"kujivua gamba"... Dhambi ya kumuua kolimba!

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,658
3,646
Habari wakuu,
Mnamo mwaka 1997 aliyekuwa katibu mkuu wa CCM marehemu Horace Kolimba aliwahi kutoa kauli kwamba CCM haikuwa na dira wala mwelekeo. Kauli ambayo vigogo wa juu wa CCM walikuja juu kwamba amekidhalilisha chama. NEC wakamwita ajieleze!! Akaitika wito akajieleza na baada ya maelezo akaanza kujisikia vibaya na akafa siku hiyohiyo. Lengo langu si kukumbushia jinsi kifo kilivyotokea bali ni kuelezea umuhimu wa kuyafanyia kazi mawazo ya mtu hata kama ni mabaya kiasi gani.
Laiti kama wangemuuliza Kolimba ajieleze kiufasaha na si kwa shinikizo, lawama na hamaki kisha na yeye akatolea ufafanuzi wa kina kwa kauli yake hiyo, leo tusingesikia CCM ina programme ya kujivua gamba..... Matokeo ya kujivua gamba ni dhambi ya kumuua Kolimba. Wangeyafanyia kazi mawazo yake leo hii kusingekuwapo mpasuko huu uliopo ccm na ufisadi huu wa kutupwa ndani ya serikali usingalikuwapo. Na dhambi hii itaendelea kuwatafuna mmojammoja mpaka chama kitakufilia mbali ingawa kikifa watakimbilia CDM kuendeleza ulaji...sijui watapokelewa?
Niisie hapo.
Nawasilisha wakuu.
 
Mkuu mbona mada unayoiongelea ina pwaya pwaya!
Kolimba na kujivua gamba wapi na wapi, kuna phase difference ya karibu miaka 15 kati ya Kolimba na kujivua gamba.
Hivi Kolimba aliuwawa? tujuze, naye alinyweshwa sumu?
 
Back
Top Bottom