Kujikwamua kielimu au kibiashara huku ukijitegemea

CCSN

Member
Apr 7, 2019
8
4
Habari, wanajamii?

Kuna wazo moja ninapenda nililete kwenu nikitumai kubadilishana mawazo nanyi.

Kuna huu mfumo, uliojiimarisha hasa katika nchi za magharibi, wa kujisomesha kwa kufanya kazi au wa kuwekeza katika biashara, bila kuitegemea biashara hiyo kiuchumi. Jambo hili linawawezesha - hasa vijana - kujitegemea kiuchumi kwa kufanya kazi/vibarua huku wakisoma chuo, au kujijaribu katika biashara huku wakiwa na ajira zao zenye kipato cha uhakika.

Kwa hakika, mazingira tunayoishi hufanya watu kutekeleza jambo hili kwa namna tofauti tofauti. Wengine hukaa nyumbani kwa wazazi/ndugu kwanza kutokana na ukaribu na chuo pamoja na mazingira ya kazi ili kuweza kumudu gharama za maisha kabla ya kusonga na hatua nyingine za maisha.

Wengine hukodi sehemu ya kukaa pamoja na rafiki au ndugu ili kumudu gharama za maisha. Ni hakina, ukilinganisha gharama za maisha kwa mwezi (chakula, mavazi, kodi ya nyumba, vifaa vya nyumbani, ada, bima ya afya, mengineyo) na kipato cha vibarua (k.v. tempo shuleni, shughuli za ufasi maofisini, kazi za hotelini/mgahawani) kupata uwiano ni ngumu.

Lisha ya changamoto nyingi za upatikanaji ajira/vibarua, pesa za kuwekeza katika biashara au vipato vidogo katika biashara, watu wanapambana kutatua changamoto.

Vipi uzoefu wenu wa kazi ya kujikimu maisha huku mkijiendeleza kiuchumi au kielimu? Mumemudu vipi changamoto zinazojitokeza?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom