Kujibizana na wakwe...kumewahi kukutokea ?

huyo mama amemgeuza mwanae mtaji
 
Reactions: SG8
Nisome vizuri mpendwa, ukijibu calmly itamfanya akuogope na akae mbali na wewe. Confrontations ni mbaya sana. Kwani ungemgeukia mkeo na kumuuliza unataka kwenda na mamako akakutunze vizuri zaidi ya ninavyokutunza? Dawa yake umsikie atakavyojibu mbele ya mamake.

Mjinga hapo ni mkeo, angemkemea mama yake kuwa hujui hali yetu na hayakuhusu haya yasingetokea. Na isitoshe mkeo ni mgonjwa sawa, lakini huhitaji kuacha hela ya matumizi kwa mama mkwe wala mamako kama yupo. Mkeo haumwi akili, anahitaji kupumzika. Kutoka alipolala hashindwi kusema mkanunue mchicha na mifupa tuchemshe supu. Binafsi hakuna anaeweza kuhoji matumizi ya fedha nyumbani kwangu unless anachangia budget, na sihitaji kujieleza. Nikiachiwa elfu kumi, mama atasikia namuagiza dada akalete nyama nusu kilo, matunda ya buku etc. Hapo kuna mjadala tena?


Ndo maana naona umuhimu wa kulindana na kujenga himaya yenu isiyoingiliwa na yeyote. Huwezi kuishi kwa std ya nyumbani kwao mwenza wako! Na mwenza wako akijua hili maisha yanasonga.
 

Usikae kimya.Si kakuomba ruhusa akamuuguze mwanaye mwenyewe?
Mwambie " sawa mama mkwe, haina shida hata kidogo.Basi mcukue tu maana naona utakua umenisaidia kwa kweli.Asante sana kwa msaada."
Kama alikua anatafuta ugomvi na wewe, utakuwa umemmaliza kisayansi.
 
me nawashauri kua wavumilivu na kuishi kulingana na tabia ya huyo mkweo kwa maana wengine unaweza kubishana nao ukaumiza kichwa chako
 

Umenena vema happiness win
 
Last edited by a moderator:
Of course nakuelewa unachojaribu kusema hapa....Hii ni story imemtokea rafiki yangu. For sure binafsi ilinikera kwa sana kwa sababu jamaa akiongea na mkewe wanaelewana vizuri...akienda kazini jioni anakuja kukuta mambo yale yale....Ni kweli kabisa anayepaswa kulaumiwa hapa ni Mke, anayeruhusu Mzazi wake aendeshe nyumba yake...Pointi yangu hapa ni kwamba tusifanye generalization kwamba Wazazi wetu wote wako perfect...kwa utafiti wangu mdogo tu (sio lazima uwe wa kweli) wazazi wa kike (hasa ambao ni single) ni tatizo sana. Jambo la muhimu ni ku keep distance, muwe mnakutana kwenye matatizo tu basi (where necessary lakini)
 
Imagine familia zetu za Kiafrika, Mama yako Mzazi pia amekuja kuuguza mgonjwa aliyejifungua halafu Mama Mkwe anaomba akakusaidie kuuguza utakubali na kumwambia mama yako arudi kijijini kwake alikotoka au utasema na yeye aambatane na mgonjwa?
 
Nakubaliana na wewe. Kwanza mie sioni sababu ya mama mzazi.kuja kuhudumia.mzazi. Kama inalazimika aje basi 2 weeks ndo maximum. Kwani anashindwa kuhudumia mkewe for the first week? Kuna housegal na utaratibu wenu wa maisha, mzazi anashindwa kuambia dada chemsha nyama unipe supu?

na kama hali inajirudia, dawa ya huyo mama unamuambia aondoke na mwanae, na humpi fedha. Kama mwanamke ana akili hataondoka na atajua mwenzie kakasirika. Ukikasirika huongei maneno mengi, saa zingine mama mkwe unamkata jicho tu anajua kavuka mstari. Mie hata unisimulie.mama mkwe kanisema, simuulizi ng'ooo, nikikutana nae namchekea hadi ajishuku mwenyewe kama najua ama sijui.
 
Reactions: SG8
Maisha ya kisasa kuishi na watu ni ngumu sana,,kila kitu lawama, na ki africa kuishi familia moja as baba , mama, watoto wenyewe ni ngumu sana,, sasa hapo mama mzaz wa mume yupo, na wa mke nae yupo si kunaweza gombanisha wazaz,,

Mungu anisimamie wife akizaa nikae nae home tu na msaidiz wa kaz, as kwetu au kwao ataenda 2 weeks za mwanzon tu mimba ya kwanza.. Akapate direction ya anatakiwa aweje after that anarud geto kwa kamanda maisha yanasonga.. Kuishi na ndugu ni kazi sana especially wa kike
 
sijawahi kujibizana nao ila kama mara 2 hivi nimewahi kuwakalisha kitako na kuwaambia yangu ya moyoni......wakaniomba msamaha, tunaendelea kama kawaida
 
mimi huwa nakaa nao mbali sana ili kuepusha migongano km hiyo, nimeweka utaratibu wa kuwa nawapigia simu mara 1 tu kwa mwezi kuonana ndo usiseme japokuwa wote tupo mjini hapa.
 

yote yanawezekana kama haukai nao nyumba moja ila kukaa nao nyumba moja ipo siku mtajibizana haswa maana wazazi wengine wanadandia mambo hayawahusu. Wanataka muishi kama yeye alivyoishi na mumewe, inabidi kwanza atambue hiyo inakua ni ndoa nyingine kabisa na ina sheria zake.
 

Nakubaliana nawe, japo nina maswali ya nyongeza. Tunafanyaje pale ambapo mwenye mzazi naye hasemi kitu, ukumbuke naye ana mtazamo kuwa mzazi wake hakosei.

Sijaelewa kipande cha mwisho, mzazi wangu namjibuje wakati hapa nina-deal na mzazi wa mwenzangu?
 
Reactions: SG8


Hapana. Ukikaa nao nyumba moja ni rahisi sana kuwaepuka maana utakuwa umewasoma na kujua tabia zao, hii itakusaidia kujipangia misimamo yako ya uhakika na itakufanya ujiamini zaidi na itakufanya usijibizane nao hata waseme nini maana penye ujinga utadharau na utasimama kwenye ukweli bila kelele nao wataishia kuguna tu maana una usimamo na huna majibizano nao!
 
Imagine familia zetu za Kiafrika, Mama yako Mzazi pia amekuja kuuguza mgonjwa aliyejifungua halafu Mama Mkwe anaomba akakusaidie kuuguza utakubali na kumwambia mama yako arudi kijijini kwake alikotoka au utasema na yeye aambatane na mgonjwa?
Usipoangalia vizuri utageuka mwamuzi wa "sakata" la mama mkwe na mama mzazi.
Always avoid hawa wamama wasikutanie kwako. Utaambulia laana.
 
Reactions: SG8
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…