Ni Kwanini unaamini kwamba hawakuomba kibali je umeshindwa kuwapigia na kuwauliza au una kinyongo nao tangia walipokuudhi?
Kama wanakamatwa na kushinda kesi mahakamani unajifunza nini juu ya aliyewakamata? Umesema Watu waongee fact ambalo Ni jambo jema unadhani wewe umeongea fact gani? Uko Canada na unajua siasa za vyama vingi Tanzania Ni Kweli hukusikia Raisi aliposema hakuna mikutano ya hadhara?
Wakati ule unatangaza list of shame ulipata kibali? Unadhani leo unaweza kuwa na nafasi hiyo kama hiyo bila kuwekwa ndani? Unadhani wakati wote ulipowekwa ndani ulikuwa hukufuata taratibu?
Ndipo Chama kilipofika baada ya kuondolewa viongozi makini kwa bei ya kunde kisa njaa ya siku moja.Dr.Slaa kama ilivyo jadi yake ametoa somo. Kaomba pia aelimishwe kwenye maeneo tunayoona kuwa kwa hoja aliyotoa kapitwa na wakati.
Kama viongozi waliokamatwa walitimiza matakwa yote ya kisheria waweke hadharani taarifa zao.Kama polisi walikosea kawapa tahadhari na madhara ya hatua hizo.Nini kinakufanya utukane au uhoji mahali alipo? je ukiwa nje ya Tanzania unauza utanzania wako?