Kujiajiri: lipwa kwa kupost na ku manage accounts za social media

ForeverMore

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
813
1,928
Naona kuna vijana wengi wapo vizuri kwenye kuandika na kupost vitu humu karibia kila siku. Kwanini tusitumie uwezo huo kujiingizia kipato? Bei na maamuzi ni yako, unaweza fanya ku charge kwa siku, wiki, mwenzi au kwa idadi ya posts utakazo post kwenye social media za watu kama makampuni au biashara mbalimbali.

Ukiingia kwenye social media, utakutana na accounts nyingi ambazo mara ya mwisho ku post ni miezi. Ni kwamba mara nyingi wahusika hawana muda.

Raha ya hii kitu, ni kwamba unaweza ku manage account za kampuni nyingi kwa wakati mmoja. Utatakiwa ku post vitu vinavyo husu kampuni husika kwenye social media zao siyo ili mradi tu.

Kama nilivyosema, bei na idadi ya post ni maamuzi yako. Ningeweza kuandika zaidi sema jamaa hawa (Jf Moderators) hawataki links humu, mara nyingi wana futa post za namna hiyo. Haswa link za mitandao ya bongo. Kwa hiyo nitajibu nitavyoweza kwenye comments ila kwa maelezo zaidi una weza ni PM for details na hata kuongea kwa whatsapp call.

Watu wanao jua graphic designs yani kwao ndo raha mara dufu.

Vijana tuanze kuangalia njia mbadala za kujiajiri. Tunahitaji kuwa wajanja kwenye kutafuta pesa. Mfano wenzetu wanavyofanya, hapa bongo tunaweza pia na sehemu ya kuwezesha ipo.
Social Media.png
 
Graphic design kama hujui upati deal au ?
Unaweza pata, yaani inaongeza uwezekano wa kuata dili, maana ukiangalia platform kama ya instagram ni picha tu. Pia siyo lazima ufanye mwenyewe, unaweza kuangana na mtu mwingine anayejua graphic na kufanya wote.

Au unamlipa mtu afanye graphics. Kwa mfano. wewe unachukua dili la mwezi la laki 2 au tatu, alafu unampa mtu kama huyu (https://ajiras.com/gigs/banner-ads/i-will-design-banner-ads-for-your-social-media-posts/) akufanyie graphics. Unavuka tayari.
 
Izo deal tunazipaje mkuu sasa ?

Kitu cha kwanza, unahitaji sehemu ya wahitaji kukupata na watakayoweza kukulipa. Mfano: wenzetu huko duniani, wanatumia mitandao kama www.fiverr.com. (fungua hiyo search Manage Social Media) utaona wanavyofanya. Tatizo ni kwamba sisi hatuwezi kupokea hela kutoka huko. Maswala ya paypal hayo.

Kwahiyo, hapa bongo unaweza tumia mtandao wa www.ajiras.com maana utaweza pokea hela yako kwa Tigopesa, mpesa, airtel money na hata bank transfer. Kwahiyo, ukiangalia wenzetu service wanazotoa kwenye www.fiverr.com, unaweza na wewe ukagelezea na kuweka kwenye www.ajiras.com

Kinachobaki, ni kujitangaza tu kwenye ma group ya facebook, huku jamii forums na sehemu mbalimbali. Ajiras pia wanasaidia kutangaza.

Pia haulipii chochote kama hujapata kazi. Pindi umepokea order na kazi kukamilika, wao watachukua 10%. Wakati 90% inakuja kwako. Kwahiyo kwenye elfu10, wao watachukua elfu1 wakati elfu 9 inabaki kwako.

Angalia hii post (https://www.jamiiforums.com/threads...ao-jiajiri-badala-ya-kutengeza-ajira.1618256/) haswa kwenye kipengele cha mikopo na misaada kifedha.
 
Modereta futeni huu uzi UCHWARA. Maana huko tunakoelekea ni : tuma ile pesa kwenye number hii
Yaani unaanza ponda kabla hata ya kujua mtandao unafanyaje kazi. Mtanzania kwanini usiulize? Kwanini usiseme wasiwasi wako ujibiwe? Nyie ndo mnao kuja kufa masikini. Umeona na kuelewa mtandao kama wa www.fiverr.com wa Israeli na dunia nzima unavyofanya kazi? Ajiras unafanya kazi hivyo hivyo. Fungua mtandao wa ajiras alafu scroll chini kabisa angalia kampuni na mfumo wa malipo wanaotumia.

Hiyo ni kampuni imekuwa registered, fungua about us uangalie jina la kampuni inayo endesha hiyo website (One Two One Consultant Ltd) alafu cheki Brela kama imekuwa registered. Wao wana shikilia hela mpaka mteja atakapo ridhika na kazi. Bila hivyo hela yake inarudishwa. Na pia wewe ukifanya kazi yako fresh, mteja hawezi kukuzungusha malipo maana alishalipa anavyo toa order.

Angalia pia mfumo wamalipo wanaotumia ambao ni Direct Pay Online (www.directpay.online). Ni mfumo mkubwa zaidi Africa. Kama umeshasikia mfumo wa Pesapal unaotumika na site kama Jumia, ni chamtoto. Direct Pay Online upo nchi nyingi za africa na juzi kati wameununua mfumo wa PayFast wa South Africa. Ingia site yao uone mashirika mangapi yanatumia mfumo wao ikiwemo hoteli za kitalii na mashirika ya ndege. Wemedhibitishwa na Visa, Mastercard, American Express na kadharika. Alafu wewe unakuja na kuropoka tu makande uliyokula Juzi, jana na leo. Cha ajabu zaidi eti na wewe ni Senior Member. Kweli?
All-Cards-and-Mobile-Money-257×95.jpg

Yaani hapo hakuna uswahili wa kusema umemlipa mtu akatokomea na hela. Au umefanya kazi alafu mtu akakimbia bila kukulipa.

Ndugu kama hujui kitu au hujaelewa uliza. Siyo kuropoka tu, yaani ilimradi tu na wewe umechangia. Daa bongo tunashida nyingi sana...
 
Kama wewe umetengeneza iyo platform iko vizuri kwenye flexibility kwa level za Tz, ila mkuu kitu kimoja ungeangalia reserch ya East Africa wanapendelea nini Online ingekusaidia kupata wazo bora zaidi ila kwa hii mzee ngumu kwa watanzania.

Nina wazo moja tatizo programming sijui, resource sina, pesa kisanga wazo langu nimechakata kwenye trend ya East Africa wanapenda nini na nimeangalia Tz wanapenda nini.
 
Mkuu kwa huku bongo malipo ni shi ngapi kwa uzoefu wako ni kiasi gani
Kitu cha kwanza, unahitaji sehemu ya wahitaji kukupata na watakayoweza kukulipa. Mfano: wenzetu huko duniani, wanatumia mitandao kama www.fiverr.com. (fungua hiyo search Manage Social Media) utaona wanavyofanya. Tatizo ni kwamba sisi hatuwezi kupokea hela kutoka huko. Maswala ya paypal hayo.
Kwahiyo, hapa bongo unaweza tumia mtandao wa www.ajiras.com maana utaweza pokea hela yako kwa Tigopesa, mpesa, airtel money na hata bank transfer. Kwahiyo, ukiangalia wenzetu service wanazotoa kwenye www.fiverr.com, unaweza na wewe ukagelezea na kuweka kwenye www.ajiras.com
Kinachobaki, ni kujitangaza tu kwenye ma group ya facebook, huku jamii forums na sehemu mbalimbali. Ajiras pia wanasaidia kutangaza.
Pia haulipii chochote kama hujapata kazi. Pindi umepokea order na kazi kukamilika, wao watachukua 10%. Wakati 90% inakuja kwako. Kwahiyo kwenye elfu10, wao watachukua elfu1 wakati elfu 9 inabaki kwako.
Angalia hii post (https://www.jamiiforums.com/threads...ao-jiajiri-badala-ya-kutengeza-ajira.1618256/) haswa kwenye kipengele cha mikopo na misaada kifedha.
 
Kama wewe umetengeneza iyo platform iko vizuri kwenye flexibility kwa level za Tz, ila mkuu kitu kimoja ungeangalia reserch ya East Africa wanapendelea nini Online ingekusaidia kupata wazo bora zaidi ila kwa hii mzee ngumu kwa watanzania.

Nina wazo moja tatizo programming sijui, resource sina, pesa kisanga wazo langu nimechakata kwenye trend ya East Africa wanapenda nini na nimeangalia Tz wanapenda nini.
Uza wazo lako kama lipata soko au tafuta watu unaowahitaji kwenye wazo lako mshirikiane.
 
Nimependa iko poa sana na ni idea nzuri sanaa
Ndiyo, fungua account ya mtu anaitwa Sunday, ndiyo mimi, nimepiga zaidi ya laki 6. Wateja wanu walionunua ni kutoka Marekani na Turkey. Unaweza ona review zao kwenye kazi walizo nunua.

Watanzania ni wazito mno, yaani ni kama kipofu mpaka apapase mikono au umshike mkono umuongoze mpaka pale kabisa. Ni hichi kinatufanya tubaki kuwa masikini.

Lazima tuwe wepesi kuangalia, kuchambua na kuchukua hatua. Fursa ikipita siku tu, kiuhalisia, ule mzuka unapotea, unaanza kupata uwoga na kuhukulia poa. Matokeo yake, wiki, mwezi, mwaka unakata.
 
Nimependa iko poa sana na ni idea nzuri sanaa
Shukrani, tukiweza itumia vizuri, nadhani inaweza kutusogeza kidogo. Haswa ikifika kwenye atua inayotaka kufika ya kutoa mikopo na misaada kwa vijana wanao jishughulisha kupitia mtandao huu.
 
Uza wazo lako kama lipata soko au tafuta watu unaowahitaji kwenye wazo lako mshirikiane.
Hili wazo siyo kwamba tumekurupuka, ni research ya muda mrefu na imechufuka karibia 2 years mpaka kuanza kazi. Tatizo watanzania hatukosi visingizio, yaani ukiwapa wanachotaka, watataka kingine. Tupo wepesi kulalamika ila wavivu ku take action.

Ki ukweli, hakuna watu wavivu probably Afrika nzima kama sisi watanzania. Mtu kutwa nzima yupo nyumbani hana kazi (ajira), ana chat huku siku nzima, lakini kuchumua 30 minutes kujiunga Ajiras na kupost ali ajiajiri awezi. Ni visingizio tu, yaani ni leo kesho, kesho kutwa. Ana ahirisha kila siku.

All the best kwenye wazo lako, ukifanikisha, utagundua na maanisha nini kuhusu watanzania na visingizio.
 
Mkuu kwa huku bongo malipo ni shi ngapi kwa uzoefu wako ni kiasi gani
Inaweza anza elfu 50 mpaka laki 5. Ilivyo unahitaji kupata reviews nzuri ili upandishe bei. Unaanza small, ili upate wateja haraka. Kila mteja unayemfanya kazi, anaandika reviews, baada ya muda, unaweza pandisha bei maana kuna watu wengi ambao ishu siyo bei ni uwakika wa quality.

Pia kila unapopata reviews nzuri, unapanda level, utaanza na New Seller, then Level 1 seller, level 2 na mwisho Top Seller. Hiyo inaonyesha una experience kiasi kagi na watu wanazi kubali kazi zako kiasi gani.

Mwelekeo wa ajiras, ni kuweza kuungana na NGOs na taasisi zingine za fedha, ili kuweza kuwapa watu mitaji wale waliofika Top Seller, maana hao wana asilimia kubwa ya kuweza kutumia hizo fedha kutoka kimaaisha kuliko mtu mwenye business plan ambayo hajaanza kuitumia. Unaweza soma zaidi kwenye hii post https://www.jamiiforums.com/threads...ala-ya-kutengeza-ajira.1618256/#post-32521005
 
Back
Top Bottom