Kukosa malezi ya baba kunanitesa sana.

Kinachokusumbua sasa hivi kitakwisha pindi utakapooa na kuanzisha familia yako. Mke wangu alilelewa bila baba na mama na alikuwa anajiita yatima ila tulipofunga ndoa alisahau yote na sasa yuko sawa tunalea familia na pia maisha yanaenda vizuru tunashukuru Mungu
 
Huenda ikawa kuna ukweli. Shukrani.
Kinachokusumbua sasa hivi kitakwisha pindi utakapooa na kuanzisha familia yako. Mke wangu alilelewa bila baba na mama na alikuwa anajiita yatima ila tulipofunga ndoa alisahau yote na sasa yuko sawa tunalea familia na pia maisha yanaenda vizuru tunashukuru Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume hata ukizaa na kichaa usiache kumtunza mtoto.
Wengi wetu tunaacha watoto tuliozaa na wanawake wengine wanateseka kwa kuogopa wake zetu na watoto wa ndani.
Maskini kumbe hao watoto tunaoona Ni wetu tumeuziwa mbuzi kwenye gunia.

Ukiwa na mtoto popote pale be selfish.
Huyo asiyetaka mtoto atunzwe aachwe yeye.!!

Sent using Jamii Forums mobile app
daah Upo sahihi kabisa hasa hapo mstari wa mwisho" asiyetaka mtoto atunzwe aachwe yeye" Mimi huwa naamini ukiacha ndugu wa kuzaliwa nao..basi anayefuata ni mtoto/ watoto wangu...hawa wanawake tumekutana tu ukubwani kila mtu ana malezi yake kwahiyo mtu asibabaishwe nao!!
 
Huenda ikawa kuna ukweli. Shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna ukweli mkubwa kwa kuwa kwa sasa wewe bado unajiona mtoto na kuwazia walezi. Pindi utakapo pata mwenza na wewe kuwa mlezi utabadilisha mindset na kusahau yaliyopita. Nimeiona hiyo kwa mke wangu yeye hakuwa na baba wala mama na alilelewa na ndugu yake ila kwa sasa ameshasahau yote yaliyopita na analea watoto vema tu
 
Habarini za usiku huu wapendwa?. Poleni kwa mihangaiko na majukumu ya weekend ya leo, yote kheri tumshukuru Mungu.


Bila kupoteza muda basi niende moja kwa moja kwenye kipengele taja hapo juu.
Ni kwamba mm ni mtoto wa kwanza kwa wazazi wangu(baba na mama) na umri wangu uko kwenye 20's. Baba na mama walikutana shule na wakati huo mama akiwa na umri wa miaka 15 tu na wakati huo akiwa std 7 na mzee wangu alikuwa ameshamaliza std 7 miaka 2 mbele ya mama means mama alipata ujauzito akiwa ana miezi kadhaa tangu aingie std 7, miaka ya 90 hiyo.
Kulingana na mzee wangu mazingira ya kwao kutoruhusu means baba yake kuwa mkali kupita maelezo, alimwambia mama amsakazie mhuni mmoja hv huo ujauzito(Nilihadithiwa na mama mkubwa japo mama hajaniambia). Mama naye alifanya hivyo bila kujua madhara yake baadaye. Huyu baba wa kuuziwa mbuzi kwenye gunia hakujua hivyo alikubali bila pingamizi na akalea ujauzito hadi nilipozaliwa.
Miaka alisonga mbele kwa kasi na ilipofika 1998 huyu mzee wangu wa kufikia alifariki nami nikiwa najua ndo baba yangu.
Mwaka 2002 nilipoanza std 1 ndipo nilipomjua baba yangu mzazi, nilikuwa mtoto lkn sikuweza kumwamini hata aliponifuata shule akiwa na zawadi kedekede, nilikuwa nachukua zawadi zake na kumpelekea mama na kumwambia kuhusu huyo mtu aliyenifuata na kujitambulisha kuwa ni baba yangu, mama aliishia kutabasamu tu.
Ilipofika 2005 ndipo nilipozoea kuwa huyo ndo baba yangu baada ya mama kunithibitishia kwa kinywa chake sababu pia mm na huyu baba yangu tunafanana sana.

Maisha ya upande wa mama hayakuwa mazuri sana sababu km ni kulala njaa, kutembea peku nikiwa naenda shule, kunyeshewa mvua nyumba inavuja, nk. vilikuwa vitu vya kawaida sana.
Upande wa baba maisha yalikuwa vzr yy na familia yake(mke na watoto).
Siku zingine mambo yalipokuwa magumu sana, nilikuwa naenda kwa baba kuomba msaada nakuwa najihisi km ombaomba hasa nikijilinganisha maisha ninayoishi mm na wale madogo wa pale, najisikia vibaya sana na kujumlisha na mishauo ya mama(mke wa baba) hapo ndo nilikuwa nahisi kufa siku si zangu . Hadi nilikuwa nahisi tu labda baba alikuwa anahitaji nimjue lkn hakuhitaji anisaidie kwa chochote sababu niliweza hata mkuta yy halafu akanionesha dharau waziwazi na wale madogo wakiwepo hivyo nao wakiona hivyo heshima inashuka kwangu.

Baada ya kumaliza std niliamua nihamie kwa mzee wangu baada ya yy kuniambia ili aweze nilipia ada form 1, nilikaa miaka 2 kwa maumivu lkn baada ya hapo nilipata hifadhi kwa msamalia mwema aliyekuwa karibu na shule sababu shule ilikuwa mbali na kwa baba hivyo ilinilazimu nitembee umbali mrefu ili kufuata masomo na nikirudi home jioni napo hamna kupumzika naingia shamba hivyo usiku hakuna hata muda wa kujisomea sababu nakuwa nimechoka sana.

Baada ya kupata hifadhi nilikomaa na shule ingawa baada ya necta matokeo yalikuwa mazuri kiasi ingawa si sana.

Baadaye nilipata mfadhili wa kuja kwenye jiji letu maarufu la Makonda kufanya kazi ambapo kwa sasa niko na maisha yangu angalau si sana najitegemea na kurudi mkoani kwetu huwa naenda mara moja moja kusalimia.

TATIZO;
Kwa sasa shida inakuja yaani nakuwa napretend kuwa niko sawa na mzee lkn roho yangu haipo hivyo, kuongea sawa hata kwenye simu tena tunaweza ongea story za wapi na wapi na kucheka nn na nn lkn huwa nahisi naidanganya nafsi yangu. Na kuongea kwenye simu hadi baba anitafute yeye na kuna muda huwa anajishtukia kwa kuniambia niwe karibu na mkewe(mama wa kufikia) akiamini labda ukimya wangu yy(mkewe) ndo chanzo wakati si kweli.

Kitu kingine nakuwa mpweke kupitiliza means napenda kukaa peke yangu sana hadi muda mwingine sipendi hata kupiga story na watu, naweza nikajifungia ndani nikiwa nipo home bila hata kutoka hata nje na ikitokea akaja mtu kupiga labda story, nitatafuta sababu yeyote hata kujifanya natakiwa nifike mahali ili mradi tu aondoke. Lkn nakuwa na huruma na matatizo ya watu means naweza kulia hata kimoyo moyo sababu ya matatizo ya mtu

Kwa ufupi pia, ni mcheshi sana kwa watu(hadi huwa nasifiwa) lkn nafsi yangu nahisi inakuwa imebeba vitu vizito kuliko capacity yake.
Na napenda utani sana hasa nikiwa maeneo ya kazi na hii ndo maana ya watu kunisifia ucheshi na naamini hiyo hali inaficha maumivu niliyo nayo moyoni.


Ningependa sana kuondokana na hayo matatizo lkn nakuwa nashindwa hivyo msaada wako hasa wa kimawazo unahitajika sana.
Pia hata wale wa matusi karibuni sana.

N.B; Nilichogundua, malezi ya mtoto yanafaa kuhusisha wazazi wote wawili na km kuna tofauti kati ya wazazi bora zikamalizwa haraka sana ili kuweza kumlea mtoto ktk maadili mema.
Asante.


Wako ktk ujenzi wa Tanzania ya viwanda;
DON YRN.

Sent using Jamii Forums mobile app
nadhani hukupat amboko za baba, ndio hizo zinakufanya uwe mpweke ndani !
 
Kwa wale wote mliozaliwa na kulelewa na mzazi mmoja hasa single mother tafadhali mnapokua tumieni nguvu zenu zote kuhakikisha mnawatunza mama zenu waliotukanwa malaya ila wakapigana mpaka mkajiweza. Kuanza kumtafuta baba ambaye amemsababishia mama yako na wewe mwenyewe mateso na dhihaka maisha yote ni kuendelea na matusi yaleyale ambayo mama yako ametukanwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu umenikumbusha,nimekosa malezi ya baba,nikiwa mdg sikuona tatizo lolote lkn siku zilivyozidi kusonga nilianza kuhisi nakosa kitu flani,namiss uwepo wa baba.
Ingawa baba mlezi alikuwa ananipenda sana tena sana na hakuwahi kunitenga kwa moja wala mbili na ht majiran walijua alikuwa ni baba yng mzazi,alinilea tangu nikiwa na 4 yrs..mpk alipofariki last yr(r.i.p dady)..yote ktk yote nilimiss uwepo wa baba yng mzazi,.
Nikiwa na wenzangu na wanapoanza kuongea hbr za baba zao ghafla nakuwa mnyonge,nakuwa mdogo kama piriton na nitajitenga na wenzangu na kuanza kulia na by that time nilikuwa form 6.

Likizo moja nilimuambia mama mlezi"Mama kuna kitu nakitamani sana,ingawa najua it's too late kukipata na uwezekano haupo lkn natamani sana,natamani ningepata malezi ya baba mzazi"
mama alinihurumia sana na kuniasa nimshukuru Mungu kwa kila jambo na nimshukuru Mungu hata kwa baba mlezi alienipa(Mungu)
Polee sana
 
Kabisa yaani.
Kwa wale wote mliozaliwa na kulelewa na mzazi mmoja hasa single mother tafadhali mnapokua tumieni nguvu zenu zote kuhakikisha mnawatunza mama zenu waliotukanwa malaya ila wakapigana mpaka mkajiweza. Kuanza kumtafuta baba ambaye amemsababishia mama yako na wewe mwenyewe mateso na dhihaka maisha yote ni kuendelea na matusi yaleyale ambayo mama yako ametukanwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika masiaha haya, kila mtu anayo story yake; ukweli kitendo cha kuzungumza kuhusu hao baba zako 2 binafsi nimekuchukulia very serious, is like umeizungumza aibu kubwa ya mama yako, hapa ni kweli unahitaji msaada but msaada wenyewe ki ukweli upo akilini mwako mwenyewe; vipo vitu katika Maisha vikiisha kutokea you can't change them, tatizo lako ni la kisaikolojia tu, nakuombea sana kwa Mungu upate mke mtakaye pendana nae cause ukipata mwanamke ambaye hakupata malezi mazuri ukweli utaumia Zaidi ya hapa but again watu wa namna yako huaga wababa wazuri sana kwa watoto wao. Dogo, fanya hivyo, that is history already, jitahidi kulisahau hilo tukio kwasababu halikua katika uwezo wako na hauna namna ya kulibadiri, baba yako kwasasa kaona UMRI unamtupa mkono so anatafuta namna ya kuelewana na wewe ili uzee wake usiwe wa shida tena.
Vipi, una mchumba au na wewe unachapa chapa nje? Angalia usije na wewe ukamtengenezea huzuni mtoto mwingine kama ulioipata.
 
Back
Top Bottom