Kukopa bia Baa sio ajabu

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
2,067
2,302
Nimemsikia Mkuu wa Mkoa, Chalamila akiwaasa watumishi wa chini yake kuwa kukopa bia anakuwa amejimaliza. Nimwambie tu kuwa sii ajabu. Kukopa kwa shughuli yoyote sii ajabu. Cha msingi ni kutunza na kuwa ndani ya bajeti yako. Mfanyakazi anaamua maisha yake awe anapata bia 2 kila siku. Kwa mwezi bia 60. Kwa mwezi 120,000. Mshahara unatoka mara moja kwa mwezi. Kwa nini asikope.

Akumbuke. Kantini za polisi na mesi za majeshi zinakopesha. Kosa liko wapi.

Huku mitaani kukopa bia ni masuala ya kawaida kabisa. Cha msingi ni kutokuwa mlevi.

Sina uhakika na maisha yake lakini angejitahidi kuvunja mnyororo wa mikopo umiza kwa walimu na watumishi wengine kuliko kusikitikia kukopa baa.

Hata suala la madanguro ni kukurukupa tu. Zile ni nyumba za kupumzikia. Angeagiza zirekebishwe na zikatiwe leseni kuongeza mapato. Unavunja nyumba ya mtu kwa sheria ipi?

Hata nyumba ya jambazi haivunjwi. Mpaka kwa kibali cha mahakama. Arejee kisa cha Nyerere na Rwegasira enzi hizo akiwa mkuu wa mkoa ea PWANI, Dsm ikiwemo kuhusu makahaba.
 
Back
Top Bottom