Kwani Sumaye ni fisadi, labda hamelewi maana ya fisadi. Fisadi ni binaadamu aliyefikia hali mbaya sana ya afya ya ubongo na akili kiasi cha kufananishwa na Shatwani. Mzinzi, jambazi, muuaji, mwizi, mlaruswa, asiyetosheka na chochote, mwenye tamaa isiyoelezeka. Utaona kwamba kama binaadamu amekuwa fisadi, maro nyingi ni mshirikina mwenye kuweza hata kula nyama ya mwanae mpendwa. Sasa neno fisadi si la mchezo hata kidogo.
Hebu tuone mfano wa fisadi katika Least Developed Countries:
1. Kiongozi ambaye hana uchungu na nchi yake kiasi cha kuingia mkataba wa aina yeyote ile ambao anajinufaisha binafsi kwa kuliletea taifa hasara kubwa sana. Mfano mrahaba wa madini asilimia tatu na ishirini za kwake.
2. Kiongozi mshirikina mwenye kuua nduguze kwa ajili ya madaraka.
3. Kiongozi asiye na kiasi, mbinafsi, mwenye kujilimbikizia mali hata kama itaoza, bilu kujali waliomzunguka na shida zao (Kama kuna mtanzania kwenye hii kampuni inayodai Tanesco, ni mfano mzuri)
4. Kiongozi anayeabudu mashetani na ushetani. (walala makaburini).
hawa wanakuwa wamepoteza kabisa "guilty conciousness" na hivyo huwa na mithili ya hayawani. neno fisadi si mchezo bwana, hawaendi mbinguni ng'o, kama vitabu vya mwenyezi Mungu vinavyosema.
Hawana utu, hawajui haki, sio wakweli wanaweza kuuza hata wake zao. Kwa kifupi hamna maneno mazuri zaidi ya kufananishwa na shetani aliyevaa mwili wa mwanadamu. Afrika ina viongozi wa namna hii? kama wapo tumekwisha.