Kukosa mwenzi wa maisha, sababu na dawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukosa mwenzi wa maisha, sababu na dawa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by eRRy, Nov 16, 2009.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]


  KUTOKUWA WAAMINIFU
  Hii ni changamoto nyingine ambayo huwasababishia watu wengi kukosa wenzi wao wa maisha, kila mtu anapenda kuwa na mpenzi anayeaminika ambaye hatompa jakamoyo la kila mara.

  Staili ya maisha ya baadhi ya watu, yamewafanya kushindwa kuaminika, wanaishia kudharauliwa na kuonekana kama daraja fulani ambalo linaweza kulinganishwa na wahuni,

  Hivyo basi, kama unataka ikuchukue wepesi kupata mwenzi wa maisha huna budi kujiangalia mwenendo wako, ujitathimini hatua kwa hatua tena kwa kwa umakini wa hali ya juu. Je umepata jawabu gani? Watu wanakuonaje? Hawakuhamini?

  Jibu, ndiyo? Basi jirekebishe mara moja jiheshimu na uishi katika misingi inayokubalika ili jamii ikuamini. Kama wewe ni kiruka njia, maisha yako hayaeleweki, utaendelea kutazamwa kama katuni isiyo na tafsiri.

  Hujulikani unafanya kazi wapi wewe ni mjanja mjanja tu, kila siku unaonekana na mpenzi mpya, watu wanakuhisi ni jambazi, muonekano wako ni wa kihuni, hali hiyo inakujengea mazingira magumu ya kupata mwenzi. Badilika ndugu!

  UONGO​

  Wengi wamekuwa wakitumia ‘gia’ tofauti kupata wapenzi, hii huwatokea zaidi wanaume ingawa kuna baadhi ya akina dada nao huwa hawajambo kwa kusema uongo ili kujisafisha mbele ya viburudisho vyao.

  Lakini ukweli umethibiti, njia ya muongo ni fupi au ndege mjanja huanaswa na tundu bovu pia wahenga walisema mbio za sakafuni huishia ukingoni.

  Hivyo basi, utadanganya wawili watatu wa mwanzo, kwa ajili ya kukidhi matakwa yako, baadaye itakuwa wazi kwa kila mtu na atajua unavyotumia, akishakubaini mmoja basi na jamii yote itakujua, kwa kuwa habari husambaa mitaani.

  Watu wakishaambiana, jua na thamani yako itashuka tu, kuporomoka kwa thamani ni wazi huheshimiwi na hiyo ni ishara kwamba unadharauliwa.

  Kwa mantiki hiyo itakuwaia vigumu kupata mwenzi wa kweli ambaye waweza kumfanya kuwa mke au mume.

  MAPENZI YA MBALI​

  Fimbo ya mbali haiui nyoka, ndivyo wahenga walivyosema, lakini ngano hiyo ina ukweli wa asilimia nyingi mno, hujawahi kusikia watu wakinena ya kwamba ni wako akiwa kwako akitoka ne si wako?

  Jibu, ndiyo basi huo ndiyo ukweli wa mapenzi ya watu wengi wa kisasa, ukiwa karibu na mwenzi wako ni rahisi kudumu naye kuliko kuwa naye mbali, si unajua tena “abiria chungu mzigo wako?”

  Hata hivyo, ni ukweli kuwa wengi hujikuta wakiwa mbali na wapenzi wao kwa sababu za kikazi, kimasomo na nyinginezo hali hiyo huharibu mapenzi ya watu wengi.

  Kuishi mbali na mwenzi wako huondoa uaminifu kwa sababu huzua chembechembe za usaliti, kwahiyo kama unataka mwenzi wako awe wa kudumu, unashauriwa kuwa naye karibu.

  Natumaini ulikuwa sambamba na mimi tangu Jumatatu, wakati nilipoanza kuchambua mada hii, kwa maana hiyo nina uhakika kwamba umepata somo murua ambalo kwa 100% litakuwa limekupa mwongozo.

  Unadhani bado nahitaji kukupa changamoto zaidi? Hapana ndugu, hizo zatosha!
   
 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unadhani bado nahitaji kukupa changamoto zaidi? Hapana ndugu, hizo zatosha!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  hii habari umecopy GP na kupest hapa sio?!
   
 4. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yap! so?

   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  So..BIG UP!

  kUNA WATU sijui wana ugomvi gani na copy and Paste!
  Mimi ninachoandika hapa ni copy and Paste ya kilichomo akilini mwangu...so whatz up!

  ................Mental Liberation...is such a mighty thang!
   
Loading...