Kujiandikisha ni 'tisa', 'kumi' yaja!

Kujiandikisha ni 'tisa', 'kumi' yaja!

faida ya mufumo huu
1. huwezi kujiandikisha zaidi ya Mara moja yaani utakamatwa kirahisi sana
2. utaweza kubadilisha kituo mfano kata/ jumbo
kifupi nirahisi kuedit sasa hii inaweza kuwa na faida na hasara ila nilichojifunza kwenye hizi machine inafaida nyingi kuliko hasara...

Si kweli kwamba huwezi kujiandikisha mara mbili, hili linawezekana tena kirahisi kabisa.

Kama kweli umezifuatilia hizi mashine na mifumo yake, kuna ile sehemu ya kujaza fomu namba 1. Pale kama huna mikono, maana yake huwezi kuweka alama za vidole. Sasa kama hila itatumika, kituo cha kwanza mtu anaweza kuwekewa hana vidole na akapata kitambulisho. Lakini anaweza kwenda kituo cha pili na ajaandikiwa kuwa ana mikono na alama za vidole zikachukuliwa, pia hapa atapewa kitambulisho.
 
image.jpg

Mashine hazina uwezo wa kutambua sura, ila zina uwezo wa kutambua alama za vidole. Hivyo unaweza kujiandikisha mara mbili kama Waandikishaji watashorikiana na wewe kufanya kosa hilo.
 
Hutaweza kupiga kura ya mbunge kwa sababu karatasi za mbunge hazitakuwa kila mahali. Pia hizo ni mashine za uandikishaji tu. Siku ya kupiga kura kutakuwa na mashine itakayotambua vidole na kama umejiandikisha.

Kwa maana hiyo unaweza kupiga kura tofauti na sehemu uliojiandikishia?
 
Mashine zinatambua vidole na siku hiyo ukiweka vidole vikitambuliwa na mashine na picha yako inatokea na taarifa zote ndio unapewa karatasi ya kupiga kura.


View attachment 262711

Mashine hazina uwezo wa kutambua sura, ila zina uwezo wa kutambua alama za vidole. Hivyo unaweza kujiandikisha mara mbili kama Waandikishaji watashorikiana na wewe kufanya kosa hilo.
 
tume ya kina jaji lubuva imeshindwa kazi. ilipaswa kuondoka ofisini mara moja
 
Back
Top Bottom