Kuitwa kwenye Usaili NHIF

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Wadau kwa wale walioomba nafasi mbalimbali NHIF mwaka jana November hatimae hilo lundo linaloitwa orodha fupi limetangazwa. Tembelea tovuti ya NHIF ujipatie kuona. Natanguliza shukrani!

LINK: CALL FOR INTERVIEW
Mnamo mwezi Nov 2015 NHIF ilitoa tangazo la nafasi za kazi. Kila nafasi walihitaji watu 2 au 3 au 4 Sasa watu wameitwa kwa interview lakini unakuta nafasi zipo Tatu (3) na wameita watu 1700! Hii ina maana gani? katika taratibu za ajira nafasi moja inapaswa kugombewa na watu angalau 3 au hata wakiongezeka kidogo si mbaya.

Sasa kwa staili yenu nafasi moja inagombewa na watu zaidi ya 550! Kwanini kuwasumbua watu? Vijana wengine wako mikoani huko mbali hata nauli hawana wasafiri mpaka Dar (manake interview inafanyika DUCE), lakini nafasi za kshinda ni ndogo sana. Candidates wauri wapo wengi tu sio lazimauweke wigo mpana namna hiyo katika kutafuta watu wazuri.

Tafadhali waoneeni huruma vijana wetu kwa kutokuwapa matumaini yasiyotimilika!Tangazo la kazi pia linaonekana hapa 46 Jobs at National Health Insurance Fund (NHIF) 4 NOV 2015 | Jobs in Tanzania
Tangazo la kuitwa kwenye interview hili hapa kama linavyoonekana kwenye website ya NHIF hii ni kwa nafasi ya "membership officer".
http://www.nhif.or.tz/index.php/careers1/39-membership-officers/file
 
Mkuu fanya msaada wa kuyacopy na kuyapaste hapa ili kwa wenye cmu nao waweze kuyaona.
 
Hellow wanajamii....mimi ni mmoja Wa walioitwa kwenye written hii ya NHIF je kuna yeyote anayeweza kushare nasi inakuwa kwenye format gani( sample question hasa)
 
Hellow wanajamii....mimi ni mmoja Wa walioitwa kwenye written hii ya NHIF je kuna yeyote anayeweza kushare nasi inakuwa kwenye format gani( sample question hasa)
Ngoja waje wadau watupe maujanja mana hawa NHIF hata mim sijawai kupiga interview yao
 
Hizo clue dondosha hapa kwa waliowahi ku-attempt written interview ya NHIF before sio mbaya ukisaidia maswali yapo kwenye trend ipi ni general questions ama ni questions related to NHIF, msikabe basi wenye awareness.
 
Watahiniwa wa usaili zaidi ya 4000 wanatarajiwa kufurika DUCE katika mchuano wa kuwania nafasi za kazi zipatazo 46 za kada mbalimbali zilizotangazwa katika shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF). Kati ya kada zilizovunja rekodi ya watainiwa wengi kulingana na idadi ya nafasi ni pamoja na kada ya Copliance Officer ambapo nafasi 9 zinatarajiwa kuwaniwa na watainiwa wapatao 3088, ingine ni kada ya membership officer ambapo nafasi 3 zinatarajiwa kuwaniwa na watainiwa wapatao 1783. Kada zinazohusika ni hizi zifuatazo;

1. Assistant Accoutant Nafasi 8 Watainiwa 1776
2. Internal auditor Nafasi 2 Watainiwa 329
3. Claim Officer Nafasi 2 Watainiwa 600
4. Compliance and Field Officer Nafasi 9 watainiwa 3088
5. Driver Nafasi 12 watainiwa 626
6. Membership Officer Nafasi 3 watainiwa 1783
7. Quality Assurance Officer nafasi 7 watainiwa zaidi ya 1500
8. Quantity surveyor nafasi 1 watainiwa 81
9. Risk Officer nafasi 1 watainiwa 32
Nafasi zilizotangazwa unaweza kuziona >>>>>>hapa au>>>>>(NAFASI ZA KAZI NATIONAL HEALTH INSURANCE FUND (NHIF) MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAR 30 NOVEMBA 2015)
Walioitwa kwenye usaili ni hawa >>>>HAPA au hapa (KUITWA KWENYE USAILI NHIF CALL FOR INTERVIEW – 2/23/2016)

Kiroho safi wana JF hatuna budi kuwatakia watainiwa usaili mwema.
 
Hivi hao ma hr wa huko serikalini hawanaga vigezo vyao vya kupunguza watu?maana haiingii akilini nafasi 3 igombaniwe na watu zaidi ya 1700..wasiite watu kama fashion tu.
 
Wacheni watu waitwe kama una vigezo na huko vizuri utachaguliwa , je unafikiri wengeita wachache hao wanaokosa wangejisikiaje?? Je unafikiri hao walioitwa asilimia kubwa watakwenda kwenye usaili?? Na pia wengne hapo hawana vigezo wamefoji vyeti kwa hyo wakija vyeti orijino itagundulika wataondolewa, waacheni waite watu kadri ya uwezo wao ilimradi wawafanyie usaili ambao upo fair na wa wazi kwa wote
 
@ugalila,kama ushawahi kuhudhuria usaili nadhan utakua unajua,pale kwenye kukaguliwa vyeti huwa hakuna umakini,so ni easy kwa mtu kupenya,afu pia wale wakaguaji hawana vifaa vya kugundua kama cheti ni halali au feki.me nawajua weng tu wamefoji vyeti na wako huko huko serikalini.
 
Watahiniwa wa usaili zaidi ya 4000 wanatarajiwa kufurika DUCE katika mchuano wa kuwania nafasi za kazi zipatazo 46 za kada mbalimbali zilizotangazwa katika shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF). Kati ya kada zilizovunja rekodi ya watainiwa wengi kulingana na idadi ya nafasi ni pamoja na kada ya Copliance Officer ambapo nafasi 9 zinatarajiwa kuwaniwa na watainiwa wapatao 3088, ingine ni kada ya membership officer ambapo nafasi 3 zinatarajiwa kuwaniwa na watainiwa wapatao 1783. Kada zinazohusika ni hizi zifuatazo;

1. Assistant Accoutant Nafasi 8 Watainiwa 1776
2. Internal auditor Nafasi 2 Watainiwa 329
3. Claim Officer Nafasi 2 Watainiwa 600
4. Compliance and Field Officer Nafasi 9 watainiwa 3088
5. Driver Nafasi 12 watainiwa 626
6. Membership Officer Nafasi 3 watainiwa 1783
7. Quality Assurance Officer nafasi 7 watainiwa zaidi ya 1500
8. Quantity surveyor nafasi 1 watainiwa 81
9. Risk Officer nafasi 1 watainiwa 32
Nafasi zilizotangazwa unaweza kuziona >>>>>>hapa au>>>>>(NAFASI ZA KAZI NATIONAL HEALTH INSURANCE FUND (NHIF) MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAR 30 NOVEMBA 2015)
Walioitwa kwenye usaili ni hawa >>>>HAPA au hapa (KUITWA KWENYE USAILI NHIF CALL FOR INTERVIEW – 2/23/2016)

Kiroho safi wana JF hatuna budi kuwatakia watainiwa usaili mwema.
Hili ni jipu nalo lahitaji utumbuzi,Magu ona vijana wako tunavopata shidaaaaa
 
Nilishaangaika sana n interview za mashirika ya umma niliambulia tu kuwasindikiza wenzangu kuchukua ajira zao.dah!
 
Back
Top Bottom