gambachovu
JF-Expert Member
- Dec 29, 2011
- 1,854
- 293
Mara nyingi tunasikia na kuona watu wakinyooshewa vidole kua "wanajiuza tu hao" au "anajiuza tu huyo".
Sasa nimejikuta najiuliza Je kujiuza kunaanzia wapi na kuishia wapi? Ni mpaka mtu atilie pamba matata na kusimama barabarani huku akisubiria atakaevutiwa nae atokee? Ni mpaka mtu awe na buzi ambalo linamuweka mjini? Vipi anaeoa/olewa kabisa kwasababu ya pesa na sio mapenzi. . . huyu nae anajiuza?
Hahahaah. . . watu wana vurugu kweli.mimi kuna dada nilipewa namba yake,tukawa tunawasiliana sana lakini kabla hata ya kuonana, tayari alianza kunipiga virungu vya,mara leo vocha,mara viatu na suti inayomatch kwa ajili ya ofisini...,gharama yake sijui laki na ngapi...
Sikuwahi kumtumia fedha katika ombi lake lolote...ila nililisitiza kuonana naye kwanza.. Akaanza kuuliza," Kwani we unapenda mwanamke wa aina gani..? Je, kama utaona sina vigezo unavyovitaka je?"
Tulionana na nikamwambia nimefurahi kumuona ni mwanamke mwenye vigezo vyote ninavyovitaka.. Baada ya vinywaji tukaagana..
Tulipoachana na nakafika nyumbani,alinishangaza kwa kunitumia ujumbe kuwa hakufurahia kukutana kwa kuwa sikutoa maneno yoyote ya kumhakikishia kuwa atapata uniform hiyo ya readymade kwa ajili ya ofisini kwao...
Niishie hapo.. Je,huyu atakuwa group gani?
@Konnie . . . nidai zawadi.
Tunatakiwa tutofautishe hapa,kwanza mfumo wa maisha na maumbile umewafanya wadada kuwa tegemezi,hivyo kuomba msaada kwa rafiki yake,mpenzi wake au yoyote isiingizwe kwenye mjadala huu,kujiuza kuko kwa jinsia zote,wapo wanaume kazi yao kujipodoa na kujipitisha mbele ya wanawake wenye hela ili wauze sura,huku ni kujiuza,hata wale kaka poa wanapokaa barabarani kutafuta watu wawape hela in return kwa kuingiliwa,huku ni kujiuza,na wale dada poa nao ni hivyohivyo,so mwanamke anapokuwa na mpenzi wake halafu akawa anahudumiwa nae huyu hajiuzi!
afu ukumbuke hii ni ya 2
nazitaka valentini dei
inamaana umefunga mjadala mapema hivi?
Naona umefanya koknlusheni.
Hhhmm we sinilikwambia unipe kijiwe cha kukuachia zawadi yenyewe hujanipa. . .
ni kweli kabisa mara nyingi watu husema au hutumia neno kujiuza bila sababu za msingi,,Mara nyingi tunasikia na kuona watu wakinyooshewa vidole kua "wanajiuza tu hao" au "anajiuza tu huyo".
Sasa nimejikuta najiuliza Je kujiuza kunaanzia wapi na kuishia wapi? Ni mpaka mtu atilie pamba matata na kusimama barabarani huku akisubiria atakaevutiwa nae atokee? Ni mpaka mtu awe na buzi ambalo linamuweka mjini? Vipi anaeoa/olewa kabisa kwasababu ya pesa na sio mapenzi. . . huyu nae anajiuza?
huwezi muita mtu na mpenzi 'anajiuza' eti kwa kuwa anapewa pesa...
tfsiri sahihi ya wadada wanaojiuza ni machangodoa
na wanajiuza kwa yeyote yule bila kujali ni mpenzi wake au sio....
kama mdada anapenda kupewa pesa unaweza kusema anapenda kuchuna
au kuhongwa...
kuna tofauti ya prostitute na gold digger.......
Mi nafikiri si sahihi kusema mwanamke ambaye yupo kwenye uhusiano wa muda mrefu na mwanaume eti anajiuza hata hata km hampendi kwa dhati,
Asilimia kubwa ya wanawake wa kabila fulani huko kaskazini mwa TZ zamani, walipatikana kwa njia ya kutekwa halafu taarifa rasimi inapelekwa kwa wazazi , na huyo alihesabiwa kuwa ameshaolewa je, huyo naye ahesabiwe anajiuza maana hakumpenda mwanaume lkn amelazimika kuishi naye kwa kuwa mila ziliruhusu hali hiyo!?.
Wanaume walichaguliwa wenzi wao na bado mfumo huo unaendelea ktk baadhi ya makabila pasipo kujali km wanapendana au la, na mwanamke anaweza asiwe na kipato chochote hivyo mwanaume anawajibika kwa kila kitu kwa mkewe, jekuna biashara hapo?.
kuna mabinti waliopewa ujauzito wakaozeswa kwa hao waliowapa, wakati wao walikuwa wanaburudishana 2na hatimaye wanalazimika kuwa mke na mume, je kuna biashara hapo?
Hivyo, si sahihi kuwahukumu wanawake waliokwenye nyumba ndogo kwamba wanafanya biashara. Kwa imani ya dini yangu, mwanaume anatakiwa awajibike kumtunza mwenzi wake, ndo maana baadhi ya wanaume hata km wake zao wanafanya kazi bado huendelea kuwajibika kwa familia.
Tamati; anayejiuza jambo la msingi kwake ni soko(wateja) hivyo hachagui mteja ilimradi ana fedha za kulipia huduma, pia mteja anakuwa na mamlaka dhidi ya huduma inayopewa kwa maana hiyo anaweza kuitumia namna atakavyo ilimradi akidhi haja yake pasipo kumjali mtoani, jambo ambalo kwenye mahusiano hayo hapo halipo.
Smile smile hebu nipe kwanza definition ya kujiuza ndio nijue kama nabisha au lahasilimia 85 ya wanawake wanajiuza au walishawai kujiuza katika maisha yao ,anaebisha aseme
Na huko namuachia nani?
C/O inaweza ikawa poa zaidi.
Lizzy, People do whatever they have to in order to survive. I seriously hope you are not judging these kind of people for what they do- after all
at least they are doing something to support themselves - so much better than the people who steals which they are not really entitled and then run other people down.
Give them a break and respect them for what they do and remember your job is what you do not who you are.
Lizzy, People do whatever they have to in order to survive. I seriously hope you are not judging these kind of people for what they do- after all
at least they are doing something to support themselves - so much better than the people who steals which they are not really entitled and then run other people down.
Give them a break and respect them for what they do and remember your job is what you do not who you are.