Kukithiri kwa Rushwa ya Ngono! nini kifanyike?

Kamanda Kazi

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2012
Messages
2,618
Likes
82
Points
145
Kamanda Kazi

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2012
2,618 82 145
[h=1]Moshi: Wafanyakazi Nakumatt waandamana kupinga kuombwa rushwa ya ngono[/h]
WAFANYAKAZI wa Supermarket ya Nakumatt, iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wameulalamikia uongozi wa duka hilo kwa madai ya kuwanyanyasa na kuwaomba rushwa ya ngono.

Wafanyakazi hao ambao tayari walishafikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama walidai wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono na Meneja Mkuu na na msaidizi wake.

Walisema imekuwa kawaida kwa kila msichana anayefika kuomba nafasi kazi, lazima aombwe rushwa ya ngono huku wanaume wakitakiwa kinyume na maumbile: “Kila msichana anaefika hapa kuomba nafasi ya kazi, anaombwa rushwa ya ngono ndipo apatiwe kazi huku wanaume wakiingiliwa kinyume na maumbile,” walisema.

Aidha walisema sababu iliyowafanya wafikie maamuzi ya kuandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa

kutaka msaada ni kukithiri kwa vitendo hivyo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Meneja wa Nakumatt Moshi, Alfrick Milimo alikanusha tuhuma hizo na kudai kwamba zote hizo ni njama za kupakana matope za watu wasiolitakia mema duka hilo.

Alisema kumekuwa na watu wanaozunguka kuwashawishi wafanyakazi huku akikumbushia matatizo yalitokea kipindi cha nyuma kati ya uongozi na wafanyakazi wake na kuwa tayari wameshabaini njama hizo.

Alisema katika duka lake kuna wafanyikazi wa Kenya na Tanzania lakini mara nyingi tatizo linatokea pale wanapowalazimisha Watanzania kufanya kazi maana wengi hawapendi kufanya kazi bila kushurutishwa: “Niko hapa kwa ajili ya kuwafundisha, kuwaonya na kuwaelekeza lakini inaonekana kuwa unapofanya hivyo unaonekana kuwa wewe ni mbaya na wanafika kazini na mavazi yasizoendana na maadili ya kazi pia wanasinzia kazini,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wafanyakazi hao na kuahidi kuyashughulikia. Alisema tayari ameshaagiza Idara ya kazi kulifuatilia suala hilo kwa karibu na kutoa taarifa mapema ikiwa ni pamoja na idadi kamili ya Watanzania na Wakenya wanaofanya kazi katika duka hilo.

HII NI KERO KUBWA!!! TUJADILI, NINI SERIKALI IFANYE NA SISI TUFANYE NINI?

M

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2010
Messages
15,206
Likes
2,355
Points
280
M

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2010
15,206 2,355 280
Iwekwe hukumu kali sana pale inapothibitika kuna waajiri wanaofanya huu upumbavu
 
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Messages
5,554
Likes
197
Points
145
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined May 8, 2013
5,554 197 145
^^
Serikali ni sisi wenyewe,,serikali za vichwa vyetu zianze kwa kuwa na msimamo wa miili yetu.
^^
 
Blaine

Blaine

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2012
Messages
2,280
Likes
14
Points
0
Blaine

Blaine

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2012
2,280 14 0
...... huku wanaume wakiingiliwa kinyume na maumbile,” .......
toba!! yamefika huko. bora mie nipo kwenye family business

Iwekwe hukumu kali sana pale inapothibitika kuna waajiri wanaofanya huu upumbavu
professional ethics hakuna mkuu. hukumu kali ziko ulaya/US. unakumbuka yule bosi CIA aliyejiuzulu bcoz ya small hausi, hapa it will be "swept under the rug''
 
Lovebird

Lovebird

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2012
Messages
2,538
Likes
355
Points
180
Lovebird

Lovebird

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2012
2,538 355 180
...kwani wamelalamika wanoombwa? walalamikapo ndipo watasaidia kubaini watuhumiwa...wasipolalamika jua wanapenda kutooa rushwa hiyo....:A S 576:
 
Kamanda Kazi

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2012
Messages
2,618
Likes
82
Points
145
Kamanda Kazi

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2012
2,618 82 145
professional ethics hakuna mkuu. hukumu kali ziko ulaya/US. unakumbuka yule bosi CIA aliyejiuzulu bcoz ya small hausi, hapa it will be "swept under the rug''
ni kweli kabisa! tatizo rushwa ya ngono ni ngumu kuitokomeza kwa sababu mbili. moja, watoa rushwa ya ngono (akina dada) wamefikia pahala wameiona ni jambo la kawaida, tena hata katika masuala ya kupandishwa vyeo kazini. pili, wapo viongozi wakuu ambao ndio wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuipiga vita ndio hao hao mabingwa wa kudai hizo rushwa! kwa kifupi rushwa ya ngono imekuwa kama ni desturi katika jamii zetu!
 
kabiriga

kabiriga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
583
Likes
357
Points
80
kabiriga

kabiriga

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
583 357 80
Ningalikuwa mkuu wa mkoa ningalilifunga hilo duka kwanza wakati uchunguzi ukiendelea.ikibainika kuwa lilifanyika hilo,pamoja na hukumu ya mahakama ni kuifutia lesseni hiyo kampuni ili iwe fundisho kwa walewenye tabia kama hiyo.
 
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
11,314
Likes
111
Points
145
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined Sep 30, 2009
11,314 111 145
^^
Serikali ni sisi wenyewe,,serikali za vichwa vyetu zianze kwa kuwa na msimamo wa miili yetu.
^^
hapa ndo panapoudhi....
yaani mtu anataka serikali iingilie kati hata swala la mtu anataka kulala na nani!
hii serikali haina kazi?
kwani kila mtu akikataa kutoa rushwa ya ngono watu watakuwa hawaajiriwi? hawapandishwi vyeo? hawagraduate?
uvivu wa kusoma unamfanya mtu atoe rushwa ya ngono ili agraduate.....
uvivu wa kusoma unamfanya mtu apate grades za ajabu na hapo inampasa atoe rushwa ya ngono ili apate upendeleo kwenye ajira......
uvivu wa kufanya kazi kwa bidii kunapelekea mtu atoe rushwa ya ngono ili apandishwe cheo........
sasa tunataka serikali iingie vichwani kwetu itusomee? itufanyishe kazi kwa bidii?
unajua wakati mwingine nashindwa kuelewa
 
Kamanda Kazi

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2012
Messages
2,618
Likes
82
Points
145
Kamanda Kazi

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2012
2,618 82 145
hapa ndo panapoudhi....
yaani mtu anataka serikali iingilie kati hata swala la mtu anataka kulala na nani!
hii serikali haina kazi?
kwani kila mtu akikataa kutoa rushwa ya ngono watu watakuwa hawaajiriwi? hawapandishwi vyeo? hawagraduate?
uvivu wa kusoma unamfanya mtu atoe rushwa ya ngono ili agraduate.....
uvivu wa kusoma unamfanya mtu apate grades za ajabu na hapo inampasa atoe rushwa ya ngono ili apate upendeleo kwenye ajira......
uvivu wa kufanya kazi kwa bidii kunapelekea mtu atoe rushwa ya ngono ili apandishwe cheo........
sasa tunataka serikali iingie vichwani kwetu itusomee? itufanyishe kazi kwa bidii?
unajua wakati mwingine nashindwa kuelewa
Serikali ni jalala la kila lawama! hata wanaoishi mabondeni licha ya kutakiwa kuhama na wao kukaidi, mafuriko yakiwakumba lawama kwa serikali!
 
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
11,314
Likes
111
Points
145
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined Sep 30, 2009
11,314 111 145
Serikali ni jalala la kila lawama! hata wanaoishi mabondeni licha ya kutakiwa kuhama na wao kukaidi, mafuriko yakiwakumba lawama kwa serikali!
jana nilikasirika sana....
hawa vijana wetu wanataka utajiri wa haraka haraka, wanabeba madawa ya kulevya, wanakamatwa huko nchi za watu, halafu watu wanailalamikia Serikali iende ikawasaidie wanapata shida sijui wengine wanataka kunyongwa.......
keli hii ni kazi ya serikali? kutetea waovu?
 
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
4,541
Likes
1,469
Points
280
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
4,541 1,469 280
Huyo mmiliki wa duka ni Mtanzania?
 
K

Kamawewe

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2013
Messages
432
Likes
270
Points
80
K

Kamawewe

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2013
432 270 80
Sijui ukweli wa tuhuma hizo lakini ninafahamu mishahara wanaolipwa wafanyakazi wa nakumatt na pia ni mteja wa nakumatt inatia hasira Watanzania wenzetu wanavyolipwa ukilinganisha na Wakenya, kwani wenye elimu sawa na Wakenya na wanafanya shughuli za kiofisi na wanahudumia vizuri ninasema hivyo kwa sababu I know the fact mwisho wa siku unaweza sema hii nchi kama haina mwenyewe kwanini Watanzania walipwe ujira mdogo kiasi kile hawafiki ata nusu ya Wakenya, wafanyishwe kazi masaa mengi bila malipo yanayoendana,kwanini Wakenya wafanye kazi ambazo kisheria hawaruhusiwa serikali ipo wapi na idara zake za kazi,uhamiaji, TIC na vyama vya wafanyakazi husika mambo haya haya ya ajabu utayakuta Bonite (Wahindi wanapanga hadi mafaili wanaingia nchini kupitia Tanzanite one) .Watanzania wenzangu kwenye hili tuwe wazalendo tuwajali wenzetu bila kujali tulipo sisi, issue ni Utanzania wetu mbona sisi tukienda kwao tunaishi Mungu nisaidia I HATE THIS VERY MUCH
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,245
Likes
13,782
Points
280
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,245 13,782 280
Na wanaume waliandamana??
 
N

Napoleon 1

Member
Joined
Apr 5, 2013
Messages
79
Likes
1
Points
0
N

Napoleon 1

Member
Joined Apr 5, 2013
79 1 0
Serikali ni jalala la kila lawama! hata wanaoishi mabondeni licha ya kutakiwa kuhama na wao kukaidi, mafuriko yakiwakumba lawama kwa serikali!
Rushwa ni kosa na kama hii ni aina ya rushwa basi inatakiwa sheria ifuate mkondo na hivyo Serikali anahusika, Wahusika wameonesha nia ya kupambana na Rushwa huo ni mfano wa kuigwa
 
N

Napoleon 1

Member
Joined
Apr 5, 2013
Messages
79
Likes
1
Points
0
N

Napoleon 1

Member
Joined Apr 5, 2013
79 1 0
Nilisha kutana na hilo tatizo sehemu nyingi, sikuwa na pakushtaki mwisho ni Uadui na Kuchukiwa, Wakati mwingine Familia yangu ilibidi ingilie kunisaidia
 
Kingmairo

Kingmairo

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Messages
4,973
Likes
1,239
Points
280
Kingmairo

Kingmairo

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2012
4,973 1,239 280
hapa ndo panapoudhi....
yaani mtu anataka serikali iingilie kati hata swala la mtu anataka kulala na nani!
hii serikali haina kazi?
kwani kila mtu akikataa kutoa rushwa ya ngono watu watakuwa hawaajiriwi? hawapandishwi vyeo? hawagraduate?
uvivu wa kusoma unamfanya mtu atoe rushwa ya ngono ili agraduate.....
uvivu wa kusoma unamfanya mtu apate grades za ajabu na hapo inampasa atoe rushwa ya ngono ili apate upendeleo kwenye ajira......
uvivu wa kufanya kazi kwa bidii kunapelekea mtu atoe rushwa ya ngono ili apandishwe cheo........
sasa tunataka serikali iingie vichwani kwetu itusomee? itufanyishe kazi kwa bidii?
unajua wakati mwingine nashindwa kuelewa
Kwa historia ya tatizo lilivyo kwa sasa intervention ya serikali ni muhimu. Tatizo ni kubwa na njia mojawapo ni kuua chanzo cha tatizo. Kama vyombo husika vya dola vingekuwa na nia ya kupambana na hii kitu, ingezuilika kirahisi kuliko kutegemea washawishiwa kushinda vishawishi. Wengi wataoshinda kishawishi ni wenye alternative, lakini wasio nazo wataangukia huko tu.
 
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Messages
9,905
Likes
1,345
Points
280
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2010
9,905 1,345 280
hii thread itanifanya nione kila mwanaume anayefanya nakumatt pale moshi ameshapigwa ndogo... maana ndicho wanacholalama hapo
 
Ablessed

Ablessed

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2013
Messages
4,620
Likes
120
Points
145
Ablessed

Ablessed

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2013
4,620 120 145
jana nilikasirika sana....
hawa vijana wetu wanataka utajiri wa haraka haraka, wanabeba madawa ya kulevya, wanakamatwa huko nchi za watu, halafu watu wanailalamikia Serikali iende ikawasaidie wanapata shida sijui wengine wanataka kunyongwa.......
keli hii ni kazi ya serikali? kutetea waovu?
Hapo mi ndo nashindwa kuelewa. Watu wanafanya biashar chafu huku wakijua wazi matokeo yake ikiwa ni pamoja na kufungwa, kunyongwa n.k. Back to topic rushwa ya ngono haiwezi kuisha iwapo kama unyanyasaji wa kijinsia hautawekewa sheria kali. Nachelea kusema wanaotoa rushwa ya ngono ni uzembe wao, wakati mwingine si kosa lao baadhi wanalazimika kukubali eg mtu katafuta kazi kwa muda mrefu bila mafanikio na wengine wana watu wanaowategemea. Sasa anapoombwa rushwa ya ngono inakua vigumu kwake kukataa. Wengine wanapata manyanyaso sana kazini hasa boss anapokua amemtaka. Anakua na wakati mgumu sana na pengine kufikia hatari ya kufukuzwa kazi. Sasa nini kifanyike mimi kwa mtazamo wangu inapaswa pawe na sheria zinazomlinda mwanamke na zizuie unyanyasaji wowote wa kijinsia na hatua kali ziwekwe bayana lili wahusika waweze kuogopa mbona wenzetu wa magharibi wameweza tena hakuna watu wanaovaa vibaya kama hawa. Nieleweke vizuri sio kwamba nahalalisha hii rushwa ya nono la hasha ila nataka kuzungumzia uhalisia wake wapo wasioweza kujitetea au kukataa sasa ikiwekwa sheria na ikasimamiwa basi itawasaidia hawa wenye roho nyepesi
 
Forum statistics

Threads 1,273,512
Members 490,428
Posts 30,483,678