Kukabwa usiku ukiwa umelala

Millifire69

Member
Jul 8, 2021
94
109
Kwanza niwatoe hofu kwa wale wote ambao wamepatwa na Hali hii na kudhani ya kuwa ni mambo ya kishirikina, kisayansi Hali hii inaitwa SLEEP PARALYSIS.

Sleep paralysis ni Hali ambayo inawapata watu wakati wa kuamka au kulala, ambapo fahamu za mtu zinakuwa zikifanya kazi lakini mtu huyo anakuwa amepooza kabisa. Hali hii inapompata mtu, mtu anaweza kupata maono ya ajabu aidha kwa kusikia, kuhisi au kuona vitu ambavyo havipo, Mara nyingi sleep paralysis huchukua dakika chache tu, hazizidi 3, Hali hii inaweza kuwapata wenye afya njema au walio na ugonjwa wa nakolepsia.

Dalili
🐾 Kutoweza kusogea au kuzungumza wakati wa kuamka.

🐾 Kusikia sauti zisizo na uhalisia kama vile mivumo, kama kelele za nyoka hivii, king'ora flani hivi...nk

🐾 Kupata hisia kama unavutwa kutoka kwenye kitanda kwa nguvu

🐾 Kuhisi uwepo wa viumbe vya ajabu katika chumba ulicholala

🐾 Kupata hisia ya kupaa angani

🐾 Maumivu ya kifua na kichwa, unaweza kuhisi kama kuna uzito kifuani.

Mara nyingi Sleep paralysis inasababishwa na kukosa usingizi unaoshauriwa na wataalamu wa usiopungua masaa 8. Kama wewe unalala below masaa 8 unahatihati ya kupata sleep paralysis.

Pia ulevi na msongo wa mawazo vinaweza kuwa visababishi.

Asanteni sana naamini mmepata elimu nzuri. Good evening to every one.! ✊
 
Kuna uhusiano wa moja kwa moja na nguvu za giza, wana sayansi ndio wanaongea hayo yako,ila katika ulimwengu wa roho unakuwa hauko salama..
 
Kuna uhusiano wa moja kwa moja na nguvu za giza,wana sayansi ndio wanaongea hayo yako,ila katika ulimwengu wa roho unakuwa hauko salama..
Sipingani na mambo ya giza, ila kwa taaluma niliyonayo hayo ni maelezo sahihi, kama unakabwa usiku kabla hujafikiria hayo mambo ya giza, lala usingizi zaidi ya masaa nane, fanya mazoezi ilikuepuka msongo wa mawazo, punguza vilevi, endapo utaendelea kukabwa pengine inabidi sasa uangazie upande wa pili. 🙏
 
Back
Top Bottom