Mahunguchila
Member
- Jun 11, 2012
- 74
- 34
Kwa sie watu wa bara wengi wetu hatuna huu utamaduni wa kujifukiza udi, ila wenzetu wa pwani naona wanao huu utamaduni. Hivi kazi ya udi ni nini hasa na je wake kwa waume hujifukiza hii kitu au wanawake tu?
Mimi kiukweli harufu ya udi naichukia sana kama vile navyochukia moshi wa sigara. Majuzi nimepanda daladala nikakaa na mama mmoja kapiga baibui lake ananukia (naogopa kusema ananuka) udi balaa! Kiukweli niliacha seat akaja kukaa mtu mwingine. Hivi wenzangu/wana JF kuna mmoja kati yenu ambae hapendi hii kitu kama mimi au ni ushamba wangu tu? Kweli nakereka sana na hii harufu! Leo pia nimepishana na mbaba mtu mzima na kanzu yake nae kajifukiza hiyo kitu, nikashangaa kumbe na wanaume nao wanatumia? Mwenye kufahamu anaijuze tafadhali ila dah, hii kitu inanuka/kia vibaya to be honest!
Samahani kama kuna watu ntakuwa nimewakera.