Kujuana na watu wengi(Networks)!!!!

Kuna tofauti ya kujuana na rafiki. Rafiki ni Yule anayeweza kuwa nawe wakati wa dhiki, kujuana ni Yule anayekujua na si lazima awepo wakati wa dhiki ila Mara nyingi Yuko wakati wa raha.

Fanya kile unachotaka. Michango ya harusi, kipaimara ni matumizi mabovu ya hela hivyo Probability ya kupata ni karibu na Zero hata kwa familia yangu.
Mkuu nimekuelewa vema ila sasa nataka nifanye maamuzi magumu
 
Wadau mwenzenu nimejaaliwa kuwa na marafiki wengi sana ukiachilia mbali wale niliofahamiana nao katika maisha ya shule na nika-maintain urafiki nao, lakini bado katika mazingira ya kazi na maisha ya mtaani napendelea sana ku “keep in touch” na watu wengi sana ambao nakutana nao. Kama mjuavyo watu wengi maisha huanza kwa kuwa wapangaji, hapa Dar maisha nilianzia Manzese nilikaa mwaka mmoja na nikajikuta nina marafiki kibao, nikahamia Sinza nikapata marafiki kibao, Nikahamia Tabata nikajipatia marafiki kibao, nikahamia Mbezi Tank Bovu nikajipatia marafiki pia, na mwisho nipo Tegeta nako nimepata marafiki wapya wengi tuu na kama kawaida huwa na “keep in touch” Miaka yoote nimekuwa nafanya hivyo kwa makusudi kabisa kwasababu nimekuwa nikisikia kwamba kujuana na watu wengi(Networks) ni kitu muhimu sana.

Mpaka sasa sijajua umuhimu wa kujuana na watu wengi zaidi ya Usumbufu, kwa mfano hapa nilipo nina kadi kumi na nane 18 za michango ya Harusi, Send offs, Vipaimara, Anniversaries nk. Haishii hapo nina SMS Tatu zinaniomba nihudhulie hizi weekend mbili bila kukosa vikao vya kwanza vya Harusi na Sendoffs.

Kujuana na watu wengi kumenifanya ghalama zangu za kuishi ziwe kubwa sana. Nifanye nini ili uwingi wa marafiki zangu na mimi uninufaishe???

Anza kuwaomba misaada utaona taratiibu wataanza kujikata,na utajikuta uko hulu hautapata usumbufu tena.
 
As of me ni kama vile unajuta kuwa na marafiki...
Ulimaanisha marafiki au just people you know??? Maana kuwa na marafiki kila unapoenda ni kazi nayo as inataka muda sana kukutana oftenly, kuzoeana na mpaka muwe marafiki. Or else you mean unafahamiana na watu wengi

To your topic
1.Never regret kuwa na marafiki wengi as ndo hao utacelebrate nao na kulia nao as well although kuna exception to every general rule thus dissapointment yaweza tokea pia
2. Marafiki hawawezi kwa of equal weight so waweke kwa uzito wao na hapo ndo litakapokuja suala la michango utajua give and take ballance inakuelekeza wapi uto na wapi upige ndiiii
 
Unajuana na watu ambao hawaleti faida. Jifunze kuwa selective unapotengeneza network.
 
Pole sana mkuu,
Nakushauri changia kutokana na uwezo wako, usifanye kuchangia kufurahisha marafiki/jamaa zako wakati huna huo uwezo.

Mimi binafsi huwa nachangia zaidi ndugu zangu wa karibu na baadhi ya marafiki kwenye mambo ya sherehe na shughuli nyinginezo, ila hao wengineo huwa natoa msaada/mchango endapo tu mtu anaumwa/ada (amefukuzwa shule)/imemtokea shida ambayo nafahamu kabisa huyu mtu hana uwezo naweza kumsaidia kwa hayo tu na sio mambo ya sherehe yoyote, kitchen party au send off.
:A S-coffee:
 
Huu utamaduni wa kuchangiana harusi kwakweli itabidi ufe

La msingi zichuje angalia za muhimu wape mchango wengine wachunie maana siku hizi mtu hata ukikutana kwenye daladala ukisalimiana nae ukamchekea anakupa kadi anakwambia mpwa wake anaoa/olewa
keshakwambia wote huwa anakip intouch na kila mtu kwake ana umuhimu
 
Wadau mwenzenu nimejaaliwa kuwa na marafiki wengi sana ukiachilia mbali wale niliofahamiana nao katika maisha ya shule na nika-maintain urafiki nao, lakini bado katika mazingira ya kazi na maisha ya mtaani napendelea sana ku “keep in touch” na watu wengi sana ambao nakutana nao. Kama mjuavyo watu wengi maisha huanza kwa kuwa wapangaji, hapa Dar maisha nilianzia Manzese nilikaa mwaka mmoja na nikajikuta nina marafiki kibao, nikahamia Sinza nikapata marafiki kibao, Nikahamia Tabata nikajipatia marafiki kibao, nikahamia Mbezi Tank Bovu nikajipatia marafiki pia, na mwisho nipo Tegeta nako nimepata marafiki wapya wengi tuu na kama kawaida huwa na “keep in touch” Miaka yoote nimekuwa nafanya hivyo kwa makusudi kabisa kwasababu nimekuwa nikisikia kwamba kujuana na watu wengi(Networks) ni kitu muhimu sana.

Mpaka sasa sijajua umuhimu wa kujuana na watu wengi zaidi ya Usumbufu, kwa mfano hapa nilipo nina kadi kumi na nane 18 za michango ya Harusi, Send offs, Vipaimara, Anniversaries nk. Haishii hapo nina SMS Tatu zinaniomba nihudhulie hizi weekend mbili bila kukosa vikao vya kwanza vya Harusi na Sendoffs.

Kujuana na watu wengi kumenifanya ghalama zangu za kuishi ziwe kubwa sana. Nifanye nini ili uwingi wa marafiki zangu na mimi uninufaishe???

Ajipatiaye marafk wengi ajitengenezea mwnyw shimo la uharibifu. Kwa ushaur wangu kua makin na hao marafk coz c wote unawafaham undan wao!
 
Back
Top Bottom