Kukandwa baada ya kujifungua

Kukandwa baada ya kujifungua

KIDOLEGUMBA

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2013
Posts
498
Reaction score
110
Habari zenu wadau,

Nina mwenza wangu ambaye anakaribia kujifungua. Kwa siku za hivi karibuni ananilalamika anaogopa kukandwa maji ya moto kwa sababu alivyojifungua mara ya kwanza anasema maji ya kukandia yalikuwa ya moto sana yalikuwa yanamuunguza ila alikuwa anavumilia maumivu, naomba kufahamishwa.

Je, hakuna njia nyingine inayoweza kutumika zaidi ya hii ya kukandwa kwa mzazi anayejifungua?
 
Kama anajifungua kawaida ni lazima akandwe maji ya moto ili kurudisha mwili katika hali yake ya kawaida si lazima mimaiji iwe ya moto sana, tatizo wakandaji wengine wanakomoa. Huyo mkandaji wa mwanzo badala ya kumkanda alikomesha ndio maana anaingia woga. H

Hata mie yalinikuta hayo uzazi wa mwanzo, kwa uzazi uliofata nilitafuta mwingine
 
nijuavyo mimi,kama mwanamke kajifungua kwa operation hawezi kandwa lakini kama kajifungua kawaida ukandaji wa maji moto asubui na jioni kwa muda wa wiki mbili na kulifunga tumbo muda wote husaidia kumrudisha mwanamke kwenye hali yake ya mwanzoni kabla ya kubeba ujauzito, akifanyia uzembe tumbo hubaki limening'inia vibaya
 
Sio lazima yawe ya moto sana, ya moto kiasi kuufanya mwili urudi kawaida.
 
Kwani akina mama,hawawezi kujikanda wenyewe?Wengi wamesema walitafuta watu wa kuwakanda,Sii mjikande wenyewe?
 
Kwani akina mama,hawawezi kujikanda wenyewe?Wengi wamesema walitafuta watu wa kuwakanda,Sii mjikande wenyewe?

Mtu anaweza kujikanda mwenyewe uzazi Wa pili kwasababu anakuwa ameshaelewa!
 
Mkuu ni vizuri akasaidiwa kukandwa kwani yale maji ya moto husaidia zile damu zilizobakibaki kutoka.

Ila cha msingi yasiunguze jamani..kukandwa kuna umuhimu aisee asipuuzie damu zinaweza kubaki tumboni na akapata matatizo zaidi...
 
Habari zenu wadau,nina mwenza wangu ambaye anakaribia kujifungua. Kwa siku za hivi karibuni ananilalamika anaogopa kukandwa maji ya moto kwa sababu alivyojifungua mara ya kwanza anasema maji ya kukandia yalikuwa ya moto sana yalikuwa yanamuunguza ila alikuwa anavumilia maumivu, naomba kufahamishwa, je hakuna njia nyingine inayoweza kutumika zaidi ya hii ya kukandwa kwa mzazi anayejifungua?

Sijawahi kukandwa na sijapata madhara yoyote two years now since nimejifungua,kikubwa tu nilikua naoga maji ya moto na kujisafisha vizuri,hizo ni believes na mazoea it has no any impact,

Nilikua na uoga huo,ila end of the day nikamuuliza dokta wangu by then nilikua naatend clinic kwa profesa mgaya,alinijibu tu sio lazima na sio muhimu
 
Mkuu ni vizuri akasaidiwa kukandwa kwani yale maji ya moto husaidia zile damu zilizobakibaki kutoka.

Ila cha msingi yasiunguze jamani..kukandwa kuna umuhimu aisee asipuuzie damu zinaweza kubaki tumboni na akapata matatizo zaidi...

My dada,ndio maana huwa inashauriwa kunywa vitu vya moto kama supu,maziwa,pua inasaidia kuondoa ule uchafu,
 
Habari zenu wadau,nina mwenza wangu ambaye anakaribia kujifungua. Kwa siku za hivi karibuni ananilalamika anaogopa kukandwa maji ya moto kwa sababu alivyojifungua mara ya kwanza anasema maji ya kukandia yalikuwa ya moto sana yalikuwa yanamuunguza ila alikuwa anavumilia maumivu, naomba kufahamishwa, je hakuna njia nyingine inayoweza kutumika zaidi ya hii ya kukandwa kwa mzazi anayejifungua?
Akande Maji ya uuvuguvu kisha ajifunge kanga kwa nguvu ikaze tumboni ili tumbo lipate kurejea kama mwanzo asipo fanya hivyo tumbo lake litakuwa sio zuri litakuwa tumbo tepwe tepwe.

Na awe anakula uji wa mtama wenye pilpili mtama kwa muda wa siku 40 na awe anakunywa sana supu ya kuku yenye pilpilpili mtama kwa wingi kwa huo muda wa siku40 atakuwa na afya nzuri na asikose kula mchicha na matunda na mboga zingine za majani kwa wingi ili aweze kupata maziwa ya kutosha kuweza kumnyonyesha mtoto maziwa yake ya kifuani ni dawa kwa mtoto kiafya maziwa ya mama kwa mtoto mchanga ni bora kuliko maziwa ya makopo.@KIDOLEGUMBA

Cc MziziMkavu, njoo utupe ushauri wa kitabibu kuhusu hii kitu
Kwani wewe Mtende hujuwi hayo mambo? hujawahi kuzaa nini? njoo nikuzalishe nikupe watoto 4 mapacha wawili wa kiume na wawili wa kike nikikupa mimba utazaa mapacha Double Usijaribu kwangu.
 
Akande Maji ya uuvuguvu kisha ajifunge kanga kwa nguvu ikaze tumboni ili tumbo lipate kurejea kama mwanzo asipo fanya hivyo tumbo lake litakuwa sio zuri litakuwa tumbo tepwe tepwe...

hahahaa,mkuu mimi sikukandwa wala sikufunga mavitamba wala hiyo mikanda mnayosema,kama mtu ana asili ya tumbo atakua nalo tu na kama mtu HANA tumbo atabaki kua hana,mimi sina tumbo, sijakandwa sijafunga mikanda ila nimekunywa sana supu za moto na uji,na hata ukiniangalia huwezi kujua kama nimezaa,ukiweka jukwaani nachukua taji la miss world
 
hawakandwi nowdays iwe kawaida ama operesheni
 
hahahaa,mkuu mimi sikukandwa wala sikufunga mavitamba wala hiyo mikanda mnayosema,kama mtu ana asili ya tumbo atakua nalo tu na kama mtu HANA tumbo atabaki kua hana,mimi sina tumbo,sijakandwa sijafunga mikanda ila nimekunywa sana supu za moto na uji,na hata ukiniangalia huwezi kujua kama nimezaa,ukiweka jukwaani nachukua taji la miss world

hahahaa Mtende bana fasta umejipiga promo hongera:A S 11:
 
Last edited by a moderator:
hahahaa,mkuu mimi sikukandwa wala sikufunga mavitamba wala hiyo mikanda mnayosema,kama mtu ana asili ya tumbo atakua nalo tu na kama mtu HANA tumbo atabaki kua hana,mimi sina tumbo,sijakandwa sijafunga mikanda ila nimekunywa sana supu za moto na uji,na hata ukiniangalia huwezi kujua kama nimezaa,ukiweka jukwaani nachukua taji la miss world

nakupongeza kwa kufuata ushauri wa dc. Manake nikimsoma Mzizi,v2 vngne kjjn havpatkan hayo masupu,ma pilipili manga kwngne hakuna na wzee wetu wanawazalisha tuu na kuwakanda kawaida bila mbwembwe nyng na mwsho tumbo hali tepeti.

Mi nadhan na desturio na Mazoea tuu,sio wote wanafunga tumbo kwa matambala,Wengne wanajfngua kwny mazngra magum,Mungu ndio anajua lkn wao wala hizo mbwembwe hawakufanyiwa.
 
asante mkuu,sasa hao mapaca ntawapataje maana napenda kweli twins
Ningojee nije nikupe hao mapacha mimi pia nimezaliwa mapacha ila mwenzangu amesha kwenda Akhera tangu mwaka 1991. Umenikumbusha pacha mwenzangu ahhh machozi yananitoka nime m -miss sana ukitaka fanya subira nikirudi nikupatie zawadi ya mapacha hhahahahah Mtende

kumbe mkuu wewe ni uzao wa pacha,may he/she rest in peace,pole sana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom