Kukosolewa ni kitendo kinachopingwa na wengi

Mungu Mweusi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
1,474
1,079
Habari zenu; napenda kuwasilisha mada hii mbele yenu ili nanyi mpate kujifunza jambo; binadamu wengi hawapendi kukosolewa pale wanapokuwa wamekosea jambo Fulani la kikazi, kitaaluma, au katika mambo mbalimbali. Je ningependa kufahamu kwa nini watu hawa wapo na inatokana na nini? Maana huwa tayari wafanye tukio baya kwa yule mkosoaji. Je huu ni ugonjwa wa akili au mapungufu ya fikra?
 
Ni mapungufu tu kujiamini kuliko pitiliza ila ni upuuzi na ujinga pia.
Upo sawa kabisa mkuu,
unakuta kwa mfano mtu anaanzisha thread hapa jf basi ukimkosoa tu anawaka kama nini!! anataka kila mtu amsupport na kumsifia tu! kitu ambacho sio rahisi kutokea kwa watu wote..
Screenshot_2016-03-24-08-12-42.jpg
Ni ile hali ya mtu kujiona yupo perfect na anajua zaidi kuliko watu wote mpaka anakua ni kituko mbele za watu!!
 
Tatizo ni namna ya kuwasilisha ukosoaji huo.
Wakosoaji wengi hukosoa kwa mihemuko ya wivu na chuki binafsi.

Lakini kama mtu anakosoa kwa ustaarabu kwanini asieleweke?
 
Tatizo letu hasa watanzania tulio wengi hatupendi kuambiwa ukweli. Hii inajitokeza sana inapopewa huduma mahali, utakapasema umepewa huduma mbovu watu wanamind umewadharau. Tujifunze kwa wenzetu hasa wazungu. Hiki kitu kinachoitwa "feedback" huwa kwao kina maana kubwa sana, iwe +ve au -ve wataifanyia kazi. Sisi sasa tunapenda kusifiwa tuu, ukitoa -ve feedback msala
 
Back
Top Bottom