Kujivua gamba ni heshima kwa chama - Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujivua gamba ni heshima kwa chama - Mwakyembe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Moses Mabula, Tabora

  NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba kitendo cha Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujivua Gamba kimeleta heshima ndani
  chama hicho.

  Alisema kuwa kitendo hicho kimerudisha imani na heshima kubwa ndani ya chama hicho, na wananchi kwa ujumla hivyo wapenzi na wanachama wa CCM wakipe kura za kutosha katika Uchaguzi Mkuu 2015.

  Dkt. Mwakyembe aliyasema hayo wakati akihubia wananchi
  mjini Tabora ambapo alisema kuwa kumekuwepo na maneno mengi kuhusu kujivua gamba kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho taifa.

  Alisema kuwa kitendo hicho kinafaa kuigwa na watu wengine ili kuimarisha uhai wa chama.

  "Kitendo cha kujivua gamba hakina maana kwamba viongozi waliojivua ni wachafu hapana bali ni utaratibu wa kukijenga chama msije mkasema hao wote waliojivua walikuwa na makosa ndani ya chama ni watu wasafi na waadilifu.

  "Nawashangaa sana hawa wapinzani wanapiga kelele nyingi kuwa eti kujivua gamba ni kuvua uchafu nawaomba wasiigilie ni bora wakae kimya wasiingilie mambo yasiowahusu" alisema Dkt. Mwakyembe.

  Kuhusu ujenzi wa barabara hapa nchini Dkt Mwakyembe alisema kuwa Serikali imejipanga vilivyo kuhakikisha kwamba barabara zote ambazo zimo katika mpango kujengwa, kazi hiyo inaanza mara moja ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

  Alisema kuwa serikali kuanzia sasa itakuwa makini kwa wakandarasi wazembe na ambao kazi zao huwa zinafanyika kwa kusuasua ili kama wakibainika kufanya hivyo wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

  Kuhusu uimara wa barabara zinazojengwa chini ya alikiri kuwepo kwa
  hali hiyo na kuwataka Wakala wa Barabara nchini (TANAROADS) kuwachukulia hatua kali, bila kuwaonea haya wakandarasi wazembe.

  "Ninatoa maagizo kwa Mameja wote wa TANROAD hapa nchini wakaangeni wakandarasi wa hali hiyo kwani lwawama hizo zinaelekezwa kwetu na sio wao.

  Hata hivyo aliwataka wananchi waliojenga ndani ya Hifadhi ya Barabara umbali wa mita 22.5 kubomoa haraka wenyewe lasivyo nyumba hizo zitabomolewa na serikali kwa nguvu bila kujali sura ya mtu wala cheo chake.
   
 2. k

  kaiyurankuba Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: May 16, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe please! Nini kimekukumba?
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Asante Mwakyembe nimekuelewa sasa;kumbe kuna magamba masafi na machafu?
  Hayo masafi kwanini mmeyavua?au yamezeeka na nyie hamtaki magamba mazee?hayo magamba mazee yameisha?
  Hayo yasiyo machafu ni yapi tusije tukayahukumu pamoja na machafu?
  Unawaita "viongozi waliojivua gamba",kwani wamejivua ama wamevuliwa?ni chama kimejivua ama viongozi wamejivua gamba?
  Kama hamtaki wapinzani waseme kujivua gamba ni kujivua uchafu mnataka wasemeje?
   
 4. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  So what?
   
 5. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  ninasashaka na MWA anaelekea kule alipokuwa anapapigia kelele kuwa ni pabovuu nini? amakweli ****** alitumia akili kumshatap mdomo!
   
 6. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mweeeee
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Wizara ya Ujenzi ndugu yangu, kitovu cha tatu cha ufisadi nchini ukiacha Maliasili na utalii, Nishati na madini. Hapo pesa ni bwelele ilmradi tu hupigi zile kelele za kinyume. Na hapo hata mwaka hajamaliza.
   
 8. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  huyu bwana Mwakyembe sikudhani kama angeanza kuwatetea mafisadi... kumbe amepata pa kuweza kuchuma pesa naye ametugeuka katika vita dhidi ya mafisadi??? kazi ipo...tuna safari ndefu, mungu atusaidie
   
 9. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,283
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Mpambanaji kamung'unya maneno.

  Ni nguvu ya EL au tamu ya uwaziri?
   
Loading...