Binadamu na mitazamo yao, sisi na maisha yetu

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Unaamua kuposti picha zako nzuri, wanasema anajishaua sana anapenda sana kujionyesha kwa watu. Unakaa kimya, hupost chochote kuhusu wewe wanasema hana lolote ni wa kawaida sana tunabidi kuona matokeo na sio maneno.

Una mpenzi wako, humpost kwenye mitandao ya kijamii wanasema ni malaya hana mtu mmoja na ndio maana hawezi kupost chochote kuhusu mpenzi wake. Basi unabadilika unamposti kwenye mitandao ya kijamii wanakuja wanasema kwa mpenzi gani, hawawezi kufika popote wataachana tu.

Unaenda kuabudu lakini kimya kimya hupost chochote kile wanasema mtu mwenyewe hamjui Mungu hajui hata mlango wa Kanisa/Msikiti upoje. Basi sawa, unaamua kwenda kuabudu unapost picha wanasema ibada gani ile kwenda tu Kanisani/Msikitini ndio atangaze vile kwa watu.

Haya yote kheri, basi unawasaidia wenye uhitaji unawatembelea watoto yatima unapost picha kuwavutia na kuwashawishi wengine wafanye hivyo kwa wakati wao wanasema ana maisha ya kujionesha sana hakuna msaada kama ule. Basi sawa unabadilika, unatoa misaada kimya kimya hupost chochote wanaendelea kusema Hana moyo wa ukarimu hajui hata kuwasaidia watu.

Unanunua nguo, simu vitu vizuri vinavyokuvutia wanasema anashindana sana kimaisha na wengine. Hajitambui, umri wake sio wa kufanya vitu kama vile basi sawa hununui vitu vya bei ghali unakuwa na maisha ya kawaida wanasema hajijali maisha yake yapo yapo tu hajipendi hata thumni.

Basi sawa hivi unajua watu wanaweza kukuomba msaada na ukawa huna uwezo wa kuwasaidia, lakini usipowasaidia tu husema ni mchoyo, ana roho mbaya sana hana utu kabisa. Lakini hao hao wakikuomba msaada halafu ukawasaidia haraka na kuwajali wanaweza kusema anajikuta ana moyo sana, tena wanaweza kudhani kama huna wa muda maana hivi kwani unapatikana kila wanapokuhitaji kwenye shida zao.

Unajua kwanini imekupasa kusoma hii;
Kwa sababu nilikuwa nataka nikukumbushe jambo moja tu kuwa kamwe binadamu hawaachi kusema. Huwezi kuwazuia wanadamu kuongea, huwezi kumfurahisha au kumvutia kila mtu bila kujali una moyo mzuri kiasi gani, u mkarimu kiasi gani, tarajia mawazo mabaya na yenye chuki mara Kwa mara kutoka kwa wanadamu. Binadamu watakuchukia lakini wewe mwenyewe hupaswi kukata tamaa sababu ya chuki zao.

Binadamu wataendelea kukusema tu, ukiwa bora watakusema, ukiwa dhaifu watakusema hivyo chaguo ni lako usemwe kwa ubora wako au kwa udhaifu wako.
Lakini usisahau kuishi maisha ambayo yatakupendeza wewe pamoja na Muumba wako.

Ahsante sana kwa kunisikiliza naitwa Amani Dimile

stress-african-man-dark-room-low-key-style_73622-2079_1.jpg

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Una mpenzi wako, humpost kwenye mitandao ya kijamii wanasema ni malaya hana mtu mmoja na ndio maana hawezi kupost chochote kuhusu mpenzi wake. Basi unabadilika unamposti kwenye mitandao ya kijamii wanakuja wanasema kwa mpenzi gani, hawawezi kufika popote wataachana tu.
Tupia picha yake basi
 
Ahsante sana kwa kunisikiliza naitwa Amani Dimile View attachment 2700714

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
kikubwa ni kufata mfano wa nge ni yeye yule habadiliki yeye ni kung'ata tu. Hata umwokoe kweny maji hajali wema wako.Nampenda sana huyu mdudu na siku izi nishaacha kumuua akining'ata mana namwelewa sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom