Kukaliwa na mwanamke

Kukaliwa na mwanamke

benteke, lazma Kuna mdada unamtongoza humu. Hii si bure kabisa. Naamini kwa sredi hii ameshakupa maksi.

hahahaha...... umenifungua macho aisee. Ngoja niangaze kama kuna mmoja anaweza volunteer .
 
Ukiona mtu anazo hizo tabia ujue ni wale walio balehe maumbo ila akili zao bado ni za kitoto.
Tena hata hawajui maana ya ndoa, mke wala baba wa familia ni nini! Yaani kwa ujumla hata hawajui kwa nini wako duniani yaani hawa ni watu wanaojaza dunia bila kuwa na impact hata kwa viumbe waliovileta!
Bibi yangu alikuwa anawakemea wajukuu zake wa kiume akiwaambia hata ng'ombe ana thamani! Atakupa maziwa, nyama na mengineyo lakini si nyie mnaoshinda baa nyumbani wala pesa haionekani nyumbani!
 
Usikubali kuogopa kumuonyesha mke wako au girlfriend wako unampenda kisa unaogopa washikaji au ndugu watakusema umekaliwa naye.

Ni tabia mbaya sana unakuta mtu mzima eti anajitamba mbele za wanaume eti "mimi bwana mwanamke hawezi niuliza niko wapi" sasa ndugu yangu wewe ndio ulimtongoza mwenyewe tena ulimsumbua hasa msichana wa watu leo hii anakupigia simu anakuuliza uko wapi unaanza kupanic.

Tusifanye vitu ili kuwaridhisha washkaji huko viringeni, tufanye vitu kuwaridhisha wake zetu, imefikia wakati mwanaume usipokaa bar mpaka saa nane au saa saba usiku unaonekana na ukiangalia ligi ya ulaya sebuleni kwako na mke wako unaonekana pia au usipokua na demu wa nje eti wewe sio mjanja.

Huu ni upuuzi tubadilikeni jamani. Ndio sikatai usikae na washikaji lakini usipitilize sasa.

Naona huruma sana unakuta mtu kavaa lipete likubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia.

benteke nimekupenda bure
 
Last edited by a moderator:
kwani kuna tatizo mtu akiosha na kupiga deki nyumbani kwake?!!!...mimi napika, nafua nguo...hakuna kazi nayoipenda kama kuogesha watoto wangu!
Tatizo hakuna...tatizo ni kuchochea ugomvi kwa wanaume wenzio kumbe kwako ni mume mtiifu...
 
 
Last edited by a moderator:
tinna mrembo.. sasa mwanaume hataki aulizwe yuko wapi na mke wake si kituko hicho. Tena napaaza sauti katikati ya wanaume wenzake. Ni ujinga sana. Sasa asiulizwe yuko wapi kwani yeye ni nani hapa daslam. Mengi mwenyewe anaulizwa na Jaki.
ivoo, haya.
 

Naona huruma sana unakuta mtu kavaa lipete likubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia.
hili tunalifanyaga mamawatoto akitupanda kichwani, nyumbani hakulaliki, gubu!

Chai ofisini, mchana hukohuko, jioni bar, usingizi unaanzia bar unaamkia home kubadilisha nguo.
 
Inferiority complex ndiyo tatizo pia au mtu km alizoea nafasi duni kwenye hatua mbalimbali za maisha yake ndiyo huwa na hayo mambo sana......

Ila pia mwanamke ukimuendekeza hachelewi kukukalia kichwani na kuanza kukufanyia maamuzi.....

Cha muhimu ni kuishi nao kwa akili bila kutawaliwa na mihemko.

N:B siyo wote waangaliao mpira nje ya nyumbani au kukaa bar muda mrefu wanawaonesha wake zao uanaume, ,,,,,wengine ni sehemu ya maisha yao ,na kumbuka maisha hapana formula.
 
Ukiona mtu anazo hizo tabia ujue ni wale walio balehe maumbo ila akili zao bado ni za kitoto.
Tena hata hawajui maana ya ndoa, mke wala baba wa familia ni nini! Yaani kwa ujumla hata hawajui kwa nini wako duniani yaani hawa ni watu wanaojaza dunia bila kuwa na impact hata kwa viumbe waliovileta!
Bibi yangu alikuwa anawakemea wajukuu zake wa kiume akiwaambia hata ng'ombe ana thamani! Atakupa maziwa, nyama na mengineyo lakini si nyie mnaoshinda baa nyumbani wala pesa haionekani nyumbani!
Kwahiyo pesa ikionekana nyumbani ruksa kushinda bar siyo?
 
Back
Top Bottom