Kuishi na Mwanamke.....Sheria inasemaje?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuishi na Mwanamke.....Sheria inasemaje??

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Sajenti, May 4, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sheria inasemaje inapotokea mwanaume ameishi na mwanamke kwa kipindi cha mwaka na wakazaa mtoto? Uhusiano wao hapo awali ulikuwa ni wa kirafiki zaidi kwani watu hawa hawakufunga ndoa ya aina yoyote. Baada ya mwaka huo mmoja uhusiano huo unavunjika na mwanamke anaondoka na kwenda kufungua kesi akidai kupata mgao wa mali iliyopatikana katika kipindi cha mwaka huo mmoja walioishi na mwanaume. Je, sheria inasemaje katika hili?

  Kuna uwezekano wa mwanaume kuamua kufunga ndoa na mwanamke kwa mkataba wa kipindi maalumu kama vile miaka 5 au 10 na baadae ndoa hiyo kufikia kikomo baada ya muda uliokubaliwa kwisha?? Naomba wataalamu wa sheria mnipe darasa hapo.
   
 2. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,032
  Likes Received: 564
  Trophy Points: 280
  Sajenti kweli wewe mwanajeshi unataka uishi na mwanamke umtumie na kumchakaza halafu umbwage. Kaka hakuna kitu kama hiyo bahati mbaya sio mwanasheria muda siujui
   
 3. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanza sheria ya ndoa ya Tanzania inatamka wazi kuwa ndoa ni muungano wa mwanamke na mwanaume kwa hiari yao kwa maisha yao yote. Hii ina maana kuwa katika sheria yetu wanandoa hawatakiwi kuachana na mnapo dhamiria muungano huu mjue kuwa ni mpaka mmoja awe amefariki. Lakini kuna mazingira mengi ambayo sheria imeelezea ambayo yanaweza yakafanya muungano huu ambao ulitegemewa uwe hadi mmoja atakapofariki uvunjike kabla ya wakati huo. Hivyo basi Tz hatuna ndoa ya mkataba wa miaka hiyo uliyosema kaka. Ukiingia kwenye mkataba wa ndoa ni mpaka mmoja afe. Au uwe na sababu za kutosha kuishawishi mahakama iweze kutengua ndoa hiyo. Pia ukikaa na mtu kwa muda wa miaka miwili mfululizo kwenye nyumba moja na watu wote waliokuzunguka wakaamini kuwa kukaa kwenu pamoja ni kama mume na mke sheria inamtambua huyo mwanamke ni mke na wewe ni mume ila sheria hii ni "rebuttable" yaani mmoja wenu anaweza akathibitisha vinginevyo na mahakama ikaamini kuwa sio mume na mke, na kuamua suala la matunzo ya mtoto kama mtoto huyo ni wakwenu wote. Na kila mtu akaenda kivyake vyake. Na mgao wa mali mlizochuma kwa kipindi hicho kila mmoja itabidi aishawishi mahakama kama ana haki nayo. Ikimaanisha mkataba kama upo wakati mkichuma hiyo mali. Au nani ana nini kwa kuthibitisha kutokana na risiti mlizokuwa nazo na mambo mengi ndio itaamua na ana haki na kitu kipi au kwa kiasi gani katika mali hizo.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Kweli we Bazazi , kwani kwenye ndoa kuna anayemtumia na kumchakaza mwenzie au tuko katika kutimiza mambo yaliyo wazi hata kwenye katiba mazee??? Sorry mkuu naomba ushauri wako basi ni muhimu sana....achana na mambo ya kuchakazana hayo ni matumizi ya kawaida tu!!!
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kwa nini uingie kwenye ndoa kwa lengo la kuivunja baada ya miaka 5 au 10?
   
 6. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli kaka na mimi natamani kujua hilo....ni baada ya kuishi pamoja kwa muda watu huhesabiwa mke na mme kisheria?
   
 7. T

  Tall JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kutokana na sheria ya ndoa na talaka ya 1971 as ammended,''ukiishi na mwanamke zaidi ya miezi sita mfululizo huyo ni mkeo'' ANA HAKI ZOTE.mpe haki zake(mali)
  Haya mambo muhimu kuyajua sio mpaka uwe mwanasheria vinginevyo andika UMEUMIA
   
 8. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kama alivyosema Mapondela, sheria yetu ya Ndoa ya mwaka 1971 haitambui ndoa za mikataba, tafsiri ya ndoa iliyotolewa na mkuu hapo ni sahihi kabisa, lakini napenda kuongezea kitu kidogo ili watu waelewe vizuri, kuna kitu kinachoitwa dhana ya ndoa (pressumption of marriage) ambapo ili hii iweze kutumika ni lazima wahusika wawe wameishi pamoja kwa muda usiopungua miaka miwili na jamii yote inayowazunguka iwe imewajengea dhana kuwa wao ni wanandoa, matumizi ya dhana hii yanakosewa na wengi sana, baadhi ya watu wanafikiri kuwa ukikaa ma mwenzi wako kwa muda wa miaka miwili basi nyie ni wanandoa, haipo hivyo kwani ingelikuwa hivyo basi sheria ingekuwa inarasimisha mahusiano yasiyo rasmi, kifupi tu ni kwamba ili watu mtambulike kuwa ni wanandoa ni lazima mfunge ndoa inayotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.
  Dhana hii ya ndoa huwa inatumika tu kumlinda mwenzi mmoja ili asipoteze haki yake ambayo angestahili kuipata kutokana na kuishi na huyo mwenzake kwa muda wote huo walioishi, kwa hiyo si ajabu mtu akaenda mahakamani na ku-base madai yake kwenye dhana ya ndoa na bado akashindwa madai yake.
   
 9. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Naomba kuuliza hivi hii sheria ilitungwa na wanawake? kwa nini isisomeke hivi "ukiishi na Mwanaume zaidi ya miezi 6 huyu ni mumeo" mpe haki zote.!??
  kwanini ni MWANAMKE TU.? JE madume hayana haki zao?
  mnaojuwa sheria palipozungumziwa wanaume hebu wekeni wazi manake siku hizi kuna wanawake kama madume vile.!
   
 10. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
   
Loading...