Kukata rufaa nje ya muda sheria inasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukata rufaa nje ya muda sheria inasemaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mukama talemwa, Feb 20, 2012.

 1. m

  mukama talemwa Senior Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamaa yangu ameshinda kesi CMA baada ya mwezi mmoja kupita bila mwajiri kusema lolote akaamua kukazia hukumu ambapo Mahakama kuu ikatoa order kwa mwajiri ikimtaka kutekeleza maamuzi ya CMA jamaa yangu alipopeleka order ndani ya week moja mwajiri akampatia copy ya appeal ya High Cort ambayo inaonyesha kuwa ameikata baada ya order ya Mahakama, na siku zilikiwa zimefika 54 tangia mwajiri amepata nakala yake ya hukumu.Waungwana sheria inasemaje kuhusiana na hali kma hiyo.
   
 2. Lord K

  Lord K JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Rufaa siyo rufaa mpaka iwe imekidhi masharti na vigezo ,muda ukiwa ni mojawapo hivyo hiyo rufaa ni null and void.
   
 3. B

  Bandio Senior Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani mahakama inaweza kuruhusu kama mwombaji anaweza kueleza to the satisfaction of the court ni kwa nini alichelewa kuomba. Au hakuna mazingira yanayoweza kumzuia mtu kutenda jambo fulani? Na mimi nisaidieni msimamo wa hili kisheria.
   
 4. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 280
  Unachosema ni kweli, nikipitia vifungu nitakuhabarisha, ila kila mashauri yana muda wake maalum na kama una sababu za msingi huwa mahakama inaruhusu appeal ila napo kuna muda wake pia. Sikumbuki vifungu ila hata ukiwa na sababu za msingi kuna limit ya kuappeal nje ya muda uliowekwa.
   
 5. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Angalia kamaametimiza haya:

  1.He has applied for leave to appeal out of time

  2.Then leave to appeal out of time has been granted

  Angalia kama masharti hayo yametimizwa, if not then you have a chance to raise a PO (preliminary objection)
   
 6. m

  mukama talemwa Senior Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamaa ameisha raise hiyo PO,maana mwajiri ame-file High Cort Misc application na Revision tu.Sasa anasikilizia Mh Jaji maamuzi yake,ila nasikia hawa majaji wa High Cort Labour Division uwa wako fear sana na wote ni wakinamama
   
Loading...