Sikujui nikupe nini Mbu,post yako ni nzuri sana,tena sana ngoja nimtafute muhusika naye ajisomee.
Yeah, we all want to do this for our wives/husbands, to re-kindle our love
But, truly, an innocent Tanzanian salary man/woman can afford this luxury?
I doubt, may be, after saving for a life time!!
Cheers!
Hahahahah lol! MR zipo sana hizo! We Baba nanihii lakini huku sikufuja hela? Kile kibanda tutamaliza lini? Hii hela tunayotumia hapa ni sawa na mifuko mingapi ya saruji!?.....Kujirusha mwiko mpaka kibanda kiishe!!!
Mbu aksante kwa Remainder nzuri kama hii. Duh kama unamfanyia hayo umpendae mbona namwonea wivu!
Ngoja na mimi nitafute wa kumshika mkono nimlete aje asome hapa kama alivyofanya chauro.
MR umenichekesha sana wanawake wengine tunajifanyaga tuna uchungu na maendeleo kuliko wanaume na cha ajabu ni kuwa hatuzipigii kelele zile zinazotumbuliwa karibu kila siku Baba Chanja kwenye viti virefu akizungusha rounds za bia, konyagi, value, JDs; rounds za nyama choma na mafuta ya gari maana viti vingine huwa vinafuatwa mpaka nje ya mji!
Mbu aksante
Wewe una mtritigi? kwa kweli mambo kama haya yanaongeza sana mapenzi basi tu hatujagundua, i wish ......
Ehee?!! kumbe wanafaidi sana wenzetu.................................Hamna mtu anayetafuta nyumba ndogo humu jamani? Mkinionea mnijuze. Natanguliza aksante.Mwj1 hapo penye wekundu umesema yote. Huo ni ukweli usiopingika.
Kuna watu wanagharamikia Nyumba ndogo mpaka washkaji tunaona kufuru!...
Swali lako zuri ila nikikujibu ndio nitakuwa najikweza. Kuileta mada hii hadharani ni uthibitisho wa kile ninachokifikiria. Majibu mengine acha tu 'yafunikiwe kombe mwanaharamu apite!'
mkuu wapi hapo?
...asante yanitosha mie, mhusika asijenuna akiisoma hiyo 'nikupe nini Mbu!' LOL...Enjoy!
mkuu wapi hapo?
nikipelekwa kwenye hiyo picha ya mwisho namzalia mtu kabisaaaaaaaaa
Unakuta mtu mzima umelipia mkae siku tatu halafu unaanza pewa lecture kama hizo...mwishoe waulizwa siku tatu zote za nini naomba twende ukaombe wakurudishie hela ya siku mbili turudi nyumbani.halafu haya mambo ya kuchukua hela benki bila kunishirikisha mi sipendi kabisa.
Ehee?!! kumbe wanafaidi sana wenzetu.................................Hamna mtu anayetafuta nyumba ndogo humu jamani? Mkinionea mnijuze. Natanguliza aksante.
Mbu una mafumbo kama mwalimu wa kiswahili!!
Nice thread... Ila mkuu, umetulenga wanaume kwa sana mbn? Nadhan hata wake zetu nao wanapaswa kututoa maeneo kama haya.. Hasa ukizingatia mifuko yetu mara nyingi ipo kimaendeleo zaidi...
Jamani mbona wengine tumeshaanza siku nyingi????????Ukisubiri mpaka hela zijae mifukoni mpaka zimwagike chini raha kama hizo hutaziona kamwe maishani mwako. Kama una kibanda, kausafiri (ka-RAV4), vitoto vipo kwa mama Rwakatare, basi anza kula raha. Mimi naona hivyo
Washukie tuone watakavyo react!..Avatar pole kwa kukukwaza bro,...natamani kusema lililo rohoni lakini acha thread isoge sogee kidogo...soon nitawashukia na wao![/COLOR][/SIZE][/FONT]
Hicho kitanda kinaitwa victoria bed we acha tuTanzania hii bana, Tembea ujionee...
Picha ya juu ni Serengeti Plains....Kirawira, Seronera, Serengeti Serena unapata mandhari kama hiyo.
Picha inayofuatia ni Pwani ya Zanzibar....lakini pia Bagamoyo waweza pata mandhari kama hiyo
Picha ya tatu ni Ngorongoro...kwa mbali (chini) unaona mandhari nzuri ya Crater.
Picha ya Mwisho chini ni kusini mwa Tanzania,....Selous Game reserve...unapata viburudisho vya namna hii;
...ha ha ha!, BB mambo si ndio hayo bana.
Ni haki yako ya msingi kila baada muda kumsisitiza mumeo mkafanye 'semina elekezi' mambo yaliyotekelezeka
na yanayohitaji msukumo mpya kwa zile ahadi mlizopeana kwenye honeymoon.
Kwa wale wenzangu na mie ambao tukishanuniwa ndio 'hakieleweki mpaka anunuliwe khanga,' si vibaya tukajitutumua na kum-surprise mother house na bonge la week end 'Romantic' retreats kama hizi angalau mara moja kwa mwaka jamani...