Kukaliwa na mwanamke

Kukaliwa na mwanamke

benteke

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
1,305
Reaction score
1,069
Usikubali kuogopa kumuonyesha mke wako au girlfriend wako unampenda kisa unaogopa washikaji au ndugu watakusema umekaliwa naye.

Ni tabia mbaya sana unakuta mtu mzima eti anajitamba mbele za wanaume eti "mimi bwana mwanamke hawezi niuliza niko wapi" sasa ndugu yangu wewe ndio ulimtongoza mwenyewe tena ulimsumbua hasa msichana wa watu leo hii anakupigia simu anakuuliza uko wapi unaanza kupanic.

Tusifanye vitu ili kuwaridhisha washkaji huko viringeni, tufanye vitu kuwaridhisha wake zetu, imefikia wakati mwanaume usipokaa bar mpaka saa nane au saa saba usiku unaonekana na ukiangalia ligi ya ulaya sebuleni kwako na mke wako unaonekana pia au usipokua na demu wa nje eti wewe sio mjanja.

Huu ni upuuzi tubadilikeni jamani. Ndio sikatai usikae na washikaji lakini usipitilize sasa.

Naona huruma sana unakuta mtu kavaa lipete likubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia.
 
benteke kumbe ukitulia huwa unaweza kuandika mambo ya maana sana...
 
Last edited by a moderator:
Mie hili swala la watu kukaliana ama akukaliwa sielewagi maana yake ni nini hasa. ila nikionacho ni kunawatu wanataka kujionyesha vidume kumbe hata kwenye udume hawapo. heshima haiji kwa kuwqa mwamba ama mbabe heshima inajengwa na aina ya uwajibikaji mtu alionao. Mbaya zaid kuwajibika kwenye maisha hakunaga kuwajibika kwa wastati its either you do it perfect or not perfect.
 
benteke sijakuona muda aisee! Naona umekuja kivingine sasa.
 
Last edited by a moderator:
Mie hili swala la watu kukaliana ama akukaliwa sielewagi maana yake ni nini hasa. ila nikionacho ni kunawatu wanataka kujionyesha vidume kumbe hata kwenye udume hawapo. heshima haiji kwa kuwqa mwamba ama mbabe heshima inajengwa na aina ya uwajibikaji mtu alionao. Mbaya zaid kuwajibika kwenye maisha hakunaga kuwajibika kwa wastati its either you do it perfect or not perfect.

Aaanh asee wapo bhana wanaokaliwa wake kwa waume!!!
Mie natoka jamii ya mfumo dume lakini nashukuru nimepita madarasani kiasi kwa hiyo naona jinsi mifumo invyofanya kazi ingawa hatutopata definition moja ya concept hii ila kama "Gender studie" ipo na inakubalika basi kukaliwa pia kupo!!!

1. We mwanaume na sharubu aamke kumi na nusu, deki, vyombo, fua, pika chai, oga nenda job jua na mvua na mkewe mama wa nyumbani hii ni nini kwa mfano??!!!

2. Mama anaamka anaandaa watoto, waende shule aandae chai ya mumewe, atoke mpaka sokoni na beseni anachukua matango, machungwa na mihogo huyo mpaka magerejini anazunguka kuuza na mtoto mdogo mgongoni mume kalala tuu akitoka hapo kucheza bao na karata, abishanie Simba na Yanga tu jioni amarudisha suruali home na anataka wali syenzi type!!!

Asee wapo wanaokaliwa wengine kwa mabavu wengine kisaikolojia na wengine vyote kwa pamoja
 
Sikuhizi umeacha unyanyapaa wa mapenzi..huhuu kweli benteke umekua
 
Ila kuna wanaume hawapendeki kutwa kashfa! kashfa tu na uroho Baaasi ! :tongue: Ogopa sana Mwanume ambaye anapenda sana kusema mimi mwanamke hawezi fanya hivi , mimi mwanamke hawezi kuniuliza /kunipangia fyoko fyoko yaani kama ndio Boyfriend please toka Nduki hawafai!
 
Kiukweli hii dhana ni potofu pale unapoonyesha upendo kwa mwenzi wako halafu punguani wanakuona umekaliwa au kutawaliwa, ilishatokea mjadala kama huu siku moja tupo msibani nikawa natetea upande wa mwanamke......nilikoma......nilishambuliwa nikaona kumbe hili tatizo ni kubwa katika jamii.........kama alivyosema benteke tubadilke.
 
@Kanigini nipo. Nimeamia Kigamboni nyumba haina umeme basi balaa tupu.

Umeshafanya mazoezi ya kupiga mbizi? Maana kivuko hakichelewi kubuma.

Nunua solar mkuu, mimi ninaishi Malamba Mawili (Mbezi kama unaenda Kinyerezi) nina solar yangu, sina hata habari za mgao, luku imeisha nk.
 
Maneno yana afya haya benteke

tinna mrembo.. sasa mwanaume hataki aulizwe yuko wapi na mke wake si kituko hicho. Tena napaaza sauti katikati ya wanaume wenzake. Ni ujinga sana. Sasa asiulizwe yuko wapi kwani yeye ni nani hapa daslam. Mengi mwenyewe anaulizwa na Jaki.
 
Hilo unalolisema wewe umeliseme aupande mmoja. Mfano mie napenda mume awe mkali kwangu yaani mume soft touch simuwez kabisaa. napenda mumea ambaye akisema najua hapa hubby kasema na kwakauli hii siwez kwenda kulia ama kushoto. mwingine atasema mume wangu kanikali lakin ukweli si kwamba kanikalia ila ndo dizaini ya mtu nimpendae. uchagani wanawake hasa wa bibi kama siye tumelelewa kama wachapa kazi wa familia na ni ukweli bila kuamka na kwenda kufagia zizi la ngombe, nikamue, nilishe mifugo nipike chai ndipo nioge kwenda job sioni kama nimejitendea haki. na hii sio nalazimishwa najua kwamba ni wajibu wangu kila siku. kuna desturi za wengine wanaume ndio wasaidizi wa wake zao. na naomba niseme hili wazi \(muslim husbands wanaongoza kwa mapenzi ya dhati wka wake zao) wao ndo waenda sokoni, wanaokwenda kushop na wake zao wanakaa home kuzidi kupendeza. mie kwangu kati ya hii miwili sion kama ni kukaliwa unless kama mmojawapo atakuwa analalamika
Aaanh asee wapo bhana wanaokaliwa wake kwa waume!!! Mie natoka jamii ya mfumo dume lakini nashukuru nimepita madarasani kiasi kwa hiyo naona jinsi mifumo invyofanya kazi ingawa hatutopata definition moja ya concept hii ila kama "Gender studie" ipo na inakubalika basi kukaliwa pia kupo!!! 1. We mwanaume na sharubu aamke kumi na nusu, deki, vyombo, fua, pika chai, oga nenda job jua na mvua na mkewe mama wa nyumbani hii ni nini kwa mfano??!!! 2. Mama anaamka anaandaa watoto, waende shule aandae chai ya mumewe, atoke mpaka sokoni na beseni anachukua matango, machungwa na mihogo huyo mpaka magerejini anazunguka kuuza na mtoto mdogo mgongoni mume kalala tuu akitoka hapo kucheza bao na karata, abishanie Simba na Yanga tu jioni amarudisha suruali home na anataka wali syenzi type!!! Asee wapo wanaokaliwa wengine kwa mabavu wengine kisaikolojia na wengine vyote kwa pamoja
 
Umeshafanya mazoezi ya kupiga mbizi? Maana kivuko hakichelewi kubuma.

Nunua solar mkuu, mimi ninaishi Malamba Mawili (Mbezi kama unaenda Kinyerezi) nina solar yangu, sina hata habari za mgao, luku imeisha nk.

Nafikiria nifanye hivyo ila kuna majamaa yamenikatisha tama yameniletea quotation utafikiri nafunga kiwandani..ntaenda kariakoo mwenyewe...ila asikuambie mtu nakesha nje usiku kucha kama mchawi. maana kuna vibaka balaa.
 
Back
Top Bottom