Kujamiiana wakati wa ujauzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujamiiana wakati wa ujauzito

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 8, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watu wengi wamekuwa wakijiuliza je, baada ya kupata mimba bado mtu anaweza kuendelea kufanya mapenzi? Ni salama? Halafu huwa inakuwaje? Wataalamu wanasema mtu anaweza kuendelea kula uroda pamoja na kuwa ana mimba.
  Mapenzi, kujamiiana, na kuwa karibu zaidi kimoyo yote ni mambo muhimu kwa furaha ya ujauzito.Baadhi ya wanawake wanajisikia vizuri kujamiiana wakiwa wajawazito. Baada ya wiki ya 12, wakati ambapo hali ya kichefuchefu na uchovu kwa kawaida hupungua, hisia nzuri hujitokeza. Damu hutiririka kwa wingi maeneo ya kiunoni, na kiwango cha homoni za kujisikia vizuri huongezeka hadi karibu na mwisho wa ujauzito.

  Hii yote inachangia kukuza hamu ya kujamiiana. Ni salama kujamiiana? Kama ujauzito wako ni mzuri kiafya na unajisikia vizuri, hakika hakuna sababu ya kutokujamiiana. Baadhi ya wanawake madhara ya ujauzito yanawafanya wasijisikie kufanya mapenzi. Hii inaweza kuwapata hata wanaume. Kichefuchefu na uchovu vinaweza kukufanya usiwe na mawazo ya kujamiiana.

  Baadhi ya wanaume hukataa kufanya mapenzi kwa kuogopa kumdhuru mtoto. Usikilize mwili wako. Usijilazimishe kufanya kitu ambacho hakikupi raha. Ni muhimu pia kukumbuka kwamba tumbo kubwa linaweza kuwa kipingamizi kati yenu. Hapa inabidi kubadilisha mtindo / miondoko. Wapenzi wanaweza kuwa karibu bila kujamiiana. Kupigana mabusu na kukumbatiana kunawafanya kujisikia kama vile mmeshafanya mapenzi. Kitu cha muhimu ni kuelewa mwenzako anajisikiaje. Zungumza na sikiliza mahitaji ya mwenzio.
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Lazima ujamiane na mwenzio mjamzito maana unasaidia kupanua njia ya mtoto kutoka
   
 3. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Asante sana Jpinduzi kwa kutukumbusha!
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kujamiiana wakati wa ujauzito kuna madhara kwa mtoto aliye tumboni................ najua wapenda ngono watanibishia, lakini huo ndio ukweli wenyewe.
  Ikumbukwe kwamba mtoto aliye tumboni hutumia pumzi ya mama, hivyo basi wakati tendo la ndoa linapofanyika na mama anapotaka kufika kileleni kunakuwa namabadiiko makubwa ya pumzi na hiyo humsababisha mtoto kuhangaika kule tumboni. inaelezwa kwamba wakati mwingine husababisha kifo cha mtoti tumboni...............

  Wanawake wanalazimika kufanya tendo hilo wakati wa ujauzito kwa sababu ya kulinda ndoa zao, wanawajua waume zao wakikosa tendo kwa muda mrefu, watadesa nje......................
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hicho ni kisa asili tu, hakina ukweli wowote................. Ondoa tamaa yako hapa...........
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kwa nini msiwe mnafanya oral sex na kujisugulia kwenye mapaja???
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kama hujajaribu hii kitu; then your integrity as baba is highly questionable
   
 8. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Na wakunga wanasisitiza umkune mke wako mpaka abakishe wiki 2 kujifungua njia inakuwa wazi
   
 9. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  eeehh!! kumbe....!! acha nimwambie anipumzishe!!!!
   
 10. m

  mareche JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  je wewe utaridhika wakati ulishazoea kupata dozi ngumu sina hakika
   
 11. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  puliza puliza usiogope puliza mwenye mimba puliza. Nalog off
   
 12. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  itabdi wewe ndo uianzishe ikifanikiwa urudi na majibu ok!
   
 13. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #13
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  unaweza ukajikuta mapumziko yanakuwa ya muda mrefu na kupelekea kupoteza mpenzi/mume kabisa. we endelea kumpa tu la muhimu hapo ni kwamba missionary style should be foregone for sometime
   
 14. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  mh..ebu nkaangalie diary yangu kama tulikuwa tukiduh!
   
 15. M

  MyTz JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  shukran mkuu kwa darasa...
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mtambuzi I beg to differ na kwa hisani yako naomba uruhusu mods waipeleke kule kwa daktari tukaichambue hii kitu
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ruksa, waambie waipeleke tu...................
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,076
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mchambuzi hapo kwenye nyekundu si kweli kwa mimba zote. Kama daktari ambaye anafuatilia mimba ya mjamzito hajaona dalili zote za hatari kwenye ujauzito basi hata siku moja hatatoa ushauri wa kuacha kujamiiana kwa kuwa ni hatari kwa mama mjazito au kiumbe mtarajiwa. Tena mara nyingi kama ujauzito hauna matatizo hushauri kujamiina hata mpaka dakika za mwisho mwisho maana huongeza njia na kusaidia mama mjamzito kujifungua kirahisi hasa kama ni yule anayetegemewa kujifungua kwa njia ya kawaida na siyo kwa visu, ila kama kuna mushkeli wowote katika ujauzito ambao unaweza kuhatarisha uhai wa mama na mtoto basi daktari huweza kuzuia tendo hilo kufanyika kabisa kwa kipindi chote cha ujauzito.
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Labda nilichokosea ni kutoweka neno baadhi, lakini nilikuwa napinga swala la kwamba hakuna madhara kabisa............... kwa kuwa hakuna takwimu sahiihi zinazothibitisha vifo vya aina hiyo, labda ndio sababu wengi wanaona ni jambo lisilo na madhara, lakini yapo madhara kama nilivyoeleza. Hilo la kupanua njia, siamini kama daktari anaweza kutoa ushauri wa namna hiyo, kwamba ili kupanua njia ya uzazi ni lazima kujamiiana.......... Mimi nadhani Daktari analazimika kukubali baada yakuulizwa swali hilo na wanandoa kutokana na tamaa zetu za ngono.......... wewe unafikiri angejibu nini? Daktari amezaliwa na kulelewa katika jamii hii hii inayoamini kwamba jambo hilo halina madhara, kwa kuwa ameona wanandoa wako salama kushiriki, hana budi kukubali, labada tu pale ambapo ataona vinginevyo..........................
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,076
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Mkuu hapo kwenye blue, kwenye nyekundu Dr yeyote yule mwenye kufuata professional ethics za udaktari wake hatapindisha maneno kama anaona kuruhusu kujamiiana kunaweza kuhatarisha usalama kwa mjamzito na kiumbe mtarajiwa, kama daktari anawaruhusu ili kuwafurahisha tu na baadaye kukawa na tatizo kubwa ambalo chanzo chake kinaweza kuthibitishwa kwamba ni kujamiiana na ambapo dr alitakiwa asiwaruhusu basi Dr anaweza kabisa kufunguliwa mashtaka na pia hata kupoteza haki yake ya kufanya kazi kama daktari.
   
Loading...