Kukaa karibu na minara kuna madhara yoyote ?

Kukaa karibu na minara kuna madhara yoyote ?

2in1

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Posts
224
Reaction score
109
Habari zenu wakuu, hivi kukaa karibu na minara hii inayojengwa humu mitaani kuna madhara yoyote? na je kama kuna madhara kwanini wanajenga karibu sana na makazi ya watu?
 
Habari zenu wakuu, hivi kukaa karibu na minara hii inayojengwa humu mitaani kuna madhara yoyote? na je kama kuna madhara kwanini wanajenga karibu sana na makazi ya watu?

Hiyo ilishakanushwa sana na wataalam ikiwemo tcra wenyewe
 
Haina madhara, radio waves ni very weak kusema zinauwezo mfano wa ku-cause kitu kama cancer, itahitaji massive energy kuweza kubreak bond kwneye DNA, infact radio waves zina nguvu ndogo sana kuliko hata Ultraviolet light,

ni kweli kua ikiwa katika very high concentration inaweza sababisha heat increase kwenye tissues, lakini still si for the case ya hii mitandao, hii haina concentration kubwa kiac hicho.... sanasana ukiishi karibu utapokea reception nzuri net ya faster
 
Haina madhara, radio waves ni very weak kusema zinauwezo mfano wa ku-cause kitu kama cancer, itahitaji massive energy kuweza kubreak bond kwneye DNA, infact radio waves zina nguvu ndogo sana kuliko hata Ultraviolet light, ni kweli kua ikiwa katika very high concentration inaweza sababisha heat increase kwenye tissues, lakini still si for the case ya hii mitandao, hii haina concentration kubwa kiac hicho.... sanasana ukiishi karibu utapokea reception nzuri net ya faster
kaka minara si inatumia microwaves au
 
Habari zenu wakuu, hivi kukaa karibu na minara hii inayojengwa humu mitaani kuna madhara yoyote? na je kama kuna madhara kwanini wanajenga karibu sana na makazi ya watu?

madhara unayoweza kupata,ni kelele za majenereta,ikiwa kama umeme wa tanesco haupo,au kuna low voltage,minara hii imetengenezwa kiasi kwamba kama umeme unakuwa mdogo,jenereta inawaka na kutembea mpaka hari ya umeme itakapo kuwa katika viwango vilivyosetiwa,
 
Madhara yapo tena makubwa. ukiwa karibu na mnara radition zinazokupiga ndio zinasababisha cancer. unatakiwa uwe distance ya angalau mita 12 ambapo tunaweza kusema energy yake huwa imepungua. lakini si kila mita 12 utakuwa safe.... no.... inategemea na power ya huo mnara unavyo radiate.

kule ulaya TCRA wa kule wameweka vigezo vya max power for mnara tu radiate na wanafatilia. Base station zao zipo hapo kwa hapo haziko mbali mbali kama hukku kwetu. hivyo zinarusha (zinaradiate) minimum power possible. too costly.... huku kwetu minara ipo mbali mbali mno. kwa maana single mnara unarusha maradiation makubwa ili ku cover area kubwa.

TCRA wa huku kama waliolala vile.

kwa ufupi katika nchi nyingi ambazo hazijaendelea minara inarusha power nyingi mno. na ni busara kuwa mbali nao.
inawaathiri zaidi watoto kwani wao miili yao haijakomaa.

Better to stay very far from minara . you have been warned
 
Kwa wadada huwaletea madhara kama vile mimba na kadhalika......
 
Haina madhara, radio waves ni very weak kusema zinauwezo mfano wa ku-cause kitu kama cancer, itahitaji massive energy kuweza kubreak bond kwneye DNA, infact radio waves zina nguvu ndogo sana kuliko hata Ultraviolet light, ni kweli kua ikiwa katika very high concentration inaweza sababisha heat increase kwenye tissues, lakini still si for the case ya hii mitandao, hii haina concentration kubwa kiac hicho.... sanasana ukiishi karibu utapokea reception nzuri net ya faster
kaka radiation za mobile phone tu zina madhara makubwa kiasi je Hiyo minara yenyew ambayo inaemit hizo radiations itakosa madhara kweli!
 
Madhara mengine ni mara kwa mara utakuwa una nyoosha shingo macho juu kutazama juu ya mnara, baada ya muda wa miaka utakuwa unatembea macho juu juu mita mia kama mtu anayetafutwa na polisi.
 
Madhara mengine ni kama tezi dume nakadharika
 
Madhara mengine ni mara kwa mara utakuwa una nyoosha shingo macho juu kutazama juu ya mnara, baada ya muda wa miaka utakuwa unatembea macho juu juu mita mia kama mtu anayetafutwa na polisi.

Hahahahhaaha dah! Kazi ipo
 
Back
Top Bottom