KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Tukiyaangazia macho kwa majirani zetu Sudani ambao wanaongozwa na Omar Hassan al-Bashir kutoka mwaka 1989 -2019 chini ya chama chake cha ‘ National Congress Party( NCP), waliamua kufanya maandamano ya Amani ya kumuondoa kiongozi huyo wa muda mrefu na mwisho jeshi kutwaa madaraka.
Si Sudan tu ambapo jeshi limetwaa madaraka kwa muda baada ya wananchi kuandamana kushinikiza viongozi wa serikali zao kuondoka madarakani baada ya kuchokwa kwa kukaa muda mrefu madarakani, Zimbambwe ni mfano mwingine ulio karibu.
Licha ya kwamba wananchi hao wanaandamana kuwatoa viongozi wao lakini cha kushangaza ni kwamba bado wanaendelea kukichagua chama cha kuongozi huyo licha ya kuwa na chenyewe kimekaa muda mrefu.
Hili halina ubishi kuwa hapa Tanzania wanaokaa na kusema kuwa CCM wajiandae watakuwa hawauoni huu mtiririko wa hayo matukio vizuri au wameamu kuficha ukweli kwa kukumbatia uongo. Si Magufuli wala CCM ambao wananchi wameichoka na kuwa katiba inasema kuwa kiongozi kwa ngazi ya Urais atakaa madarakani kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano mitano, huo muda ni wa kikatiba na haufanyi wananchi wakamchoka kiongozi wao.
Tatizo la msingi ambalo wengi wanajaribu kulificha ni kuwa wananchi wameanza kuwachoka viongozi wakuu wa vyama vya upinzani yaani CUF na CHADEMA kwa kukaa madarakani muda mrefu na hiyo hali ndio naweza kuifananisha na huko wanapofanya maandano ya kuwaondoa viongozi
Sudani na Zimbabwe zimewasha taa nyekundu kwa viongozi wa CHADEMA na CUF na si kwa CCM na Magufuli, ni kwa sababu watu wanachoka kuwa na kiongozi mmoja kwa muda mrefu na si kuwa na chama kimoja muda mrefu. Ingekuwa watu wanakichoka Chama basi ZANU-PF ya Zimbabwe isingerudi madarakani baada ya Robert Mugabe kuondolewa.
Wito
Vyama vya siasa muwe na tabia ya kubadili viongozi wenu baada ya muda ili wanachi wasiwachoke na kupelekea kufanya maandamano ya kushinikiza viongozi wenu watoke na kugeuka kuwa aibu kwenu na kwa Chama.