SuperImpressor
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 1,505
- 649
Siku moja mwalimu alikuwa darasani ambamo kulikuwa na mbao mbili za kufundishia Ubao mmoja uliokuwa pembeni mwa darasa ulikuwa mweusi na mwingine uliokuwa mbele ya darasa ulikuwa mweupe, sasa huyo mwalimu akawa ameandika notisi kwenye ule ubao mweusi ambao uko pembeni mwa darasa ukawa umejaa ikabidi ahamie kweye ubao wa mbele ya darasa uliokuwa mweupe, na katika kuandika notisi akakutana na maelezo aliyoyaona kuwa ni ya muhimu sana na hivyo akajaribu kuyasisitiza kwa wanafunzi huku akisema "Look at the blackboard all student, i like to emphasize something here" basi mwanafunzi mmoja akageukia kwenye ule ubao mweusi wa pembeni mwa darasa lakini wenzake wakamkazia macho mwalimu huku wakitazama kwenye ubao wa mbele ambao ni mweupe mara mwalimu akamwona yule mwenzao kuwa yeye anatazama kwenye ubao wa pembeni(mweusi), mwalimu akamwambia kwa hasira "you stupid look at the blackboard" yule mwanafunzi akamwuliza "Teacher, the're two boards in the room, white board(located at front side of the room) & black board(located at left side) which one do you mean?" Mwalimu kusikia hivyo akainamisha kichwa chini kisha akaamuru wanafunzi wote kulala chini na akawapa mkong'oto kisha akawaambia "washenzi wakubwa nyie kumbe humu darasani nina mwanafunzi mmoja tu anayesikiliza ninachofundisha, ahsante sana kuiana" :laugh: