Kuishi pamoja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuishi pamoja!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Apr 20, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Salamuni wandugu!


  Swali la "kama ni sawa watu kuishi pamoja bila au kabla ya kuoana" lilishaulizwa hapa jamvini zaidi ya mara moja.Kama maswala mengine tunayojadili hapa wapo waliopinga vikali na wapo waliosapoti.

  Iwe ni kwasababu wawili ndo wameamua kuishi maisha yao hivyo ama wanatumia nafasi hiyo kufahamiana zaidi wakiwa na malengo ya kuona mbeleni ikiwa wataeendelea kua kwenye ukurasa mmoja au kwa sababu nyingine yoyote ile wapingaji wengi hua wanaegemea zaidi kwenye dini.
  Ohhh kwanini uishi na mtu bila ndoa???
  Biblia inaelekeza watu kuona na sio kuishi kwa makubaliano.
  Vipi kukiuka amri za Mungu na kuzini?
  Binafsi nakubaliana na haya yote....ila kwenye maisha ya karne hii ambayo ndoa haziheshimiki wala kupewa maana na hadhi zistahilizo je ni maadili yapi hayo tunayofuata kuoana?

  Ndoa nyingi za siku hizi zimejaa unafiki ....Unakuta baba ana nyumba ndogo....mara sijui katembea na dada wa kazi mpaka kumpa mimba...mama nae ana kakijana kake mtaa wa pili basi tunachoona na kutambua kama usahihi na unyoofu wa maisha kinageuka uozo.Sasa je tunapozipigia debe ndoa hizi hizi ambazo yanayofanyika ndani yake hayaelezeki na kusema au hata kufikia kuwahukumu wale wanaishi pamoja bila hizo ndoa tunakua tunamdanganya nani haswa???Sisi wenyewe na nafsi zetu au muumba wetu tunaejifanya tunafuata na kutimiza maandiko yake kwa kuoana????

  Japo sisemi watu wasiendelee kuoana ila tukumbuke kwamba mtu anapooa au kuolewa hafanyi hivyo ili aonekane na ukoo...kanisa...msikiti..au majirani bali kwaajili yako mwenyewe....kwahiyo tusijidanganye kwa kuuridhisha umma huku nafsini tukijua kinachoonekana sicho. Watu wawili ambao hawajaoana mbele ya umati na kupigiwa vigelele ila wakawa wakweli na waaminifu ndani ya nafsi zao wenyewe ni bora kuliko ndoa zinazohalalishwa kwa matarumbeta zikisindikizwa na maneno ya vitabu vya dini wakati wanaoingia ndani yake si mioyo wala akili zao zilizopo kwenye hizo ndoa.

  Usihukumu usije ukahukumiwa...haswa ukiwa unajua unayofanya wewe japo watu wengine wanaweza kua hawajui ni mabaya kuliko unayohukumu. Uaminifu na uzuri wa kweli ni ule unaouona wewe hata kama wengine hawaoni.....
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hata mkiiishi kwa muda ili muweze kufahamiana bado hamtafahamiana kivile, sema tu humu ndani tunaona vitimbi vingi coz tumeshajifunga pingu na kwa wengine kujitoa kwao ndio hivyo wanahofia jamii/watoto etc lakini ishu ya vimbwanga vya ndoa vinaweza kutokea hata mkiamua tu kuishi bila ndoa ila hapo inakuwa rahic kwa mmoja wao kama kazidiwa kujiengua na kuendelea na maisha yake japo kuna muda kwa sheria kwamba mkiishi pa1 kwa muda fulani mnatambulikana kama mume na mke....nadhani ningekuwa cpo ndani nicngeingia kwa ndoa wala bila ndoa, ningejizalia tu nilee nitulie..pwehh ote ndao.
   
 3. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  " wanaume wote wamezaliwa na baba mmoja na mama mmoja" kwa maana karibia wote tabia zao zinafanana.

  ngoja hembu tusikie watakavyosema!! wasije nitoa macho bureeee!!!!
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hii imenigusa nitarudi ngoja nivute pumzi.

  Hujambo lakini wewe??? (Jamaa ana raha kweli niko hapa almost three weeks full kujiachia)
   
 5. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Unachokoza nyuki halafu muoga eehhhh?????
   
 6. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Aiseee, we mwanamke mi nachomoka zangu!
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kingine ni kwamba ni ngumu sana kumtambua mwenzi wako kabla hajaishi pa1, iwe ndoa/kuishi bila ndoa yote sawa, mkianza kuishi pa1 kwa namna moja au nyingine ndio huwa tunayatoa makucha ye2, so hapa ishu ni kwamba hiyo ya sogea tuishi ni nzuri nayo kama mna malengo ya kujuana zaidi bila kuanzia familia(watoto) mkianzisha familia tayari mtu kama huyo atakuwa kama kina sie tu hapa.....
   
 8. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ha hahaaaaaaa uwiiiiiiiiiiii!!! dada Dena ww si ndio mtetezi wangu!!!!!!!
   
 9. The Kop

  The Kop JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 208
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  ndoa hufungwa mioyoni mwa wawili wapendanao...haya matarumbeta ni mbwembwe tu za watu wa magharibi...hata ktk vitabu vitakatifu sijaona mahali watu walienda sijui kwa shekhe au mchungaji kwa ajili ya kufungishwa ndoa...cha muhimu ni wawili kuridhiana na baraka za wazazi...ful stop...!
   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Wewe BE hujamuona sehemu unasema live hivi hebu usinitafute ubaya na laazizi wangu tafadhali eehhhh ha ha ha h
   
 11. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ngoja nikafanye rejea zaidi kwenye biblia
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  za cku hizi?....
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa faida moja wapo ni kwamb ani rahisi kila mtu kuendelea na maisha yake ikiwa mtashindwana!!

  Heheheheh....labda hiyo sheria nayo ingepitiwa kidogo maana ni sawa na kufungishwa ndoa bila kutaka na sometymzz bila kujua maana kuna watu wakati wa kuachana ndo wanaambiwa ''kisheria wewe ni mume wangu ujue...embu gawa mali hizo''!
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa bibie mbona unawaonea watoto wa watu???Kama ni kwa tabia mbaya mbona hata sisi karibu tutawafikia!!Usikute wote tulizaliwa na mtu mmoja...aliyetulea tu ndo mwingine!
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ushamaliza kuvuta pumzi mami???
  Kama ni hali yangu unaulizia sasa hivi napumua kama kawaida!!Heheheh ( shemeji shemeji nirudi kumpenda au niendelee kumchukia mpaka uniambie?? )
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red kwanini Nyamayao???Binafsi sidhani kama kuna kifungo ambacho kinaweza kuniweka kwenye mahusiano nisyoyafurahia!!Kama ni mtoto tutalea pamoja kwa makubaliano au ikibidi ntamlea mwenyewe. Unaweza ukavumilia misuko suko ''ili mtoto alelewe na wazazi wawili'' ila mwisho wa siku unakuta wewe tu ndo mlezi au zaidi mwenzako anakua kwenye kuharibu zaidi ya kumjenga mtoto. Ubaya ni kwamba kuna nafasai kubwa sana ya mwanaume ambae anamnyanyasa mwanamke kunyanyasa na mtoto pia...asipokujali wewe ambae humhitaji akulishe na kukuogesha atamjali vipi mtoto ambae anamhitaji kwa kila kitu?
   
 17. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  aaaaahhh Lizzy watoto wa watu?? wakina na nani? wanaume? subutu yake!!!!!!!

  ngoja nitoke maana naona nataka kuwaka!!!
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Ya yule mtu muache kama alivyo mara yes mara no si ndo kama hivyo tena unajua bana acha kunivizia.

  Hili linahitaji niwe nimetulia sana nitapost nikiwa home nimetulia
   
 19. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  mimi naamini ukipata ubavu wako ambao mungu ndio aliokupangia, hata awe na tabia zipi au mpate misuko suko vipi mtaishi mpaka kifo kiwatenganishe. Tatizo ndoa za siku hizi ni za kulazimisha
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hukunipata vzr my dear, nimesema kama kina sie nikimaanisha tayari mtakuwa na familia bac ndio ndoa hapo, so mtakuwa hamjafanya lolote kubadili tuliopo ndani/wasiopo ndani, ndio nikasema labda wa kuishi ili kujuana muishie kujuana mkianza familia bac ndio tunakukaribisha kwenye club hivyo...hiyo blue, maneno mazito hayo, very well said my dia...sio wote tunaweza kuvumilia hayo manyanyaso, so wengine bado hayajatuzidi but yakituzidi tutajisogeza tulee wenyewe,kwangu mie inapokuja ishu ya watoto wangu huwa cna mzaha na mtu....
   
Loading...