Wangapi kati yenu wanakumbuka waliyokuwa wakiyafanya wakati wana umri wa mwaka 1-3?????
kuna kavulana ka kike?Kavulana ka-kiume....lol
Unakumbuka kitu gani?
Ok, lakini nilitaka hata ungenitajia viwili vitatu tuu ili vinisaidie ku-Cement ushauri ninaopata kutoka kwa wadau
Mimi ningesema kuanzia miaka 2+ hivi. Mimi binafsi sipendi kukaa uchi mbele ya mtu yoyote bila sababu ya msingi. So hata kama inanilazimu kubadili nguo mbele ya mtoto nitajifunga taulo au kanga ya mama yake lakini sio kukaa uchi kabisa.Wadau naomba kuuliza kuna kitu kina nitatiza, mimi nina mtoto mchanga wa miezi13 yaani mwaka mmoja na mwezi mmoja, tokea kazaliwa huwa nafanya jambo lolote mbele yake kama vile kubadirisha nguo mbele yake, kukaa uchi mbele yake na kuchezacheza kikubwa na mama yake ilihali yeye anachezacheza kitandani na anatutazama. Nimeanza kuwa na wasiwasi kwamba huenda anatuchora, je ni katika umri gani wa mtoto natakiwa nisikae uchi mbele yake wala kucheza michezo ya kikubwa na mama yake?