashine utawaangua na kuwa na F1 YA AUSTROLOP
Na kuhusu Kuku wanao taga mayai mengi nazani Chotara wote hutaga mayai mengi kwa sababu hawaatamii na huiga tabia za kuku wa kisasa ingawa wakowanao chukua tabia za kuku wa kienyji na kuatamia,
Magonjwa, hapa kinacho takiwa ni kanuni za ufugaji bora tu, kwa sababu hata kuku wa Kienyeji wanakufa sana kwa magonjwa tena huko Vijijini ndo usiseme wana pukutika sana, hivyo kikuba ni kuzingatia kanun bora za kuwafuga ikwemo Chanjo na chakula chao plus sehemu nzuri ya kulala
Mkuu hawa hufikia 5 kg ila moja ya sifa za hawa kuku unaweza wafuga free range na wakajitafutia wenyewe. Kwa uzito bado hawajafikia DOREP ambao ni 8ngapi kg, ila Dorep kuwafuga free range kidogo ni shughuri, ila hawa pamoja na SASSO unawafuga na wanaweza jitafutia wenyewe ingawa bado unatakiwa kuwapa chakula cha ziada na unaweza pia kuwafuga kama wa kisasa
Hao Dorep unao?
mkuu wanapatikana na kuna watu wanao hapo Dar so ukitaka kuwaona walivyo nitakuunganisha nao, kama uko Dar
Naomba contacts boss ndio kusaidiana kwenyewe huko.
Majogoo yangu mengi yamechoka na sitaki kufanya interbreeding, Mkuu ninaweza kupata vifaranga waliofanyiwa sexing, nataka majogoo ya bora ya kuku mchanganyiko( wa DOREP F1, RED RHODE ISLAND F1, BLACK austrolop) nikipata hata 300
Mkuu heshima yako, Je? Naweza kumpata kwenye kampuni gani huyo f1 maana naona watu wengi wanauza kukuMkuu kwa Dorep unaweza pata ila si FI na kwa ishu ya RIR na Black Austrolorp mtu asikudanganye kwamba ana F1 kwa Tanzania na mtu akikumbia ana Black austrolorp F1 basi akuonyeshe import permit ya kuwaagiza kutoka Australia hapo itakuwa sawa.
Kwa kifupi ni kwamba Black austrolorp walioko bongo walisha choka sana watu wanafuga tu ilimuradi na hata hivyo huwezi pata F1 kwa Tanzania hata huko Malawi, F1 inapatikana South Africa,
sh ngapi hao vifaranga?yes wapo
Mkuu heshima yako, Je? Naweza kumpata kwenye kampuni gani huyo f1 maana naona watu wengi wanauza kuku
Nalog off
\sh ngapi hao vifaranga?