Kukesha Mbio za Mwenge, nipeni ushauri na uzoefu.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,311
6,605
Poleni na majukumu wadau. Mada yangu hapo juu yaeleweka. Mimi ni mmoja wa wanakamati wa mapokezi ya Mwenge ktk wilaya Fulani humu nchini mwishoni mwa mwezi Julai. Haya mambo ni mageni kwangu alafu naambiwa Mwenge hauna mzaha na niwe makini sana. Isitoshe sijawahi kuuona Mwenge mubashara sembuse kushiriki itifaki yake . Niliomba ushauri jukwa la habari mchanganyiko lakini kule kuna utani mwingi mno nikaamua kuleta mada yangu huku kwenu wanasiasa. Nimekubali kushiriki kazi hii kwa mambo yaliyo juu ya uwezo wangu. Sipendi Matusi wala kejeli, kama huna ushauri naomba upite kmyakmya. Naomba kuwasikisha.
 
Back
Top Bottom