Kukata Rufaa Mahakama ya Rufaa

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,489
1,812
Wana jamii,

Salaamu, jamaa yangu alikuwa na kesi mahakama ya Ardhi sasa anasema siku ya kusomwa hukumu alitajiwa tarehe tofauti na wakili. Baadaye alikuja kugundua kuwa hukumu ilishasomwa kama wiki mbili zilizopita. Sasa anaulizia je ni muda gani baada ya hukumu anatakiwa kukata Rufaa na anatakiwa afanye nini hasa. Mimi nimeshindwa kwani sheria not reachable lakini nikaona nitafute ushauri hapa kwenye jukwaa lenye kila aina ya professionals.

Natanguliza shukrani za dhati
 
Pole sana ndugu yangu.
Kama shauri hilo lilianzia baraza la kata, muda wa kukata rufaa kwenye uamuzi ulitolewa na baraza la ardhi la wilaya, ni siku 60 tangu hukumu iliposomwa.
Kama shauri lilianzia moja kwa moja katika baraza la ardhi la wilaya (yaani mogogoro uliozidi tshs 3,000,000), sheria ya ardhi haikuweka muda wa kukata rufaa. Katika hali hiyo inabidi utumie sheria ya kikomo cha muda sura ya 89, jedwali la kwanza sehemu ya pili inayohusu sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai, inayoonyessha kuwa iwapo sheria iliyaondikwa haikuweka kikoma cha muda wa kukata rufaa, basi muda utakuwa siku 90.
Muda huo huhesabiwa tangu siku ulipopewa nakala ya hukumu.
Mambo ya kuambatisha hutegemea pia shauri lilikoanzia. Kwa mfano kama lilianzia baraza la kata, basi inabidi sababu za rufaa zisajiliwe katika masjala ya baraza la wilaya nk.
Hivyo ndugu yangu sheria ina mzunguko mrefu. Inabidi tupate few details. kwa mfano shauri lilianzia wapi -kata? nini ilikuwa hukumu yao. je lilifikaje baraza la wilaya, nini hukumu ya baraza la wilaya nk.
 
Hivyo ndugu yangu sheria ina mzunguko mrefu. Inabidi tupate few details. kwa mfano shauri lilianzia wapi -kata? nini ilikuwa hukumu yao. je lilifikaje baraza la wilaya, nini hukumu ya baraza la wilaya nk.

Nashukuru sana kwa majibu mazuri. Kesi ilianzia Wilaya jamaa akashindwa ndo ikaenda Mahakama kuu. Hivyo usajili wa sababu za Rufaa unafanyika Wilayani ama Mahakama kuu?

Aksante sana
 
Inavyoelekea na kama nimekuelewa vizuri (umetoa details kidogo sana) kesi yako ilianzia baraza la ardhi la wilaya, ikahukumiwa na baadae ikakatwa rufaa kwenda mahakama kuu kitengo cha ardhi. Hivyo unacholalamikia ni kuwa hukumu iliyosomwa na mahakama kuu kitengo cha ardhi wewe hukuwepo na hivyo unataka kukata rufaa kwenye mahakama inayofuata ambayo ni mahakama ya rufaa.
Kama ni hivyo basi mlolongo wa kisheria uko hivi:
Fungu la 47(1) la sheria ya mahakama ya migogoro ya ardhi ambalo linasema "mtu yeyote ambaye hakuridhishwa na uamuzi wa mahakama kuu kitengo cha ardhi, anaweza, KWA RUHUSA YA MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI, kuomba rufaa kwenye mahakama ya rufaa. Ndugu yangu kuwa makini hapa -hapo nlipo-bold; ni lazima uombe ruhusa ya kukata rufaa katika mahakama hiyo hiyo iliyotoa uamuzi usioridhika nao. Usipofanya hivyo mahakama ya rufaa haitapokea rufaa yako.
Maombi ya ruhusa ya kuomba rufaa huwasilishwa kwenye hati ya maombi ikiambatanishwa na hati ya kiapo, na kusajiliwa kwenye mahakama kuu kitengo cha ardhi. Maombi ya ruhusa ya kuomba rufaa uyafanye ndani ya siku 60 tangu hukumu iliposomwa.
Baada ya maombi kukubaliwa ndipo utatuma taarifa ya rufaa iliyo kwenye muundo wa fomu namba 'D' iliyo kwenye jedwali la kwanza.
Baada ya kutuma taarifa ya rufaa katika mahakama ya rufaa, rufaa kamili inapaswa iwasilishwe kwenye mahakama ya rufaa ndani ya siku 60 tangu kutumwa kwa taarifa ya rufaa.
Nyaraka za kuambatisha ni:
Sababu za rufaa (nakala tano)
Kumbukumbu za rufaa ambazo ni majalada yanayohusika (nakala tano)
Ada ya rufaa
Gharama za dhamana ya rufaa.
(katika kila kipengele muda wa kusubiri nyaraka hauhesabiwi) Ni vyema basi ukawa na despatch book yako ambamo kila unapoomba nyaraka basi anayepokea barua hizo aweke sahihi na tarehe ya kuzipokea; na pia wewe unapopokea nyaraka hizo hakikisha unasaini na kuweka tarehe ulipozipokea; na kuwa mwangalifu na nyaraka zenye kuandikwa tarehe za nyuma sana.
Mimi si wakili wala si mwanasheria, ila nakuomba uwahusishe wanasheria katika mjadala wa suala lako.
Mwisho - usiogope, huko kwenye mahakama ya rufaa ni haki tupu.
 
Back
Top Bottom