Kuitwa kazini Law Secretary, AG office

Kuitwa kazini Law Secretary, AG office

wadadawanne

Senior Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
119
Reaction score
24
Jamani inasikitisha sana kuona watu wanatumiwa barua ya kuitwa kazini bila kutoa majina kwenye website yao, interview ya law secretary ilikuwa na utoaji wa maswali ambao ulifanywa na mzee mmoja aliekuwa anawapa watu maswali akijidai kuja na kuita jina la mtu anaemjua anafika anampa majibu na waliopewa wameitwa kazini, jaman Tanzania hii hali ya kujuana kwa kazi itaisha lini sie ambao hatuna tunaowajua ndo hatutakaa tufanye kazi??
Written test yenyewe jioni ya ijumaa watu walikuwa na test yote, haya kwa interview nayo watumishi wa secretariat wanatoa majibu kwa watu wanaowajua na hao watu wamepata hizo nafasi, mambo ya mlinde shemeji yako, tutafika kweliii!
 
duhh kumbe wameita alaf kwenye website hawajaweka ? hawa jamaa vp tena mbna wanafanya mambo ya ajab,
 
Watu wameshatumiwa barua na wameeshaanza kureport leo hii secretariati ya ajira, nimeshangaa sanaaaaa juu ya hili ila ilionekana dhahiri siku ya interview, wale wafanyakazi waliokuwa wamepangiwa makundi anakuja anamwita anamjua anajifanya Anaitwa juu wanafika. Kwenye ngazi anampa maswali na.kazi wamepata
 
Hivi watoto wasio na ndugu huko juu barua za ajira watazipataje.. Maana arghh watoto wa maskin wamebanwa kila kona
 
Pale Kuna bias kabisaaaaa, mi Sina nao imani kabisa sababu nililishuhudia hiloooo la kupewa majibu, na mtu. Anaambiwa akikisha fulani.anapata nafasi,
 
utumishi wako makini sana. mkuu wadadawanne tuhuma zako nzito sana mkuu. tunaomba uweke maelezo vizuri kama lengo lako ni zuri.
 
Last edited by a moderator:
Secret service we wasema ila mi nimejionea kwa macho yangu, si kwamba nasema nayatoa kichwani ila nimelishuhudia Ndo maana roho inaniuma saaana
 
Mdau wadadawanne hizi tuhuma zako mbona zinatia mashaka lkn, mbona huziweki vizuri ili zieleweke sawasawa lkn km ni za ukweli? Kwa sababu unaongea vitu vingi kwa wakati mmoja ukichanganya na vingine ambavyo kama ni vya kweli ulipaswa uwe ulishaviongea toka siku za huko nyuma (i.e mzee fulani kuwapa watu majibu). Kwani mashaka yako wewe ni kwa sababu uliona mzee fulani akiwapa watu majibu au mashaka yako wewe ni kwa sababu umesikia watu wamepata barua za kuitwa wkt majina kwenye website yao hawajaweka? Ebu fafanua vizuri basi mdau tukuelewe, OTHERWISE malalamiko yako yanaonekana kutokuwa na mashiko kwa sababu ya kukosa clear clarification.
 
Wewe ndio walewale
 
Inasikitisha mtu unaenda kwenye interview umejipinda kusoma wakati mwenzio tayar ana maswali ,hili swala la kupeana maswali kabla ya mtihani limeonekana katika post nyingi sio hii tu.
 
Ninayoyasema hapa ni 100%ukweli, na hoja zangu ni tatu, moja watu kuwa na maswali ya written, pili watu kuitwa siku ya interview( tena na wafanyakazi wa secretariat) waliopewa makundi ya kuita, tatu ni kwa nini wasitoe majina kwenye mtandao, km wanavyofanya wakati wa mchujo nk???? So mashaka yangu watu wanatoa wapi majibu ya written, na kwa nini wafanyakazi wa secretariat watoe maswali ya interview,na kwa nini wasiweke wazi majibu ya walioitwa kazini kwa web yao, Tosalindo malalamiko yangu yana mashikoo saaana zaidi ya unavyodhani, naomba tu mkuu wa ofisi hii awe makini kwa sababu kwa design hii ss wengine kazi tutazikia tu, na tulikuwa na imani sana juu ya uanzishwaji wa chombo hiki ila sasa naona mategemeo yetu yamekuwa kinyume
 
mkuu, mtu kupewa maswali na watu (wafanyakazi) wanaoita sio maana kapata kazi. ungeniambia wanaowafanyia usaili ndio wanapendelea maybe.. ukipewa maswali dakika 2 kabla ujaingiabkwenye chumba cha maojiano, huwezi kuongeza ata 10% ya performance yako if usingepewa.

ukiniambia mtu alipewa maswali ya written, kidogo ina make sense, coz atakua na muda wa kutosha wa kujiandaa.
 
Kupaza sauti ni muhimu na kama ni kweli itabidi wajirekebishe, lakini hii haifuti umuhimu w a kazi nzuri inayofanywa na tume hii ya ajira. Ni kweli pale kuna wafanyakazi wengi na si ajabu ukakuta kuna baadhi si waadilifu na wanavujisha maswali lakini hii haifanyi psrs kuwa ndio chombo kibaya kiasi hicho, maana kuna mashahidi wengi tu walishaandika humu kwamba wamepata kazi bila hata kumjua yeyote pale. Wapo wengine wamediriki kusema hata hawajui wamepitaje kwenye written au oral kwakuwa waliona maswali magumu bt at the end wakafaulu. Mi nafikiri cha kufanya ni kuwaambia wenye mamlaka pale wazibe mianya ya uvujaji wa maswali kama upo.
 
Jamani inasikitisha sana kuona watu wanatumiwa barua ya kuitwa kazini bila kutoa majina kwenye website yao, interview ya law secretary ilikuwa na utoaji wa maswali ambao ulifanywa na mzee mmoja aliekuwa anawapa watu maswali akijidai kuja na kuita jina la mtu anaemjua anafika anampa majibu na waliopewa wameitwa kazini, jaman Tanzania hii hali ya kujuana kwa kazi itaisha lini sie ambao hatuna tunaowajua ndo hatutakaa tufanye kazi??
Written test yenyewe jioni ya ijumaa watu walikuwa na test yote, haya kwa interview nayo watumishi wa secretariat wanatoa majibu kwa watu wanaowajua na hao watu wamepata hizo nafasi, mambo ya mlinde shemeji yako, tutafika kweliii!

acha kulalamika bila sababu,sema haikua bahati yako,jipange siku nyingine.....mdogo wangu kafanya interview hiyo na hakuna mtu yoyote tunae mjua pale wala maswali hakupewana, kapita.....sema walichokosea hawa jamaa ni kutuma barua kabla hawajatoa majina maana hata dogo alijua kakosa baada ya kusikia wenzie wanapata barua mpaka juzi alipoona majina kwenye mtandao ndio akajua amepata,kufuatilia barua imeandikwa siku tano nyuma,
 
Back
Top Bottom